Hatua zinaendelea kuchukuliwa kuhusu tuhuma na shutuma zilizotolewa

John Mnyika

JF-Expert Member
Jun 16, 2006
712
1,240
Tangu wanachama wachache wa CHADEMA walipoanza kutuhumiana na kushutumiana kupitia JF watoa maoni mbalimbali mmetoa mwito kwa chama kuchukua hatua na wengine mmehitaji majibu kutoka viongozi wengine na kwangu kuhusu hali hiyo iliyojitokeza.

Ifahamike tu kuwa mara baada ya tuhuma na shutuma hizo kuandikwa nimewasiliana na baadhi ya wahusika waliotumia majina yaliyothibitishwa (verified users) ili wawasilishe maelezo navielelezo vyao kwa chama ili hatua ziweze kuchukuliwa. Nimechukua hatua hiyo kwa kuzingatia katiba ya chama ibara ya 5.3 na Kanuni za chama 7.7.5, Maadili yachama 10.0 Itifaki ya chama 12.0.

Aidha, nimewasiliana pia na uongozi wa BAVICHA ili waweze kuagiza viongozi na wanachama wake waliohusika watimize wajibu huo kwa mujibu wa kanuni za kuongoza Baraza la Vijana wa CHADEMA kwa kuzingatia pia katiba, kanuni, maadili na itifaki ya chama.

Pamoja na kusubiri maelezo na vielelezo toka kwa waliotakiwa kuwasilisha, ifahamike kuwa hata kabla ya kuandikwa kwa tuhuma na shutuma za hivi karibuni zilizotolewa na wanachama wenye majina yaliyothibitishwa, chama (kupitia Kurugenzi ya Ulinzi naUsalama) kilishaanza uchunguzi kuhusu madai ya kuwepo kwa baadhi ya wanachama wenye kukichafua chama na viongozi wake katika mitandao ya kijamii na njia nyingine za mawasiliano.

Aidha, ushushushu umekuwa ukiendelea kufuatilia nyendo za wapinzani wa nje ya chama zenye mwelekeo wa kuhujumu kwa kutumia mbinu haramu vuguvugu la mabadiliko nchini linalohamasishwa na CHADEMA.

Hivyo, maelezo na vielelezo vitavyowasilishwa vitashughulikiwa pia kwa kuzingatia ripoti za uchunguzi huo na hatua stahiki kuchukuliwa kwa watakaothibitika kukiuka katiba,kanuni, maadili na itifaki ya chama na pia maamuzi ya ziada yatafanyika juu ya wahujumu wa mabadiliko nchini watakaobainishwa.

Kwa mliohoji kuhusu matakwa ya kanuni za CHADEMA kuhusiana na tuhuma na shutuma zilizojitokeza nawashauri mrejee sura ya kumi ya Kanuni za Uendeshaji Kazi za Chama hususan kifungu cha 10.0 kinachohusu Maadili ya Viongozi, Sifa mahususi za Viongozi na Maadili ya wanachama.

Maadili ya CHADEMA yanakataza kiongozi kutoa tuhuma zozote dhidi ya viongozi wenzake pasipo kupitia vikao halali na kuzingatia taratibu na ngazi zilizoelekezwa kwenye kanuni za chama. Ni marufuku kwa kiongozi wa CHADEMA kukashifu chama, kiongozi na mwanachama yoyote na viongozi wanapaswa kutofautisha kati ya kashfa na ukosoaji wa kisiasa.

Ni kinyume pia na maadili ya CHADEMA kwa mwanachama kufanya upinzani dhidi ya chama na kujihusisha na makundi ya majungu ya kuchonganisha viongozi na wanachama. Badala yake mwanachama anapaswa kuwa mwanaharakati wa kweli katika kutetea maslahi ya chama na jamii kwa ujumla kwa kuzingatia madhumuni, itikadi na falsafa ya CHADEMA.

CHADEMA imekuwa na kawaida ya kuchukua hatua dhidi ya utovu wa nidhamu kupitia vikao vyake na vyombo vyake vya kikatiba hivyo natoa rai kwa wanachama na watanzania wote wanaounga mkono mabadiliko kuwa wavumilivu na wastahimilivu ili hatua hizo zichukuliwe misingi ya haki na ukweli.

CHADEMA inaendelea na dhima yake kuleta uongozi bora, sera sahihi, mikakati makini na oganizesheni thabiti kwa maendeleo endelevu; masuala na matukio yanayojitokeza dhidi ya dhamira hiyo yachukuliwe kama changamoto katika kazi ya kuwezesha vuguvugu la mabadiliko.

Kwa sasa kipaumbele ni kusimamia maamuzi ya kamati kuu iliyomalizika karibuni kwa kurejea pia mikakati na mipango ambayo chama kinaendelea kuitekeleza ya kuwaunganisha watanzania kwa falsafa yake ya “Nguvu ya Umma” mpaka kieleweke.

JJ
 
Tunategemea kamati husika itatenda haki kwa wote waliohusika.Naamini haya yatakuwa maamuzi magumu kuliko yote yaliyopatwa kuamuliwa na chama.
 
Asante sana Kamanda kwa taarifa. Tuna imani na nyie makamanda wetu.
 
Hao watu wajinga kabisa, hata kama wakikana kimaneno matendo yao yalishakubali kabla, na tuliwajua kwa matano yao ili vinywani mwao walionekana kukana. Licha ya kuonekana kwa maneno kuwa wanaipenda CDM ila kwa vitendo wameonekana kabisa ni wasaliti na wabinafsi. Kuwajua tuu ni hatua nadhani imetosha tusipotezze muda wa chama.
 
Tunasubiri kwa hamu kuona Chama imara cha CDM kikichukua hatua stahiki kwa wahusika bila huruma ya aina yoyote, maana ukimchekea nyani utavuna mabua.
 
Vumbi tu! Mlikuwa wapi muda wote? Matatizo lukuki, nazidi kusisitiza uongozi ni tatizo, kaka angalia nawe usije ukawa mojawapo ya tatizo kwa sababu tayari press yako iko biased kwamba "viongozi wamekashifiwa". Hao wanatakiwa kujibu tuhuma na kila mmoja ana haki kidemokrasia kutaja maonevu, mfano Dr Slaa kuwa na kadi ya CCM ambako mimi siafiki ni kashfa?

Sana sana, kama hamna kitachotamkwa kuhusu kadi mi najitoa CDM na wewe mwenyewe utakosa kura yangu.
 
Kwasabubu tuhuma hizi zinawahusu baadhi ya watu wazito ndani ya chama naomba isije ikawa kama ile ya ccm na kujivua gamba.
 
Asante Mnyika,angalizo tu hatutegemei haya mambo yachukue muda mrefu na blah blah nyingi.Watuhumiwa wote wamesema wanaushahidi hivyo hilo si suala la kusubiri mwezi ni within 48hrs enough!

Kuhusu hatua hatutegemei ichukue muda mrefu watu kuwajibishwa maana pia umekiri hata Chama kilishafanya uchunguzi hivyo hizi ni nyama tu za kuongeza.Hatutaki tuambiwe hadithi zaidi ya wahusika kuchukuliwa hatua.

Tunataka 2013 mwanzoni tujue muelekeo wa Chama,kama tunaenda na makundi kama haya tena wengine tutanyanyua mikono kutetea vyama tusubiri harakati mitaani pengine zitasaidia.

Mwisho tuache tabia za CCM,tukiri kuna mgawanyiko ndani ya Chama hivyo kauli za Mh Mbowe eti hakuna mgawanyiko zinasikitisha.Kuna mgawanyiko usio wakupuuzia,tunataka tuone uharaka na umakini ktk kuamua mambo yenu wenyewe ili tuwaamini.
 
Vumbi tu! Mlikuwa wapi muda wote? Matatizo lukuki, nazidi kusisitiza uongozi ni tatizo, kaka angalia nawe usije ukawa mojawapo ya tatizo kwa sababu tayari press yako iko biased kwamba "viongozi wamekashifiwa". Hao wanatakiwa kujibu tuhuma na kila mmoja ana haki kidemokrasia kutaja maonevu, mfano Dr Slaa kuwa na kadi ya CCM ambako mimi siafiki ni kashfa? Acha hizo!

Sana sana, kama hamna kitachotamkwa kuhusu kadi mi najitoa CDM na wewe mwenyewe utakosa kura yangu.

Avanti, asante kwa maoni yako hata hivyo zingatia kuwa 'press' yangu ipi? Ikiwa wewe kweli ni mwanachama wa CHADEMA na una malalamiko dhidi ya kadi ya Dr Slaa andika rasmi kwa chama. Kabla ya kuandika malalamiko hayo usome kwanza katiba ya CHADEMA, katiba ya CCM na sheria ya vyama vya siasa. Dr Slaa ameshasema wazi kwamba yeye si mwanachama wa CCM, ni mwanachama wa CHADEMA toka alipohama CCM. Mwanachama akihama chama kimoja tayari anapoteza uanachama wake wa chama cha awali, hii ni kwa mujibu wa sheria ya vyama vya siasa, katiba za vyama vya siasa na pia hukumu ya mahakama ambayo imewahi kutolewa kuhusu suala la kadi. Ukishazingatia hayo na bado ukaendeleza suala hilo na ikiwa kwenye ni mwanachama utakuwa umeingia kwenye mtego wa kipuuzi wa CCM.

JJ
 
124 Reactions
Reply
Back
Top Bottom