Hatuchukii udikteta, tunachukia tunapofanyiwa sisi

IslamTZ

JF-Expert Member
Nov 22, 2010
309
182
Leo nimepitia makala iliyopo mtandao wa Chanzo ikijadili malumbano yaliyojaa matusi, kashfa na kudhalilishana kati ya Chadema na ACT. Inapatikana HAPA

Aya moja inasema: "Lakini katika hali ambayo haikutarajiwa na wengi, mnyukano huu wa maneno kati ya makada wa ACT-Wazalendo na CHADEMA uligubikwa na ukosefu mkubwa wa ustaarabu, huku nafasi ya ushawishi wa nguvu za hoja ikichukuliwa na kauli za kibaguzi, matusi, kashfa, na kudhalilishana."

Hitimisho langu:

1. Awali, hatuchukii udikteta wala hatuipendi sana demokrasia. Yote haya yanategemea tumesimama wapi. Demokrasia ikitufaidisha, twaipenda; kama haitufaidishi nasi twawa madikteta tu. Udikteta pia hatuupendi tukifanyiwa lakini tukiwafanyia wenzetu, poa. Twataka uhuru wa kujieleza lakini wengine wakiutumia kusema tusiyoyapenda, inakuwa nongwa!

2. Pili, udikteta uko katika vinasaba vyetu Waafrika, au sijui tuseme ni utamaduni wa kichifu tumerithi? Lakini kujenga demokrasia inabidi tufundishe watoto kuanzia utotoni tabia ya kuvumilia, ustaarabu wa kujadiliana bila kutukanana.
 
Back
Top Bottom