John Mnyika
JF-Expert Member
- Jun 16, 2006
- 712
- 1,240
- Thread starter
- #441
Hivi Mhe. John Mnyika mimi nina swali hili,
Hivi kipindi kile watu tunashuhudia matusi makubwa tena mengine ya ndani kabisa yakivurumushwa fcbk na vijana wenu kama Mtela Mwampamba, Juliana Shonza co kwenda kwa viongozi wakuu wa chama, Mlikuwa wapi kukemea tabia ile? Au mlisubiri kwanza Ben Saanane aje kulianzisha na nyie ndo mfate? Pia kwanini zitto kwenye nyaraka mbalimbali ambapo sehemu ya kujaza chama yeye huwa anajaza" KIGOMA KASKAZIN" inamana mnataka tuamin CHADEMA kila mtu anajivua eneo analotoka na sio chama.?
Shardcole,
Nashukuru. Naomba urudie tena kusoma katikati ya mstari mchango wangu wa kwanza utabaini kuwa kabla hata ya tuhuma na shutuma za sasa kutolewa JF tayari chama kilishaanza kuchukua hatua kuhusu baadhi ya wanachama kuchafua viongozi kwenye mitandao ya kijamii na njia nyingine za mawasiliano.
JJ