Hatua za kufuata ili kuanzisha biashara ya madini Tanzania

Vanlizerfx__

Senior Member
Jul 7, 2021
109
250
Habari wanajamii forums

Leo nimekuja na fursa ya jinsi gani wewe kijana unaweza kuanzisha biashara yako ya kuuza madini

Zifuatazo ni hatuna za kufata jinsi utakavyoweza kununua na kuuza madini

Kusajili kampuni Brela

Kijiandikisha Mlipa Kodi

Kuchukua leseni

Kuchukua Hati ya Usalama wa Mazingira

Kuajiri wafanyakazi na wataalamu wengine

Kununua na kuandaa vifaa mbalimbali

Kutafuta masoko
Kuanza uchimbaji wa majaribio

Kuanza Uchimbaji Wenyewe

1. Kusajili Kampuni

Shirkisha mshauri wa biashara na mwanasheria wa upande wa makampuni ili wakusaidie kwa ushauri na utengenezajiwa memart ambayo ni muhimu katika kusajili kampuni

Unaweza kwenda mwenyewe Brela kusajili au ukamtumia mhsauri mtaalamu wa mambo hayo. Nashauri umtumie mshauri mataalam ili kuokoa gharama za pesa na muda

2. Kijiandikisha Mlipa Kodi kwa kuchukua TIN TRA

Kujiandikisha TIN ni bure na inapatikana kwenye matawi yote ya TRA Tanzania

3. Kuchukua Leseni Wizara ya Nishati na Madini

Baada ya kukamilisha vigezo vya wizara unayo haki sasa ya kuomba leseni ya utafutaji au uchimbaji wa madini ambayo inatolewa na wizara ya Nishati na Madini

4. Kuchukua Hati ya Usalama wa Mazingira

Biashara ya madini ni mojawapo ya biashara inayoharibu mazingira kwa hali ya juu. Ni utaratinu wa mataifa yote duniani kutaka kuwa na uhakika wa utunzaji wa mazingira na hivyo bodi au mamlaka husika watahitaji kuingia mkataba na wewe ili wawe na uhakika kuwa mazingira yatakuwa salama wakati na baada ya uchimbaji.

5. Kuajiri wafanyakazi na wataalamu wengine

Biashara ya madini itahitaji wafanyakazi wa takriban nyanja zote kuanzia wahudumu, maofisa wataalamu na washauri. Hawa wote ni lazima uwaajiri au uwe na uhakika utawapata wapi kwa gharama muafaka

6. Kununua na kuandaa vifaa mbalimbali

Uchimbaji wa madini unatumia technolojia ambazo ndizo zitakazoamua kama wewe ufanikishe mradi au la. Teknolojia ya zamani ianweza kukupa hasara japo rahisi, teknolojia za kienyeji nazo zinaweza kukupa hasara. Teknolojia za kisasa zina faida japo ni ghali kununua. Unashauriwa kuwa na wataalamu washauri wa kukushauri tangu mwanzo namna ya kuamua juu ya teknolojia utakayotumia.

Kwa nini teknolojia za kienyeji au za zamani zina hasara?

Nyingi ya hizo zinatumia muda mrefu kuleta matokeo

Zina gharama kubwa za uendeshaji

Zinaharibu mazingira

Zinahitaji wafanyakazi wengi

Nk

7. Kutafuta masoko

Kulingana na ukubwa wa uchimbaji au utafutaji, ni vyema kutafuta masoko ambayo utauza madini. Ikiwezekana uingie na mikataba ili uwe na uhakika wa kuuza punde utakapovuna.

8. Kuanza uchimbaji wa majaribio

Fanya uchimbaji wa majaribio angalau kwa miezi mitatu hadi sita kwa uchimbaji mkubwa kidogo unaweza kwenda hadi mwaka mmoja. Uchimbaji wa majaribio itakupa fursa ya kujua yafuatayo:

Je vifaa vitafaa kwa malengo yako

Je wafanyakazi uliowaajiri wanaweza kufanya uzalishaji wenye tija

Je biashara nzima italeta tija iliyokusudiwa

9. Kuanza uchimbaji Halisi

Baada ya uchimbaji wa majaribio, sasa unaweza kwa ujasiri kabisa kuanza kuchima madini. Muhimu tu ni kwamba yafanyie kazi changamoto zote zilziojitokeza kwenye uchimbaji wa majaribio
 

mugah di matheo

JF-Expert Member
Jul 28, 2018
4,778
2,000
Habari wanajamii forums

Leo nimekuja na fursa ya jinsi gani wewe kijana unaweza kuanzisha biashara yako ya kuuza madini

Zifuatazo ni hatuna za kufata jinsi utakavyoweza kununua na kuuza madini

Kusajili kampuni Brela
Wewe ni mtaalam kwenye hii secta?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom