Hatua za kuchukua kumsaidia mtu aliyeanza kupoteza uwezo wa kusikia na kupata ukiziwi

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,500
9,279
Mtu anapogundua kuwa amepata tatizo la kusikia anashauriwa mara moja kwenda kituo cha afya kilichoko karibu na kuomba kuonana na mtaalam wa masikio Ili ampime uwezo wake wa kusikia.

Matumizi ya Mashine ya masikio:

Mtu anapogundulika ameanza kupata ukiziwi, atapewa msaada wa kitaalam kuendana na aina yake ya kusikia. Zipo aina tatu za ukiziwi.

Kiziwi Namba moja na mbili wanaweza kushauriwa kutumia mashine kuwasaidia kusikia kwani wao zinawasaidia kwa sababu Wanasikia nusu.

Kiziwi Namba 3 hapendi kutumia mashine ya kusikia huwa anapenda kutumia mkalimani wa lugha za Alama kwa sababu anapotumia mashine zinamsababishia matatizo ya kumuumiza kichwa kutokana na makelele yanayokusanyika na yanakuwa kama sauti za kiwandani hivyo kumsabibishia maumivu ya kichwa.

Hatua za familia na watu wa karibu kuchukua:

Familia ya mtoto kiziwi inatakiwa kupewa msaada wa kuishauri na wataalamu Ili wakubaliane na hali hiyo sababu wengi wanapoteza muda na rasilimali kujaribu kurudisha usikivu kitu ambacho hakiwezekani. Baada ya kukubaliana na Hali ya ukiziwi wanatakiwa wampeleke mtoto shule maalum ya viziwi ambapo atajifunza lugha ya Alama na kukutana na viziwi wenzake Hali itakayomfanya ajione hayuko peke yake.

Unapolazimisha kumpeleka mtoto shule isiyo ya viziwi ni mwanzo wa kumfanya awe na mawazo, atakosa furaha kwa sababu kwanza hatapata msaada ambao angepata kwenye shule maalum kwani hakuna walimu wanaojua lugha ya Alama kumsaidia.

Asilimia kubwa ya viziwi Namba 3 ambao walipelekwa shule zisizo za viziwi wameishia kukimbia masomo bila kumaliza kutokana na mazingira magumu wanayokutana nayo.

Imeandaliwa na:

FUWAVITA
 
Maelezo yako hayajakamilika sababu hujataja aina 3 za uziwi na ukoje? Mimi kama msomaji wa mada yako hii bado sijaelewa aina za ukiziwi unaozungumza?

Nijuavyo mimi kuna aina 2 za ukiziwi yaani kuzaliwa na ukubwani.
 
Back
Top Bottom