Hatua zinaendelea kuchukuliwa kuhusu tuhuma na shutuma zilizotolewa

Hapa Ben huenda akawa umeuvaa mkenge. Ila nimemtahadharisha ajaribu kumconsult kamanda Lissu! Ningeweza kukupa mfano wa kuprint screen na kuipaste hapa lakini inagoma. Ila umenipata. Good idea kwa JF ingawa huenda ikawa ngumu to implement.

Rusha PM kwa Invisible for the implementation.thanks! ndio maana ya JF pamoja tutashinda.
 
Tangu sakata la masalia PM7 lianze, mimi nimekuwa na mawazo tofauti na wengi wanaounga na wasiounga mkono. Baada ya kufuatilia kwa makini, nimegundua kwamba hakuna mgogoro/mpasuko ndani ya Chadema kama chama bali upo mgogoro ndani ya masalia PM7. Kundi la masalia kama lilivyokuwa mwanzoni limepata pigo kwa kukimbiwa na wanachama wake wawili na kusababisha mgogoro/mpasuko mkubwa ndani yake hadi mambo mawili makubwa yakafanyika;

  1. Uwanja wa usaliti kuhamia JF ukitokea FB.
  2. Majina halisi ya masalia kujulikana.
Ugomvi unaoendelea hivi sasa ni kati ya masalia wanaotaka kuendeleza mipango yao ya awali na masalia wenzao ambao wameamua kutubu na kufichua siri. Masalia wale wa mwanzo wanalalamika wenzao wamewasaliti kwa kukiri ushiriki wao kwenye mbinu ya kuichafua Chadema na uongozi wake. Kundi la Masalia linasambaratika na sasa tunachoshuhudia ni kile kinachoweza kufananishwa na the last kicks of a dying horse!...Kama ilivyo siku zote masalia wanataka wafe na mtu but what a miscalculation! Yaonekana baada ya kuondokewa na vichwa vilivyobaki ni viwiliwili tu...Ben Saanane umewaacha akina Ritz yatima!

Mag,

Shukrani. Kwa maana rahisi mgogoro ni mchakato ambao kila upande una matakwa yake na unaona upande mwingine unakwenda kinyume na matakwa hayo na kufanya vitendo vya kuhujumiana; mgogoro ni kipeo cha kutokuelewana na kutokubaliana kwa kiwango cha kukabiliana. Migogoro mara nyingi huwa na athari na taathira hasi lakini wakati mwingine huleta matokeo chanya.

Baadhi ya wanazuoni wa nadharia ya taasisi (organizational theory) wanagawa migogoro kuwa ya aina kuu tatu: mahusiano, michakato/mifumo na majukumu. Haya masuala na matukio ya wanachama wachache kutuhumiana na kushutumiana yanahusu migogoro yao wenyewe, huwezi kuyaita kwamba CHADEMA kama taasisi ina mgogoro au mpasuko mkubwa.

Migogoro ya yenye athari kubwa kubwa kwa taasisi kama chama ni ile iliyojikita katika michakato/mifumo hata kama imetokana na mahusiano.Ni vyema pia kutenganisha kati ya matukio yenye athari na taathira kwa wanachama wachache au ngazi Fulani ya uongozi wa chama na CHADEMA kama taasisi badala ya kutoa tu hitimisho la ujumla.

Hii itawezesha kutofautisha katika ya tuhuma au shutuma na matokeo ya kuchukua hatua dhidi ya utovu wa nidhamu kwa lengo la kusimamia maadili kwa upande mmoja na migogoro au mipasuko kwa upande mwingine.

JJ
 
Iwe itakavyokuwa na hakika kwa JJ umenena. Baada ya Dr. sidhani kama kuna mtu mwadilifu mwingine zaidi yake. So far hajakubali kununuliwa na hana makundi. Ila pia kwa 51 years of independence mmefanya nini unaposema eti CDM bado haijaweza kushika dola? Nyerere marehemu baba yetu naye alikuwa na pa kuanzia na CDM vivyo hivyo.
binafsi namkubali MNYIKA sana tu na anakubalika na wengi wetu tusiopelekwa na siasa za makundi.
kuhusu madaraka ya adola kwa cdm itasubiri kidogo ila kuongeza idadi ya wabunge nataka itokee hata kesho ili kuipa serikali adabu na heshima ya uwajibikaji.
 
Nimekupata mkuu gfsonwin. Xmass njema, Hope, we shall meet at our mkeka before the New Year, 2013. Hili ni keka letu la kupanua akili na kujifunza.
 
Nimetahadharisha tu. Unaweza kuwa upande wa mlalamikiwa ukatoa utetezi wako. Kuna kauli kwenye post akisema; Jaji anaamuru tuzme simu zetu, lakini mimi nakaidi kwa manufaa ya umma. Ni mfano tu.
Ila kumbuka kuna msemo wanasema 'ukijua huu huu huujuwi'.

Acheni kuhamisha mijadala kipuuzi mtu mwenyewe hata sheria ujui na wanaojua wanakushangaa tu unavyotema pumba humu.
 
aah ha haaa! we sepa tu unasubiri nini, chama makini hakihitaji wanachama viazi kama wewe- nje kinajidai kimepoa kumbe ndani cha motooo! wewe ushaambiwa katiba ya chama inatakaje kuhusu masuala kama hayo, kuna taratibu inabidi zifuatwe, je zilifuatwa au zilikiukwa? mi sijui ni kitu gani huelewi!

Achana naye, huyo ni CCM through and through ila tu kwa vile uongo na unafiki ni sifa mama kule CCM ndio huja na undumilakuwili wake hapa.

No room for masalia either
 
ndugu yangu mnyika, kinachonipa utata kila uchwao juu ya CDM ni hili hapa

ilitumika nguvu nyingi sana kuiweka CDM hapa ilipo na wakati nguvu hii inatumika kuna baadhi ya wa vijana walikuwa kimya hatukuwasikia kabisa.

je kwann vijana hawa watake kufifisha juhudi za wenzao?? na je kwann chama kiongelewe mambo yake kwenye mitandao ya kijamii kuliko kujadiliwa katika vikao husika vya chama?? je ni kwamba baadhi ya hawa viongozi wa BAVICHA hawakujua sheria ama kanuni za chama??

katika organization management good coordination ni jambo la msingi sana na hata hiyo proper accountability sasa je ni wapi ambapo coordination ilisuasua hadi kufikia hapa ama accountability ya responsible person ililega??
 
Vumbi tu! Mlikuwa wapi muda wote? Matatizo lukuki, nazidi kusisitiza uongozi ni tatizo, kaka angalia nawe usije ukawa mojawapo ya tatizo kwa sababu tayari press yako iko biased kwamba "viongozi wamekashifiwa". Hao wanatakiwa kujibu tuhuma na kila mmoja ana haki kidemokrasia kutaja maonevu, mfano Dr Slaa kuwa na kadi ya CCM ambako mimi siafiki ni kashfa?

Sana sana, kama hamna kitachotamkwa kuhusu kadi mi najitoa CDM na wewe mwenyewe utakosa kura yangu.

Vipi umesha chukua ya magamba tayari maana naona CDM hakukufai....
 
Hahahahahahahahaha
Bado uja nihakikishia kama unaelewa kiundani mantiki ya kuzima simu mahakamani!

Hapa Ben huenda akawa umeuvaa mkenge. Ila nimemtahadharisha ajaribu kumconsult kamanda Lissu! Ningeweza kukupa mfano wa kuprint screen na kuipaste hapa lakini inagoma. Ila umenipata. Good idea kwa JF ingawa huenda ikawa ngumu to implement.
 
Mhe. Mnyika,

Nashukuru kwa mwangaza huu. Bila shaka masalia nao wamepata elimu hii. Nadhani CDM ipo salama, kilichobaki ni hawa wanachama (PM7) waliotoa hizi tuhuma nzito dhidi ya Dr. Slaa kuitwa ndani ya vikao halali vya maamuzi vya chama kwa ajili ya mahojiano na maamuzi. Hakuna cha ziada.

kumbe hata masuala ya EPA tuwaulize tu wahasibu wa BOT ambao ndio wawe responsible.
Hapa kwamjibu wa TUNTE mradi ulikua bado uko chini ya slaa.sasa kama yeye amecheza deal na DED wa karatu sasa hizi shutuma zitawahusu wote wawili.
 
Hapana mkuu wangu Pasco. Najua mbali ameshafika ndio maana kwa kanuni za kudumu za bunge zinalazimisha aitwe kwa kutanguliza neno Mhe. Sala yangu ya kufika mbali ni katika yeye kuendelea kututumikia zaidi. Si wanaubungo na CHADEMA tu bali watanzania kwa ujumla na hili liko wazi kwa wapenda maendeleo wa Tanzania.

Suala la kupokezana vijiti, hilo litategemea na utashi wake, chama chake pamoja na usaili mbele ya wananchi ambao ni pamoja na mimi na wewe!
Angalia usimponze tusibakishe hata panya huko nyumbani kwake!.
 
Hivi Mhe. John Mnyika mimi nina swali hili,
Hivi kipindi kile watu tunashuhudia matusi makubwa tena mengine ya ndani kabisa yakivurumushwa fcbk na vijana wenu kama Mtela Mwampamba, Juliana Shonza co kwenda kwa viongozi wakuu wa chama, Mlikuwa wapi kukemea tabia ile? Au mlisubiri kwanza Ben Saanane aje kulianzisha na nyie ndo mfate? Pia kwanini zitto kwenye nyaraka mbalimbali ambapo sehemu ya kujaza chama yeye huwa anajaza" KIGOMA KASKAZIN" inamana mnataka tuamin CHADEMA kila mtu anajivua eneo analotoka na sio chama.?
 
Last edited by a moderator:
Kweli CHADEMA wanapaswa kujua watu hawa na kupeleka na sio wengine wanajenga na wengine wanabomoa na hivyo kuna haja ya malalamiko yote kupelekwa kwa chama
 
Mag,

Shukrani. Kwa maana rahisi mgogoro ni mchakato ambao kila upande una matakwa yake na unaona upande mwingine unakwenda kinyume na matakwa hayo na kufanya vitendo vya kuhujumiana; mgogoro ni kipeo cha kutokuelewana na kutokubaliana kwa kiwango cha kukabiliana. Migogoro mara nyingi huwa na athari na taathira hasi lakini wakati mwingine huleta matokeo chanya.

Baadhi ya wanazuoni wa nadharia ya taasisi (organizational theory) wanagawa migogoro kuwa ya aina kuu tatu: mahusiano, michakato/mifumo na majukumu. Haya masuala na matukio ya wanachama wachache kutuhumiana na kushutumiana yanahusu migogoro yao wenyewe, huwezi kuyaita kwamba CHADEMA kama taasisi ina mgogoro au mpasuko mkubwa.

Migogoro ya yenye athari kubwa kubwa kwa taasisi kama chama ni ile iliyojikita katika michakato/mifumo hata kama imetokana na mahusiano.Ni vyema pia kutenganisha kati ya matukio yenye athari na taathira kwa wanachama wachache au ngazi Fulani ya uongozi wa chama na CHADEMA kama taasisi badala ya kutoa tu hitimisho la ujumla.

Hii itawezesha kutofautisha katika ya tuhuma au shutuma na matokeo ya kuchukua hatua dhidi ya utovu wa nidhamu kwa lengo la kusimamia maadili kwa upande mmoja na migogoro au mipasuko kwa upande mwingine.

JJ

JJ
Kukuza, kupotosha na kulaghai ndio kazi/ajira kwa wapinzani wenu. Wameshindwa hata kutekeleza maazimio yao waliyojiwekea wenyewe na mbaya zaidi wameshindwa hata kujifanyia tathmini (evaluation).

Pigeni kazi makamanda, hawa wakorofi wachache wasisababishe shughuli muhimu kusimama.

Ni ulevi wa sifa, uroho wa madaraka na tamaa ya mali ndio tatizo la PM7. Hivyo sisi wazalendo wa nchi hii tunasubiri na tutawapa support ktk mchakato mzima ili haki itendeke na ukweli kamili ujulikane. Of coz, kuna wengine wamo ktk hizi hujuma ila tu majina na roles zao bado kuwekwa bayana sasa.
 
Vumbi tu! Mlikuwa wapi muda wote? Matatizo lukuki, nazidi kusisitiza uongozi ni tatizo, kaka angalia nawe usije ukawa mojawapo ya tatizo kwa sababu tayari press yako iko biased kwamba "viongozi wamekashifiwa". Hao wanatakiwa kujibu tuhuma na kila mmoja ana haki kidemokrasia kutaja maonevu, mfano Dr Slaa kuwa na kadi ya CCM ambako mimi siafiki ni kashfa?

Sana sana, kama hamna kitachotamkwa kuhusu kadi mi najitoa CDM na wewe mwenyewe utakosa kura yangu.
kama kweli upo CHADEMA basi uondoke tu mapema maana watu wa aina yako ni hatari kwa harakati za ukombozi
Wewe mpe salamu nduguyo nape mwambie mapambano yanaendelea!
 
@Gfsonwin, natofautiana nawe katika hili la CHADEMA kutoweza kuchukua dola kwa kuwa inahitaji muda zaidi. Watanzania katika sehemu kubwa ya nchi yetu wameikubali CHADEMA na ndio maana katika uchaguzi wa 2010 CHADEMA ilipata kura nyingi sana katika nafasi za Wabunge na Urais na hivyo magamba kwa kupitia vyombo vya dola wakaamua kuchakachua matokeo katika majimbo mengi nchini ili kuweza kubaki Ikulu na pia kuwa na idadi kubwa ya Wabunge.

Mkuu nakuhakikishia kama uchaguzi wa 2015 utafanyika kwa kutumia katiba mpya ambayo itakuwa imekubaliwa kihalali na Watanzania walio wengi na uchaguzi huo kuwa wa haki (free and fair election) basi magamba hawana chao katika uchaguzi huo nao wanajua hivyo. Ndio sababu wanatumia vyombo vya dola kuleta machafuko katika kampeni mbali mbali za CHADEMA zinazofanyika nchini ambapo baadhi ya machafuko hayo yamesababisha umwagaji damu na baadhi ya Watanzania kupoteza maisha yao.

CHADEMA kiko tayari kuchukua dola hata hii leo na Watanzania wengi tutafurahia sana uongozi wa CHADEMA katika kuboresha maisha ya Watanzania walio wengi kwa kutumia utajiri mkubwa ambao nchi imejaaliwa na hivyo kuleta maendeleo ya kweli nchini.

sio kwamba ccm inahaha juu ya cdm inajulikana wazi kwamba cdm itaongeza idadi ya wabunge hatua ambayo mm binafsi nitaiunga mkono na kuipongeza ila haitaweza kuchukua dola. tuache siasa za ushabiki bado CDM inahitaj muda ili kuongoza dola. serikali ama nchi sio nyumba ama familia ya mtu useme utaongoza kwa mawazo ya watu wenye dira ndogo la hasha.

na mark ma words atakaye kuja kugombea urais kwa ticket ya cdm na kupata kama CDM ikiwepo madarakan basi ni ndugu MNYIKA. kama utakubaliana na mm
 
Now I'm starting to believe that 'Operation chaos' is kind of working.

But what doesn't kill you can only make you stronger.

So hopefully CHADEMA will be able to ride out the storm.

Ila kilichonishangaza na kunisikitisha (na sijui hata kwa nini nimeshangaa na kusikitika) ni hayo mambo ya ushirikina.

Yaani "vijana" tena ambao tunaambiwa ni "vichwa" (whatever the hell that means) na "wasomi" wanatuhumiana mambo ya kula viapo mbele ya waganga wa kienyeji?

Nachoka kabisa!
 
Back
Top Bottom