Hatua za kupata leseni ya udereva class C

Kabla haujapata hiyo lesen class c unaleseni daraja gani kwa sasa?NIT wanataka mtu ambaye tayari analeseni si chini ya class E

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Kuomba leseni ya udereva kwa mara ya kwanza


  • Uwe umehudhuria mafunzo katika Chuo chochote kinachofahamika na kupewa cheti
  • Uwe na umri zaidi ya miaka 18 kwa ajili ya gari na umri wa miaka 16 na kuendelea kwa ajili ya pikipiki
  • Uwe na leseni ya kujifunzia/ya muda ya udereva
  • Uwe umelipa ada ya kufanyiwa majaribio - GRR
  • Uwe na cheti cha kupimwa macho
  • Uwe umepeleka maombi kwenye ofisi ya polisi wa usalama barabarani kwa ajili ya kufanyiwa majaribio
  • Uende kwenye ofisi ya polisi wa usalama barabarani ukiwa na gari kwa ajili ya kufanyia majaribio
Baada ya mwombaji kufanyiwa majaribio anaweza kuruhusiwa kuendesha pikipiki na magari madogo.


Kubadilisha leseni ya udereva (Daraja A B C D E F na G)


  • Mwombaji ataenda kwenye ofisi ya polisi wa usalama barabarani akiwa na leseni yake ya zamani ya udereva
  • lazima awe na cheti cha umahiri
  • mwombaji awe na umri zaidi ya miaka 18 kwa magari na miaka 16 kwa pikipiki

KUBADILI ILI KUPATA DARAJA ''C''
  • Mwombaji ataenda katika ofisi ya polisi wa usalama barabarani akiwa na leseni yake ya zamani ya udereva
  • Awe na cheti cha umahiri
  • Mwombaji awe na umri zaidi ya miaka 18 kwa magari na miaka 16 kwa pikipiki
  • Cheti cha Gari la Kubeba Abiria (PCV) kutoka Chuo cha Taifa cha Usafirishaji au VETA
  • Mwombaji anatakiwa kubainisha aina ya gari analokusudia kuendesha
  • Mwombaji atapewa daraja la leseni kulingana na mafanikio yake.

Ni viwango gani vinatumika?


Viwango vya leseni za udereva ni:
Ada za leseniShilingi 40,000/= itakayolipwa kila baada ya miaka 3
Ada ya jaribio la kuendeshaShilingi 3,000/=
Ada za leseni ya mudaShilingi 10,000/= itakayolipwa kila baada ya miezi 3



Makundi ya leseni za udereva ni yapi?


Mfumo wa leseni za udereva utakuwa na makundi mbalimbali ya madaraja ya leseni za udereva kama ifuatavyo:
Pikipiki
A – Leseni ya kuendesha pikipiki zenye/zisizo na kigari na ambazo injini zake zina ukubwa zaidi ya cc 125 au uzito wa kilo 230.
A1 - Leseni za kuendesha pikipiki zisizo na kigari na ambazo ukubwa wake wa injini ni mdogo kuliko cc 125 au chini ya kilo 230.
A2 – Leseni ya kuendesha pikipiki za magurudumu matatu na manne.
A3 – Leseni za kuendesha pikipiki baiskeli ambazo ukubwa wake wa injini hauzidi cc 50

Vyombo Binafsi vya Moto
B – Leseni ya kuendesha aina zote za vyombo vya moto isipokuwa pikipiki, magari ya biashara, magari makubwa na magari ya kutoa huduma kwa umma.
Magari ya kutoa huduma kwa Umma
C – Leseni ya kuendesha magari ya kutoa huduma kwa umma yenye uwezo wa kubeba abiria 30 na zaidi pamoja na dereva. Magari katika kundi hili yanaweza kufungwa tela lenye ujazo wa juu unaokubalika usiozidi kilo 750. Waombaji wanatakiwa wawe wamewahi kuwa na leseni ya daraja C1 au E kwa kipindi kisichopungua miaka mitatu.
C1 – Leseni ya kuendesha magari ya kutoa huduma kwa umma yenye uwezo wa kubeba abiria 15 lakini wasiozidi 30, abiria pamoja na dereva. Magari katika kundi hili yanaweza kufungwa tela lenye ujazo wa juu unaokubalika usiozidi kilo 750. Waombaji wanatakiwa wawe wamewahi kuwa na leseni ya daraja D kwa kipindi kisichopungua miaka mitatu.
C2- Leseni za kuendesha magari ya kutoa huduma kwa umma yenye uwezo wa kubeba abiria wanne lakini wasiozidi kumi na tano. Magari katika kundi hili yanaweza kufungwa tela lenye ujazo unaokubalika usiozidi kilo 750. Waombaji wanatakiwa wawe wamewahi kuwa na leseni ya daraja D kwa kipindi kisichopungua miaka mitatu.
C3 – Leseni za kuendesha magari ya kutoa huduma kwa umma yenye uwezo wa kubeba abiria wanne au pungufu akiwemo dereva. Magari katika kundi hili yanaweza kufungwa tela lenye ujazo unaokubalika usiozidi kilo 750. Waombaji wanatakiwa wawe wamewahi kuwa na leseni ya daraja D kwa kipindi kisichopungua miaka mitatu.

Magari Madogo ya Mizigo ya Biashara
D – Leseni ya kuendesha aina zote za vyombo vya moto isipokuwa pikipiki, magari makubwa na magari ya kutoa huduma kwa umma.
Magari makubwa ya Mizigo ya biashara
E – Leseni ya kuendesha aina zote za vyombo vya moto isipokuwa pikipiki na magari ya umma. Waombaji wanatakiwa wawe wamewahi kuwa na leseni ya daraja D kwa muda usiopungua miaka mitatu.

Magari yenye Trela
F – Leseni ya kuendesha magari yanayokokota trela.

Magari ya Shambani na Migodini
G – Leseni ya kuendesha magari ya shambani na migodini.
Wanaojifunza
H – Leseni ya muda ya kujifunza

KWA MAELEZO/HUDUMA ZAIDI UNAWEZA KUFIKA KATIKA OFISI YA TRA ILIYOKARIBU NAWE. AU UKAWASILIANA NAMI KAMA UTAHITAJI MSAADA WOWOTE.
Ukitaka kuwajua trafic wanavyopiga pesa uhitaji leseni .
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom