Hatua za Ugonjwa wa VVU/UKIMWI (HIV/AIDS stages) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hatua za Ugonjwa wa VVU/UKIMWI (HIV/AIDS stages)

Discussion in 'JF Doctor' started by MziziMkavu, Sep 7, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Sep 7, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  [​IMG]

  Ugonjwa wa HIV/AIDS umekuwa janga kubwa sana duniani kwa sasa kutokana kuathiri watu wengi na kukosekana kwa tiba ya ugonjwa huu. Maambukizi ya ugonjwa wa HIV/AIDS hufahamika kama maambukizi ya VVU (Virusi vya Ukimwi). Mtu anapopata magonjwa nyemelezi (opportunistic infections) ndiyo huwa tunasema mtu amepata ugonjwa wa UKIMWI au AIDS.

  Makala hii ni majibu ya swali la msomaji wetu mmoja aliyetaka kufahamu hatua za ugonjwa wa VVU/UKIMWI aliyesema “Ningependa kujua siteji 1-4 za vvu ukimwi na dalili zake zote”. Swali ambalo liliniweka kwenye wakati mgumu sana kwani hatua za ugonjwa huu zinajumuisha magonjwa mbalimbali ambayo mengine ni vigumu sana kuyaelezea kwa lugha yetu ya kiswahili. Natumai kwa kupitia makala hii tutakuwa tumetoa mwanga kidogo wa hatua za ugonjwa wa VVU.

  Je ni kuna hatua ngapi za ugonjwa wa VVU/UKIMWI na dalili zake ni zipi?
  Kwa mujibu wa uanishaji uliofanywa na wataalamu wa shirika la Afya Duniani yaani WHO, kuna hatua (stages) kuu nne za ugonjwa wa VVU/UKIMWI ambazo ni:


  [​IMG]

  1. Hatua ya kwanza [Primary HIV Infection]
  Hatua hii huwa kwa muda wa wiki nne. Ni asilimia 20 tu ya watu wenye maambukizi ya VVU walio kwenye hatua hii ambao hupata dalili na viashiria vikali vya ugonjwa huu lakini mara nyingi madaktari hushindwa kutambua kama mgonjwa amepata maambukizi ya VVU kutokana na dalili na viashiria vyake hapa kufanana sana na dalili za magonjwa mengine. Mgonjwa aliye katika hatua hii ya kwanza ya maambukizi ya VVU huweza kuonesha dalili na viashiria kama vile kuvimba tezi (swollen lymph glands), kupatwa na homa kali, kuumwa koo (sore throat), kujihisi mchovu, kujihisi maumivu sehemu mbalimbali mwilini (body aches), kutokwa na vipele mwilini (skin rash), na pia kutapika, kuharisha au kuumwa tumbo


  Mgonjwa anayepata dalili na viashiria hivi tunasema kwamba amepata “Acute HIV infection/Acute HIV retroviral infection au seroconversion illness.” Dalili hizi hutokana na mwili wa mtu mwenye maambukizi ya VVU kuanza kutengeneza kinga dhidhi ya VVU.

  Hatua ya Pili (Clinically Asymptomatic Stage)
  Katika hatua hii ambayo inaweza kudumu kwa muda wa miaka kumi, mgonjwa anakuwa haonyeshi dalili/viashiria vyovyote vile isipokuwa anaweza kuwa na tezi zilizovimba [swollen lymph nodes]. Kiwango cha VVU kwenye damu hupungua sana lakini mgonjwa anaweza kuambukiza mtu mwingine yoyote na vipimo vya VVU vina uwezo wa kutambua uwepo wa maambukizi y VVU katika damu.


  Tafiti mablimbali zimeonesha kwamba VVU katika mwili huwa bado zinazaliana [active] na hukimbilia/hujificha kwenye tezi [lymph nodes]. Kutokana na kujificha kwake katika hatua hii, kipimo cha kupima wingi wa virusi vya ukimwi (Viral load test) katika mwili hutumiwa sana ili kuweza kutambua uwepo wa VVU. Kipimo hiki pia husaidia katika kumpangia mgonjwa tiba yake.

  Hatua ya Tatu [Symptomatic HIV infection]
  Kutokana na kuongezeka kwa wingi wa VVU katika mwili, kinga ya mwili huzidi kudhoofika na hii husababishwa na;
  • Tezi na tishu zilizoathiriwa na VVU huharibika kutokana na maambukizi ya muda mrefu
  • VVU hubadilika badilika na kuwa na uwezo zaidi wa kuathiri tishu na sehemu mbalimbali za mwili na hata kuziua/kuziharibu seli zinazokinga mwili kutokana na maambukizi zinazojulikana kama T helper cell
  • Mwili hushindwa kumudu uharibifu wa T helper cell na kushindwa kuzalisha seli nyingine mpya.


  Dawa za kuvubaisha VVU au Antiretroviral therapy huanza kutumiwa wakati seli aina ya CD4 zinapopungua na kuwa kiwango cha chini sana. Kupungua kwa seli hizi za CD4 ni kielelezo cha kinga ya mwili kuwa dhaifu. Matumizi ya dawa hizi huboresha kinga ya mwili na kumfanya mgonjwa kuishi kwa muda mrefu bila kuonyesha dalili au viashiria vyovyote vile [yaani kumrudisha mgonjwa katika hatua ya pili].

  Kama mgonjwa wa VVU hatumii dawa za kuvubaisha VVU au anatumia ARV's ambazo hazimsaidii au hazifanyi kazi vizuri mwilini mwake, basi mgonjwa ataendelea kuingia kwenye hatua ya nne ya Ukosefu wa Kinga Mwilini (Ukimwi) au AIDS.

  [​IMG]  Hatua ya Nne [UKIMWI]
  Kama nilivyoeleza hapo juu, hatua hii hujulikana kama Ukosefu wa Kinga Mwilini [UKIMWI] au AIDS, ambapo mgonjwa hupata maambukizi ya magonjwa nyemelezi pamoja na saratani za aina mbalimbali kutokana na kupungua kwa kinga mwilini.


  Vigezo vilivyopangwa na shirika la afya duniani (WHO) ili kuweza kutambua kama mgonjwa yupo kwenye hatua hii ya UKIMWI hutofautiana kati ya watu wakubwa na watoto chini ya miaka 5. Pamoja na kuwa WHO wameweka vigezo vya pamoja, utambuzi wa hatua za ugonjwa wa UKIMWI hutofautiana kati ya nchi na nchi kutokana na miongozo tofauti ya nchi hizo.

  Kwa watu wazima na watoto walio na umri zaidi ya miaka mitano, uwepo wa ugonjwa wowote nyemelezi pamoja na kushuka kiwango cha CD4 chini ya 200 cells/mm3 au kushuka kwa seli za CD4 chini ya asilimia 15 hutambulika kama ugonjwa wa UKIMWI.

  Kwa watoto walio chini ya miaka mitano, uwepo wa ugonjwa wowote nyemelezi/kushuka kwa seli za CD4 chini ya asilimia 20 [kwa wale wenye umri kati ya miezi 12-35] hutambulika kama wana ugonjwa wa UKIMWI.

  Watoto wenye umri chini ya miezi 12, kupungua kwa seli za CD4 chini ya asilimia 25 ndiyo hutumika kutambulisha wana ugonjwa wa UKIMWI.

  CD4 ni nini?
  CD4 ni aina ya protini inayopatikana katika ukuta wa seli zinazojulikana kama T helper cell [pia hujulikana kama CD + lymphocyte]. VVU hushambulia na kujishikiza kwenye protini hii kabla ya kupata uwezo wa kuathiri seli za T helper cell. Seli hizi za T helper cell ndizo hulinda mwili dhidi ya maambukizi mbalimbali na hivyo kuchangia katika kustawi kwa kinga ya mwili. Kupungua kwa seli hizi mwilini husababisha kupungua kwa kinga ya mwili na hivyo mtu kupata magonjwa mbalimbali.


  Magonjwa nyemelezi/saratani (opportunistic infections/cancer)
  Baadhi ya magonjwa nyemelezi yanayoweza kumpata mtu mwenye ugonjwa VVU/UKIMWI ni pamoja na
  a. magonjwa ya mfumo wa kupumua kama vileugonjwa wa homa ya mapafu (pneumocyctic carinii pneumonia), Kifua kikuu (TB) na Kaposi’s sarcoma (saratani);
  b. Magonjwa ya mfumo wa chakula kama vile Cryptosporidiosis, Candida (fangasi), Cytomegolavirus (CMV), Isosporiasis, na Kaposi's Sarcoma
  c. Magonjwa ya mfumo wa fahamu (Central/peripheral nervous system) kama vile Cytomegolavirus, Toxoplasmosis, Cryptococcosis, Non Hodgkin's lymphoma (saratani), Varicella Zoster (mkanda wa jeshi), Herpes simplex
  d. Magonjwa mbalimbali ya ngozi [skin diseases] kama vile Herpes simplex, Kaposi's sarcoma (saratani ya ngozi) na Varicella Zoster [mkanda wa jeshi]


  Hatua za VVU/UKIMWI kulingana na dalili za ugonjwa [clinical classification of HIV/AIDS]

  Kutokana na uhaba wa vifaa vya kupimia kiwango cha seli aina ya CD4 katika nchi mbalimbali, shirika la afya duniani, limetengeza muongozo mwingine ambao utamsaidia mhudumu wa afya kuweza kutambua kama mgonjwa amefikia hatua ya ugonjwa wa UKIMWI na anastahili kuanza tiba au la. Uainishaji wa namna hii huitwa clinical classification of HIV/AIDS.


  Hatua ya Kwanza [Clinical stage I]
  • Mgonjwa hana dalili zozote (asymptomatic)
  • Kuwepo kwa uvimbe katika tezi ambao hauondoki (persistant lymphadenopathy)
  Hatua ya Pili [Cilinical stage II]
  • Kupungua uzito chini ya asilimia 10 ya uzito wa mwili bila sababu maalum
  • Magonjwa ya mara kwa mara kwenye mfumo wa upumuaji kama magonjwa ya masikio, kinywa, tezi la koo nk (sinusitis, tonsillitis, otitis media, pharyngitis)
  • Mkanda wa jeshi (Herpes zoster)
  • Vidonda pembezoni mwa mdomo (Angular chelitis)
  • Vidonda vya mara kwa mara kwenye kinywa (Recurrent oral ulceration)
  • Vipele mwilini (Papular pruritic eruptions)
  • Ugonjwa wa ngozi [Seborrhoeic dermatitis]
  • Maambukizi ya fangasi katika kucha [Fungal nail infections]


  Hatua ya Tatu [Clinical stage III]
  • Kupungua uzito kwa zaidi ya asilimia 10 ya uzito wa mwili bila sababu yoyote maalum
  • Kuharisha zaidi ya mwezi mmoja bila sababu yoyote maalum
  • Kuwa na homa isiyoelezeka [homa hii inaweza kuwa inapona na kujirudia au homa ambayo inakuwepo kwa zaidi ya mwezi mmoja]
  • Maambukizi ya fangasi kwenye kinywa [Persistent oral candiadiasis]
  • Oral hairy leukoplakia
  • Ugonjwa wa kifua kikuu kwenye mapafu [kwenye mapafu]
  • Maambukizi hatari ya vimelea vya bakteria [homa ya mapafu, ugonjwa wa uti wa mgongo, maambukizi katika mifupa na jointi, empyema, pyomyositis, bacteraemia]
  • Maambukizi hatari kwenye kinywa [Acute necrotizing ulcerative stomatitis, gingivitis or periodontitis]
  • Upungufu wa damu mwilini bila sababu yoyote maalum [Unexplained anaemia (below 8 g/dl), neutropenia (below 0.5 billion/l) and/or chronic thrombocytopenia (below 50 billion/l)]


  Hatua ya Nne (Clinical stage IV)
  • Kudhoofika mwili [HIV wasting syndrome]
  • Homa kali sana ya mapafu [Pneumocystis pneumonia]
  • Saratani ya shingo ya kizazi [invasive cervical cancer]
  • Homa kali sana ya mapafu inayojirudia inaosababishwa na vimelea vya bakteria
  • Magonjwa ya kwenye mfumo wa figo/moyo yayochangiwa na VVU [Symptomatic HIV-associated nephropathy or HIV-associated cardiomyopathy]
  • Maambukizi ya fangasi katika mishipa ya kupitisha chakula mpaka kwenye mapafu na mishipa yake ya kupitisha/kusambaza hewa mwilini
  • Ugonjwa wa kifua kikuu uliosambaa mwilini [disseminated mycobacteria tuberculosis]
  • Maambukizi ya fangasi yaliyosambaa mwilini [histoplasmosis, coccidiomycosis]
  • Saratani ya kwenye tishu za mwili [kaposis sarcoma]
  • Maambukizi kwenye mishipa ya fahamu yanayosababishwa na vimelea aina ya toxoplasma gondii [Central nervous system toxoplasmosis]
  • Maambukizi ya VVU kwenye ubongo na kusababisha mgonjwa kuwa kama mgonjwa wa akili [HIV encephalopathy]
  • Ugonjwa wa uti wa mgongo uliosambaa mwilini [Extrapulmonary cryptococcosis including meningitis]
  • Ugonjwa wa kifua kikuu uliosambaa mwilini ambao hausababishwi na vimelea aina ya mycobacteria tuberculosis [Disseminated non-tuberculous mycobacteria infection]
  • Aina ya ugonjwa unaoathiri ubongo na kumfanya mgonjwa shindwe kufikiri sawasawa [Progressive multifocal leukoencephalopathy]
  • Chronic cryptosporidiosis na Chronic isosporiasis
  • Recurrent septicaemia [including non-typhoidal Salmonella]
  • Lymphoma [cerebral or B cell non-Hodgkin]
  • Atypical disseminated leishmaniasis
  • Cytomegalovirus infection [retinitis or infection of other organs]
  • Chronic herpes simplex infection [orolabial, genital or anorectal of more than one month’s duration or visceral at any site]


   

  Attached Files:

 2. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #2
  Sep 7, 2012
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,334
  Likes Received: 22,186
  Trophy Points: 280
  Uzi huu ni chakula kwa akili zetu. Kibaya zaidi ni kwamba wabongo wengi wanaogopa kusoma makala za ukimwi wakiamini kuwa wataupata, lakini wanajipa excuse kuwa haya mambo ya ukimwi tumeyasikia sana na tunayajua.
   
 3. Triple G

  Triple G JF-Expert Member

  #3
  Sep 7, 2012
  Joined: Aug 12, 2011
  Messages: 746
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 45
  daah inatisha hii kitu jamani,?hadi nimeogopa..daah..ili kuweza kukabili hili janga mabadiliko yaanzie kwa mtu binafsi.Nimeogopa ngoja nikacheki afya.
   
 4. chameli

  chameli Senior Member

  #4
  Sep 7, 2012
  Joined: Jul 23, 2011
  Messages: 133
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Inatisha jamani.
   
 5. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #5
  Sep 7, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,345
  Likes Received: 418,852
  Trophy Points: 280
  [MENTION]
  MziziMkavu[/MENTION] kweye utafiti wangu viongozi wengi wa Afrika wana mkanda wa jeshi........hizi ni dalili wameukwaa..........mshahara wa ufisadi na dhuluma ndiyo huo......mauti.......
   
 6. Apollo

  Apollo JF-Expert Member

  #6
  Sep 7, 2012
  Joined: May 26, 2011
  Messages: 4,889
  Likes Received: 1,371
  Trophy Points: 280
  Mtu ukiisoma hii topic then ukatoka nje ya ndoa na kuparamia wanawake basi wewe utakuwa ni kichaa. Thanks kwa somo zuri mkuu.
   
 7. p

  pembe JF-Expert Member

  #7
  Sep 7, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 2,058
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Mungu akubariki kwa kazi nzuri. Hii shule tuliyopata tutaifanyia kazi kwa kuisambaza kwa wasio na uwezo wa kusoma humu mtandaoni.
  Hivi ni vitu vizito tunavyotaka kusoma na kuchangia ndani ya JF.
  Maswali: Kondomu zinazuia kupata huu ugonjwa hatari kwa asili mia kweli? Je ni kweli watumiaji wa ARV wanakuwa na mhemko sana wa kutaka kujamiiana?
   
 8. Kanyapini

  Kanyapini JF-Expert Member

  #8
  Sep 7, 2012
  Joined: Jul 25, 2012
  Messages: 299
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  HIV free generation, it begins with you!
   
 9. k

  kisukari JF-Expert Member

  #9
  Sep 8, 2012
  Joined: Jul 16, 2010
  Messages: 3,759
  Likes Received: 1,049
  Trophy Points: 280
  kusoma tu,yanatisha.mwisho utaji suspect bure,hata kama umepima.ila kukumbushana ni muhimu
   
 10. SG8

  SG8 JF-Expert Member

  #10
  Sep 8, 2012
  Joined: Dec 12, 2009
  Messages: 3,204
  Likes Received: 261
  Trophy Points: 180
  Je tuko wangapi? Tulizana!
   
 11. Zamaulid

  Zamaulid JF-Expert Member

  #11
  Sep 8, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 16,348
  Likes Received: 6,698
  Trophy Points: 280
  ngoja weekend ipite nitarudi kuusoma!
   
 12. M

  Mwanaweja JF-Expert Member

  #12
  Sep 9, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 3,576
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  kikubwa tuwe waaminifu kwenye ndoa zetu nje ya hapo ni janga kwa familia zetu soma zuri sana mwenye macho haambiwi tazama
   
 13. Dumelambegu

  Dumelambegu JF-Expert Member

  #13
  Sep 9, 2012
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 1,052
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Ngoja niibane kwa kufuli la muisrael na funguo nimwachie mywife wangu.
   
 14. salito

  salito JF-Expert Member

  #14
  Sep 9, 2012
  Joined: Dec 29, 2011
  Messages: 1,365
  Likes Received: 352
  Trophy Points: 180
  Kiongozi nashukuru sana kwa ufafanuzi wako
   
 15. s

  sweke34 JF-Expert Member

  #15
  Dec 12, 2012
  Joined: Sep 28, 2010
  Messages: 2,533
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Hivi ni ukweli vidudu vya ukimwi haviwezi kusurvive kwenye mate? Nimesikia ni vigumu sana kuambukizwa ukimwi ukiliwa koni labda mpaka wote muwe na vidonda vikubwa. Ni kweli hayo mzizimkavu?
   
 16. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #16
  Dec 13, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  Mkuu sweke34 inawezekana hivyo ulivyosema lakini cha muhimu tuwe waangalifu sana katika kufanya uhusiano wa mapenzi kupima ni kitu muhimu na tuache mambo ya uzinzi mtu uwe na Mpenzi mmoja ikiwezekana tuowe ili tuepuke na janga hili la ukimwi. Ukiwa na mpenzi wako Lazima muende kupima kabla ya kufanya mapenzi ili kuhakikisha muko salama.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 17. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #17
  Dec 13, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  MASHINE YA KUSAGIA BLENDA.jpg


  Juicer, Kifaa cha kusagia matunda (Blender), karoti nne (kwa ajili ya kuongeza nguvu ya kinga mwilini na kuongeza kiwango cha CD4 kutokana na viini lishe vya ‘beta carotene’).

  Robo ya kiazi kinachofahamika kama ‘beetroot’ (ili kuongezea nguvu maini na kuzuia uwezekano wa kuzalishwa vitu visivyohitajika mwilini kwani kiazi hicho kina kiini lishe kiitwacho ‘betane’).

  Kipande cha tangawizi (kwani ina madini ya ‘selenium’ ambayo hupunguza kuongezeka kwa virusi mwilini. Pia huhamasisha kuzaliana kwa kinga zaidi mwilini).

  Kiasi kidogo cha binzari (turmeric- kwani ina madini ya curcumin yenye uwezo mkubwa wa kupambana na sumu na kuzuia kuongezeka kwa virusi. Binzari ni rafiki mkubwa wa maini).

  Kipande cha kitunguu chekundu (kina madini viini lishe maalumu –aquercetin- vinavyoongezea uwezo wa kuponya wa Vitamini C, mpambanaji muhimu wa virusi vya Ukimwi huku pia kikiwa na ‘allicins’ inayozuia kuwapo na magonjwa nyemelezi).

  Vipande vinne vya vitunguu swaumu (hivi huondoa sumu kwenye chembe hai zote mwilini. Ni silaha zenye nguvu za ‘allicins’, ‘selenium’ na chembe hai nyingine muhimu kupambana na virusi).

  Majani nane ya ‘spinach’ (Haya yana utajiri wa ‘chlorines’ ambayo huongeza kinga mwilini na kupambana na maradhi. Pia yana SOD au ‘Super Oxide Dismutase’, ‘sterols’ na ‘sterolins’. Madini haya huongeza CD8 pamoja na CD3).

  1. Vioshe vyema vitu hivi.
  2. Osha mbogamboga vizuri kwa maji safi.
  3. Weka mbogamboga hizo kwenye bakuli lisilopitisha hewa.
  4. Tia maji safi ya kunywa hadi yafunike mbogamboga hizo.
  5. Koroga na funika haraka kwa mfuniko thabiti.
  6. Baada ya dakika tano ondoa kifuniko, toa maji na kamua mbogamboga kupata juisi yake.

  JINSI YA KUTENGENEZA
  1. Weka juisi hiyo kwenye ‘blender’ kisha ongeza:
  a) Vijiko viwili vya unga wa karanga za Brazil. Karanga hizo zina asili ya utajiri mkubwa wa ‘selenium’ miongoni mwa vyakula vingi vikavu. ‘Selenium’ huzuia kuongezeka kwa virusi na husaidia kuponya mgonjwa. (Vyakula vingine vyenye ‘selenium’ ya kutosha ni mbegu za alizeti, samaki, maini na nyama ya nguruwe (bacon). Hivi unaweza kuvila tofauti kwani haviwezi kusagwa pamoja na juisi)
  b) Parachichi nusu.

  2. Saga mara moja. Usitunze kwenye jokofu.

  Nyongeza:
  i. Kunywa juisi hiyo walau mara mbili kwa siku wakati tumbo likiwa halina kitu. Kadri ya kiwango utakachotumia ndivyo utakavyopata nafuu
  ii. Kama inawezekana pia kunywa juisi halisi ya nanasi kila siku kusaidia tiba hiyo ya maji ya matunda (juice therapy). Nanasi lina madini ya ‘bromelain’ yenye uwezo mkubwa wa kupambana na virusi.
  iii. Juisi ya tikiti nayo ni nzuri kwa mgonjwa wa Ukimwi. Hii ni kwa sababu matikiti yana virutubisho viitwavyo ‘glutathiones’ vinavyozuia kuongezeka kwa virusi.
  3. Furahia maisha huku ukiusaidia mwili wako kupambana na wavamizi (virusi vya Ukimwi)!
   
 18. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #18
  Dec 13, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  [SIZE=+3]Kondom sio kinga ya Ukimwi[/SIZE][SIZE=+2]Virusi vya HIV hupenya[/SIZE]


  Wananchi wengi wataendelea kuteketea kwa ukimwi kutokana na dhana potofu waliyo nayo kwamba kondomu ni jawabu katika kuzuia ukimwi.
  Taarifa ya Shirika la Viwango nchini (TBS) iliyotolewa hivi karibuni na kunukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari imewaonya wananchi waepukane na dhana kwamba kondomu zitawanusuru kuambukikizwa ukimwi.

  Kwa mujibu wa Taarifa hiyo iliyonukuliwa na gazeti moja la kila wiki katika toleo lake la Alhamisi Novemba 19; ukimwi umekuwa ukikua kwa kasi kubwa sana hapa nchini ambapo zaidi ya Watanzania milioni moja unusu (milioni 1.5) wamesha ambukizwa virusi hivyo. Kasi hiyo ya kuongezeka kwa ukimwi imekuwa ikienda sambamba na ongezeko la matumizi ya "Salama" kondom na nyinginezo.


  Likinukuu taarifa ya T.B.S. gazeti hilo limesema kwamba, "ni rahisi kwa

  kirusi cha ukimwi kupenya katika kondomu kwa sababu katika darubini za kawaida kondomu zinaonyesha kuwa na matundu ambayo ni makubwa zaidi ya mara 50 ya ukubwa wa kirusi cha ukimwi ambacho hakiwezi kuonekana kwa darubini hiyo hiyo. Mfano wake ni kama mtegemea mchanga usipite kwenye "wiremesh" (waya wa kashata wa dirisha).

  Aidha, taarifa hiyo imeeleza kwamba ukimwi nchini Uganda unapungua kwa wananchi kubadili tabia za uasherati wakati Tanzania kipaumbele kimekuwa katika matumizi ya kondomu.


  Toka kampeni za matumizi ya kondomu kama kinga ya ukimwi zilipoanza gazeti hili limekuwa likiwatahadharisha wananchi kwamba kondomu si kinga ya ukiwmi kwa sababu; kwanza virusi vya HIV ni vidogo sana kiasi kwamba vinaweza kupenya kwenye matundu ya kondomu. Pili, yaweza kupasuka na tatu kuvuja (spillage),

  Aidha, tumekuwa tukisisitiza kwamba upo utapeli unaofanyika katika biashara ya kondomu ambapo wananchi hupewa taarifa za uongo.

  Kwa tamaa ya kuzoa mapesa wafanya biashara wamekuwa wakiwahadaa watu kwamba waweza kumchezea mamba au simba mwenye njaa na wakawa salama ilimradi wana "Salama kondomu" mkononi. Dhana hii ilipotiliwa nguvu na viongozi wa Serikali pamoja na vyombo vya habari soko likazidi kukua.


  Kwa kipindi cha zaidi ya miaka mitano ambapo gazeti hili limekuwa likizungumzia hoja hizi na kuonekana wa 1947; ni roho ngapi zimeteketea kwa kufuata dhana potofu ya uzinzi salama.

  Nani atalipa gharama na fidia ya hasara iliyotokana na kampeni za awali?
   
 19. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #19
  Dec 13, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  [h=3]Apona UKIMWI! Kweli Kabisa![/h]

  Hatimaye, tiba ya UKIMWI umepatikana! Mzungu aliyekuwa mwathirika wa UKIMWI amepona. Hana dalili ya virusi vya HIV mwilini wake. Tiba aliyopata ni ile ya ugonjwa wa Leukemia (Kansa ya damu). Ila hiyo tiba ni ghali na si rahisi kupatikana hivyo itakuwa muda kabla waathirika wote waweze kupata tiba. Kwa sasa ni huyo mtu mmoja tu aliyepona, Bwana Timothy Brown.

  Hata hivyo, hayo makampuni yanayotengeneza dawa za cocktails wata zuia hiyo tiba. Watakuwa hawapati faida tena.

  ************************************************

  Man Cured of AIDS: ‘I Feel Good'


  [TABLE="class: tr-caption-container, align: center"]
  [TR]
  [TD][​IMG][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="class: tr-caption"]Aliyepona UKIMWI, Timothy Brown[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   KUTOKA ABC News

  The fact that Timothy Brown is a reasonably healthy 46-year-old is no small thing. Only a few years ago, he had AIDS.

  "I feel good," Brown told ABC News. "I haven't had any major illnesses, just occasional colds like normal people."

  Brown is the only person in the world to be cured of AIDS, the result of a transplant of blood stem cells he received to treat leukemia.

  "My case is the proof in concept that HIV can be cured," he said.

  Brown got lucky. The blood stem cells he received came from a donor with a special genetic mutation that made him resistant to HIV. The genetic mutation occurs in less than 1 percent of Caucasians, and far less frequently in people of other races. Before Brown got his transplant in 2007, doctors tested nearly 70 donors for this genetic mutation before they found one who was a match.

