Hatua za kufuata unapofikiria kuanza kufanya biashara yoyote

Elisha Chuma

JF-Expert Member
Jul 22, 2013
275
262
Watu tumezoea kudanganyana na kutokuelezana ukweli kuhusiana na biashara. Tumekuwa watu wa kupeana moyo na kushauriana kila mtu afanye iashara lakini biashara au ujasiriamali sio kitu rahisi kiasi hicho ambacho kinaweza kufanywa na kila mtu.

Hivyo usijitumbukize tu katika bishara kwa kufuata mkumbo aidha umeambiwa biashara fulani unaiweza, biashara fulani inalipa au wewe unaweza kufanya biashara fulani na ikakulipa, kila kitu kina ugumu wake na changamoto zake, changamoto za muuza maandazi ni tofauti na changamoto za muuza duka, hata ujuzi wa msusi ni tofauti na wa kinyozi japo wote wapo saluni, hivyo unapoamua kufanya biashara fulani usikurupuke fikiria na tathmini kwanza kwa undani kama inaendana na wewe.

Zifuatazo ni baadhi ya njia au mbinu muongozo za kufuata unapotaka kuanza biashara yako.⠀⠀⠀⠀⠀⠀⠀⠀⠀
⠀⠀⠀⠀⠀⠀⠀⠀⠀
Nitaviandika hapa kwa kuvitaja.⠀⠀
⠀⠀⠀⠀⠀⠀⠀⠀⠀
1. Wazo bora la biashara⠀⠀⠀⠀⠀⠀⠀⠀⠀
2. Utafiti wa kwanza (bajeti, muda, nguvukazi, vifaa, faida, washindani na eneo)⠀⠀⠀⠀⠀⠀⠀⠀⠀
3. Mpango biashara⠀⠀⠀⠀⠀⠀⠀⠀⠀
4. Utafiti wa pili ⠀⠀⠀
⠀⠀⠀⠀⠀⠀ ⠀⠀⠀⠀⠀⠀⠀⠀⠀
Ukiona una nafasi katika biashara hiyo basi fanya na anza mara moja kwa kufuata muongozo wako ulioutengeneza hapo awali, kama unaona nguvu yako ni ndogo kulingana na soko na ulivyojipanga, badilisha mpango uendane na soko pamoja na uwezo wako.⠀⠀⠀⠀⠀⠀⠀⠀⠀
⠀⠀⠀⠀⠀⠀⠀⠀⠀
Nukuu: Uwezo na nguvu ni akili, fedha ni mwezeshaji tu.

Kuna tofauti kubwa kati ya wazo na kitu halisi jitahidi kusimamia na kufanya ulichokiwaza mwanzo⠀⠀⠀⠀⠀⠀⠀⠀⠀
⠀⠀⠀⠀⠀⠀⠀⠀⠀
Elisha Chuma
 
Kamawewe,

Mkuu bandiko la mwisho niliombwa nipunguze nifupishe kidogo maelezo hizi hapa ni dondoo bandiko lenyewe kwa urefu wake na maelezo yake liko kwenye blogu.
 
Mkuu wewe unafanya biashara ya aina gani?

Na soko unalionaje so far?

Sent using Jamii Forums mobile app

nnafanya biashara ya Ushauri,Teknolojia na bidhaa

soko linampokea mtu kama alivyokuja lina misingi yake ukiifata unapata kulingana na nguvu yako lakini pia linachangamoto zake ukizikabili na kuzitatua unapanda kiwango chako sokoni,hivyo soko ni zuri na wateja wapo kwa kila biashara.
 
'Teknolojia na bidhaa.'

Naomba ufafanuzi hapo mkuu ni biashara gani hizo specifically.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
umekuwa ukiweka makala zako humu kuhusu biashara kumbe wewe mwenyewe huna biashara

Motivational speakers mmeanza kurudi tena

mkuu nikuambie tu, ulichokitaja hapo juu si biashara
Tafuta biashara utimize mahubiri yako kimatendo uone kama ni rahisi na si kuongea biashara nyuma ya key board
 
Naona mzee baba bado yuko bize,ngoja tusubiri akirudi atatupa feedback mkuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimekuelewa mkuu Elisha Chuma

Kuna sehemu umesema unajihusisha na ushauri bidhaa na technology, unaweza fafanua kodogo

Sent using Jamii Forums mobile app

Ndio Teknolojia nna biashara ya kufanya dizaini na printing ya matangazo,branding na Webtech ama Website Technology,lakini pia nnarasmisha biashara mtandaoni na kuzisimamia kwa kufuata taratibu stahiki za soko na sheria za mtandao,nna simamia akaunti za biashara mtandaoni kuhakikisha brand na biashara havipishani

Bidhaa ni biashara ambayo nnazalisha bidhaa na kuiweka sokoni,hivyo ni mtengenezaji na muuzaji wa bidhaa zinazotengenezwa chini yangu
 
umekuwa ukiweka makala zako humu kuhusu biashara kumbe wewe mwenyewe huna biashara

Motivational speakers mmeanza kurudi tena

mkuu nikuambie tu, ulichokitaja hapo juu si biashara
Tafuta biashara utimize mahubiri yako kimatendo uone kama ni rahisi na si kuongea biashara nyuma ya key board

Mimi sio motivational usifanye kwa kukariri kwamba kila anaeshauri ni motivational sina motive threads nna reality and coaching threads so mimi ni life coach sipo kukumotivate pitia upya tena mabandiko yangu na kuhusu biashara zipo 4 tofauti zenye matawi kila moja.

Karibu.
 
'Teknolojia nna biashara ya kufanya dizaini na printing ya matangazo,branding na Webtech ama Website Technology'.

Daah kwny maelezo yote hayo nimeelewa hayo maelezo tu hapo juu tu.

Hapo chini ndo sijaelewa kabisa mkuu.

'kuzisimamia kwa kufuata taratibu stahiki za soko na sheria za mtandao,nna simamia akaunti za biashara mtandaoni kuhakikisha brand na biashara havipishani .

Bidhaa ni biashara ambayo nnazalisha bidhaa na kuiweka sokoni,hivyo ni mtengenezaji na muuzaji wa bidhaa zinazotengenezwa chini yangu'

Ndio Teknolojia nna biashara ya kufanya dizaini na printing ya matangazo,branding na Webtech ama Website Technology,lakini pia nnarasmisha biashara mtandaoni na kuzisimamia kwa kufuata taratibu stahiki za soko na sheria za mtandao,nna simamia akaunti za biashara mtandaoni kuhakikisha brand na biashara havipishani

Bidhaa ni biashara ambayo nnazalisha bidhaa na kuiweka sokoni,hivyo ni mtengenezaji na muuzaji wa bidhaa zinazotengenezwa chini yangu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watu tumezoea kudanganyana na kutokuelezana ukweli kuhusiana na biashara. Tumekuwa watu wa kupeana moyo na kushauriana kila mtu afanye iashara lakini biashara au ujasiriamali sio kitu rahisi kiasi hicho ambacho kinaweza kufanywa na kila mtu.

Hivyo usijitumbukize tu katika bishara kwa kufuata mkumbo aidha umeambiwa biashara fulani unaiweza, biashara fulani inalipa au wewe unaweza kufanya biashara fulani na ikakulipa, kila kitu kina ugumu wake na changamoto zake, changamoto za muuza maandazi ni tofauti na changamoto za muuza duka, hata ujuzi wa msusi ni tofauti na wa kinyozi japo wote wapo saluni, hivyo unapoamua kufanya biashara fulani usikurupuke fikiria na tathmini kwanza kwa undani kama inaendana na wewe.

Zifuatazo ni baadhi ya njia au mbinu muongozo za kufuata unapotaka kuanza biashara yako.⠀⠀⠀⠀⠀⠀⠀⠀⠀
⠀⠀⠀⠀⠀⠀⠀⠀⠀
Nitaviandika hapa kwa kuvitaja.⠀⠀
⠀⠀⠀⠀⠀⠀⠀⠀⠀
1. Wazo bora la biashara⠀⠀⠀⠀⠀⠀⠀⠀⠀
2. Utafiti wa kwanza (bajeti, muda, nguvukazi, vifaa, faida, washindani na eneo)⠀⠀⠀⠀⠀⠀⠀⠀⠀
3. Mpango biashara⠀⠀⠀⠀⠀⠀⠀⠀⠀
4. Utafiti wa pili ⠀⠀⠀
⠀⠀⠀⠀⠀⠀ ⠀⠀⠀⠀⠀⠀⠀⠀⠀
Ukiona una nafasi katika biashara hiyo basi fanya na anza mara moja kwa kufuata muongozo wako ulioutengeneza hapo awali, kama unaona nguvu yako ni ndogo kulingana na soko na ulivyojipanga, badilisha mpango uendane na soko pamoja na uwezo wako.⠀⠀⠀⠀⠀⠀⠀⠀⠀
⠀⠀⠀⠀⠀⠀⠀⠀⠀
Nukuu: Uwezo na nguvu ni akili, fedha ni mwezeshaji tu.

Kuna tofauti kubwa kati ya wazo na kitu halisi jitahidi kusimamia na kufanya ulichokiwaza mwanzo⠀⠀⠀⠀⠀⠀⠀⠀⠀
⠀⠀⠀⠀⠀⠀⠀⠀⠀
Elisha Chuma
Brother biashara tunayoisoma katika vitabu tofauti na ile halisi brother

Ndio maana unamkuta mchumi Hana hata kioski Cha kuuza vocha jiulize kwann??

Biashara Ni asili ,biashara Ni talent biashara Ni ujanja wiz, udhulumat,ufitini na katika biashara Kuna meng

Mnaweza mkafungua biashara Moja watu kumi eneo moja alafu mkakuta mwenzenu anakimbiza hataree mkajua karoga kumbe Kuna mbinu za kimedani katumia tu

'Kuna mbinu za kimedani katumia tu'

Hahah wise words mkuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom