Hatua za ukuaji wa mtoto akiwa tumboni!

Song of Solomon

JF-Expert Member
Aug 5, 2021
2,733
5,490
HATUA ZA UKUAJI WA MTOTO AKIWA TUMBONI

Je wewe ni mjamzito na unatamani kufahama Hatua ya ukuaji wa mtoto wako aliyeko tumboni ??

Hizi ndio Hatua za ukuaji wa mwanao akiwa tumboni.

Hatua za ukuaji wa mtoto tumboni

WIKI YA (1- 4).
√ Yai la kike linarutubishwa na mbegu za kiume.
√ Kijusi kinaanza kujitengeza (Umba)
√ Mishipa ya damu,Tumbo,Ini, n.k vinatengenzwa

WIKI YA (5 - 8).
Viungo Muhimu vinatengenzwa na kukomaa
√ Ubongo
√ Moyo
√ Uti wa Mgongo
√ Macho,masikio,mdomo na pua.
√ Miguu, mikono, vidole na kucha

WIKI YA (9-12).
√ Shingo huanza kujitengenza.
√ Kope za macho hujitengeneza.
√ Katika kipindi hiki mtoto anafikia urefu wa inchi 2.5
Kumb.... Uhitaji mwingi wa madini ya chuma kwa mtoto.

WIKI YA (13-17).
√ Miguu na mikono inakamilika
√ Shingo inakamilika katika kipindi hiki.
√ Mifupa inaanza kukomaa

WIKI YA (18-22).
√ Mtoto anaweza Kusikia sauti za mama yake.
√ Mtoto anaanza kucheza tumboni.
√ Mtoto anafikia urefu wa inchi 7.5 na uzito kuongezeka.
√ Unaweza Kusikia mapigo ya moyo ya mtoto.

WIKI YA (23-27.
√ Vidole na kucha za mtoto zina kamilika.
√ Mtoto anaanza kulala na kuamka (kucheza)
√ Mtoto anaanza Kusikia sauti za nje na za mama.
Kumbukw...... Kuna uhitaji mkubwa sana katika kipindi hiki wa damu, Mama anaanza kuwa na upungufu wa damu kwa sababu uhitaji wa madini chuma kwa mama na mtoto ni mkubwa.

WIKI YA (28-32).
√ Ubongo wa mtoto unakamilika kutengenezwa na kukamilika.
√ Mtoto anaanza kufyonza virutubisho kwenye tumbo na utumbo mdogo wa mfumo wa mmeng’enyo wake.

WIKI YA (33-36).
√ Mboni za macho zinaweza kusinyaa na kutanuka, kuhisi mwanga.
√ Uzito unaongezeka maradufu zaidi kama ½ ya aliokuwa nao.
√ Kucheza na kuelea tumboni kunaongezeka zaidi na kwa nguvu zaidi.
√ Mifupa inakomaa na nywele zina kuwa zimeota.

WIKI YA (37-40).
√ Mtoto anakuwa tayari kwa kuzaliwa
√ Mtoto anaanza kushuka
√ Mama anaanza Kusikia chunguzi.
√ Maandalizi ya kujifungua
Kumb.... Uhitaji wa madini ya chuma ni mkubwa sana kwa ukuaji na uborashaji wa afya ya mama na mtoto
 
Back
Top Bottom