  But doctors hope that a similar solution could help other people with HIV: umbilical cord blood transplants.

  Dr. Lawrence Petz, medical director of StemCyte, an umbilical cord blood bank, said although Brown was cured by his transplant, the process was complicated because the blood stem cells came from an adult donor.

  "When you do that you have to have a very close match between donor and recipient," Petz said. "With umbilical cord blood, we don't need such a close match. It's far easier to find donor matches."

  But it's still not that easy. Petz and his colleagues have tested 17,000 samples of cord blood so far, and found just 102 that have the genetic HIV-resistant mutation. The team performed the first cord blood transplant on an HIV-infected patient a few weeks ago, and they have another transplant planned for a similar patient in Madrid, Spain, later this year. It will still be months before researchers can tell if the transplants have any effect on the patients' HIV.

  Petz also noted that transplants aren't performed solely to treat AIDS. Patients who get them have an additional condition that requires a blood stem cell transplant. Curing their AIDS would be an incredible bonus.

  "It can be done. It's just a matter of time," Petz said.

  Brown had his transplant in February 2007. Today, his body shows no signs of the virus.

  Brown said he feels guilty being the only person to have been cured of the virus when millions still live with it. But he hopes his story will inspire others that a cure is possible.

  "I don't want to be the only person in the world cured of HIV. I want a cure for everyone," he said.Swahili Time: Apona UKIMWI! Kweli Kabisa!
   
 20. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #20
  Dec 13, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  NAZI INAVYOWEZA KUPUNGUZA MAKALI YA UKIMWI  [​IMG]
  Vyakula vimetufanya tuamini kuwa maradhi mengi hayana tiba. Hiyo inathibitika wazi pale vyakula vinapotoa majibu ya tiba bila sisi wenyewe kujijua. Kwa mfano ni rahisi sana watu kula chakula wakashiba halafu wakawa hai na kusema dawa hii inafaa au dawa ile haifai na kusahau kukitaja chakula kama dawa ya msingi inayobeba mhimili mzima wa tiba zote. Hii ndio sababu madaktari na wauguzi wanakuwa wakali katika kuwasisitiza wagonjwa kula kabla ya kupewa dawa.


  Katika ardhi ambayo binadamu hajafanya uharibifu wa mazingira, inaaminika kuwa pamelala tiba za magonjwa yote zikisubiri watu waje wazigundue.

  Miaka ya 1980 ugonjwa wa AIDS ulitokea kuua wanaume, wanawake na watoto duniani kote kwa kishindo kikubwa! Watu wengi wamekufa na wengi wataendelea kufa, kitu ambacho ni tishio ulimwenguni kote mpaka hivi sasa. Wakati huo huo vyakula vimeendelea kuwa tiba na mhimili mkubwa kwa afya za waathirika wa magonjwa mbalimbali duniani kote huku gonjwa hili likizidi kuonyesha sura mbaya na ya kutisha zaidi kila kukicha.

  Zipo tiba nyingi ambazo binadamu anazipata toka kwenye vyakula anavyokula bila kujua kama anajitibu. Tena kwa bahati nzuri zaidi ni kuwa tiba hizo pia zinapatikana bila gharama yoyote zaidi ya kula chakula, ukitofautisha na gharama za matibabu ya aina nyingine kama hospitali, dawa za kienyeji nk.

  Unatakiwa ujue unapokula chakula chochote huwa unajitibu maradhi fulani bila kujijua. Kwa mfano unaweza kujitibu makali ya AIDS Endapo utatumia vyakula hivi vilivyoorodheshwa hapo chini, pamoja na dawa toka hospitali.

  Namna ya kufanya:
  Utahitaji;

  1. Nazi. Yaweza kuwa nazi, mafuta ya nazi, tui la nazi, dafu n.k.
  2. Chai mbichi isiyokaushwa.
  3. Vyakula - mchanganyiko wa nafaka.

  Nazi:
  Nazi imewahi kuthibitishwa kuwa na vitu muhimu vinavyoua virusi. Lauric Acid ndiyo acid pekee kwa kuua virusi ambayo inapatikana toka katika nazi na pengine ni toka kwenye maziwa ya mamaake binadamu tu duniani kote.

  Je, Ni kweli Nazi inarutubisha afya?
  Acid hii ndiyo kitu pekee chenye uwezo wa kuua virusi na ni rahisi kugundua hilo kama utakuwa mtu mwenye kumbukumbu basi nakupa Uthibitisho katika maeneo matatu.
  Linganisha afya mbovu za awali za watu waliohamia Dar Es Salaam kama vile wasichana wa kazi za ndani, vijana wanaokuja kusoma au kuutafuta maisha n.k. wakitokea sehemu zisipopatikana nazi. Utamkuta mtu anakuwa hajiamini, haongei sana, mwoga, ngozi yake imejikunja-kunja, miguu imepasuka na pengine hata kitambi cha kwashakoo ni kawaida kwao. Halafu angalia afya zao pale walipokula vyakula vilivyoungwa nazi kwa muda mfupi tu kama miezi mitatu tu wakiwa hapa Dar Es Salaam. Utagundua kuwa afya zao zilibadilika sana.Wananenepa, Mipasuko kwenye miguu inaondoka, Ngozi zinakuwa nyororo, kwashakoo inaondoka, wanakuwa sio waoga tena, wanaongea sana tena kwa kujiamini na kwa kusema yote ni kuwa wanachangamka kiafya.

  Kwa wale tuliosoma "Old schools" mtakumbuka tulisoma vitabu vingi vikiwemo Alfu lela Ulela ambavyo vilijumuisha Safari saba za Sindbad Baharia. Katika safari zake aliwahi kutekwa akiwa na wenzie saba baada ya chombo chao kugonga mwamba na kuvunjika. Watekaji waliwafungia ndani na kuwalisha "wali ulioungwa nazi" ili wanenepe kisha wawachinje! Sindbad kwa kujua hilo hakula kiasi kikubwa na baada ya muda mfupi wenzie walinenepa sana na walichinjwa wakaliwa! Yeye alikuwa akikonda siku baada ya siku na kuwafanya maharamia hao kumfungulia atembee tembee awe huru ili aimarike kiafya na ndipo alipopata mwanya wa kutoroka.

  Uthibitisho wa mwisho ni pale mtoto mchanga anapofiwa na mama yake basi huwa anaikosa lauric acid toka ziwa la mama na afya yake nadhani wote mmeshuhudia inavyoathirika. Kifupi ni kuwa anatakiwa pamoja na maziwa ya wanyama anayolishwa inatakiwa apate walau kijiko kimoja cha tui la nazi kila siku ili kuilinda afya yake isiporomoke.

  Hivyo kama wewe ni muathirika wa maradhi ya aina yoyote, basi tumia dawa za hospitali, halafu ili kuthibitisha hili jaribu kula vyakula vilivyoungwa nazi kwa kiasi kikubwa, au chakula kilichokaangwa kwa mafuta ya nazi, au jenga mazoea ya kutafuna nazi mbichi na pengine ni vizuri zaidi ukaacha tabia ya kunywa soda na kuanza kunywa maji ya madafu pale unaposikia kiu.

  Je Nazi yoyote inatibu?
  Kama kawaida ya uhusiano wa mmea na udongo ulivyo, zipo nazi ambazo ukizipeleka katika maabara utazikuta zina kiwango kikubwa cha lauric acid au ukakuta lauric acid ipo kidogo au pengine ukakuta nazi haina kabisa lauric acid kwa vile udongo ulipooteshwa nazi kuna kemikali ambazo zinasababisha udongo huo kuwa sio sahihi kuzalisha acid hiyo katika nazi. Kwa kutambua hilo tafiti nyingi zimefanyika na nazi zenye dawa hapa duniani zipo japo chache na zinapatikana kwa kupiga simu no 0768 215 956 au email rotion@live.com Pia mpaka sasa yapo makampuni ya kusindika nazi ambayo yanakamua nazi zenye lauric acid ya kutosha na kuuza kama dawa. Nazi hizo zimeingizwa nchini na ninazitumia kutoa tiba kwa waathirika na hakika zinapunguza idadi ya watu wenye afya mbovu. Lakini mpaka sasa hakuna taarifa zilizowafikia wawekezaji wa ndani hasa katika sekta ya afya ambao ningeweza kushirikiana nao kuitafiti bidhaa hii nchini watu wale na wapone.

  Je, Nazi zinapatikana?
  Upande wa pili wa shilingi una sura ya nazi kuwa bidhaa ya wenye nazo tu mara baada ya habari hii kuenea. Sasa Vile vile ni vema kwa wizara za kilimo na chakula pamoja na wizara ya afya kukaa chini na kuangalia namna ya kukabiliana na changamoto hii ya kupungua kwa nazi masokoni pamoja na kupanda kwa bei ya bidhaa hiyo ambayo inaweza kufikia shilingi elfu tatu kwa nazi moja endapo theluthi moja tu ya watanzania wataamua kuitumia nazi kama dawa ya kurutubisha afya zao.

  Wakati naendelea kukuletea habari hii, ni vema ukaituma email hii kwa watu ishirini au wote katika address book yako ili tupunguze idadi ya watu wenye matatizo ya kiafya. Tusifiche tiba maana kuwa na taifa lenye wagonjwa ni UMASIKINI. Tafadhali tuma sasa.  http://www.globalpublishers.info/profiles/blogs/nazi-inavyoweza-kupunguza   
Loading...