Hatua za haraka zinahitajika, Wafuatao wameihujumu CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hatua za haraka zinahitajika, Wafuatao wameihujumu CCM

Discussion in 'Chaguzi Ndogo' started by JacksonMichael, Apr 2, 2012.

 1. J

  JacksonMichael JF-Expert Member

  #1
  Apr 2, 2012
  Joined: Mar 22, 2012
  Messages: 339
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu zangu wana JF,
  Awali ya yote naomba niwapongeze kwa ushindi KIDUCHU mlioupata kule ARUMERU, kiukweli sikupenda CDM iibuke washindi ila nilipenda CCM ishindwe. Ninakiri kuwa kuna tatizo kubwa sana tokea kura za maoni, nguvu ya ushawishi na pesa nyingi zilisababisha SIOI ashinde ilihali kulikuwa na viashiria vya rushwa!

  Kuna sababu nyingi zilizopelekea CCM kutoshinda uchaguzi ule ambazo kiukweli zimenikosesha raha na hata kutype kwenye keyboard nashindwa!

  1) Lusinde alipunguza idadi ya kura Arumeru kwa kiasi kikubwa, ukitumia lugha mbaya kama zile usitegemee mtu akuchague, inshort ningekuwa na maamuzi katika CCM lusinde ningemnyang'anya kadi ya chama.

  2) Waliokuwa ndio wanaongoza kampeni hawakuweza kutoa sababu ni kwa nini muda wote ambao jimbo lilikuwa chini ya CCM na kero mbali mbali hazikushughulikiwa na leo wanaahidi kuzishughulikia, Mfano: Ni ukweli usiopingika mtu kama MKAPA hawezi kuwashawishi wana ARUMERU kuwa atamshauri Kikwete wakati alikuwa Rais na hakuweza kutekeleza matatizo hayo. Mi nafikili ilitakiwa kwa wanaccm kukiri makosa na kuonyesha ni kwa vipi watasahihisha makosa yao, Lakini baada ya kutumia njia hii wakajikuta WANAROPOKWA na kutumia lugah zisizo na staha.

  3) Kutumia watu wenye kashfa na wanaoongoza katika makundi katika CCM tena hao hao wanajulikana kuwa hawapo katika kundi moja kama OLE SENDEKA na LOWASA, hii ilidhihirisha Unafiki wa aina yake, Haiingii akilini watu hawa ambao kila kukicha wanaitana mafisadi na kushutumiana mbele ya camera za waandishi leo wanapanda jukwaa moja. Tatizo kubwa ni kuwa wanayoyasema na wanayotatenda ni tofauti tena kwa nyuzi 180[SUP]0[/SUP](Diferent Direction)

  4) UVCCM hasa wa arusha nao hawakwepeki katika hili, katika kufikili wanawakomoa wale waliopinga uteuzi wa sioi kwa kuwa unanuka harufu ya rushwa na wengine waliotilia shaka juu ya uteuzi wa sioi wao wakatumia nguvu na wingi wa kura zao kumchagua Sioi lilikuwa kosa la kihistoria.

  5) Hakukuwa na kauli ya pamoja katika kampeni za CCM kila aliyepanda jukwaani alisema yake, in short ilikuwa kama watu wamechanganyikiwa.

  Conclusion:
  Huu ni uthibitisho kuwa LOWASA na kundi lake hawakubaliki katika jamii, na CCM isije kufanya kosa 2015

  Hongera CDM ingawa ushindi wenu unatokana na UJINGA na UDHAIFU wa CCM
   
 2. z

  zamlock JF-Expert Member

  #2
  Apr 2, 2012
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 3,849
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  ndo siasa hiyo
   
 3. dallazz

  dallazz Senior Member

  #3
  Apr 2, 2012
  Joined: Aug 6, 2011
  Messages: 106
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  ​asante
   
 4. M

  Molemo JF-Expert Member

  #4
  Apr 2, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Hovyoooooooooo!!!!!!!!!!!
   
 5. M

  Mr KK New Member

  #5
  Apr 2, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Wewe ni mnafiki huna lolote, hayo makosa yenu unatwambia sisi ili iweje, nenda kazungumze huo ujinga wenu kwenye vikao vyenu na hili ndilo anguko la CCM. Tayari katika bara la Africa tumeshuhudia vyama kadhaa vikongwe vikianguka na sasa ni zamu yenu buriani CCM.
   
 6. mshikachuma

  mshikachuma JF-Expert Member

  #6
  Apr 2, 2012
  Joined: Dec 2, 2010
  Messages: 2,853
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Wasubiri Ritz na Rejeo ili upate maoni yao hapa hapa
   
 7. Myakubanga

  Myakubanga JF-Expert Member

  #7
  Apr 2, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 5,781
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  Mfa maji...
   
 8. Chum Chang

  Chum Chang JF-Expert Member

  #8
  Apr 2, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 1,001
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Ndio hatma ya dhulma kwa ale zulumiwa
   
 9. N

  NICE LAMECK JF-Expert Member

  #9
  Apr 2, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 213
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Acha huo uhoro kawaambie wenzako huko sijui utawapata wapi na sasa hivi hawapatikani na cm zao zimefungwa.
   
 10. t

  tarita Senior Member

  #10
  Apr 2, 2012
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 156
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Laana ya Mwalimu JKNyerere itawatafuna hadi kifo.Je sasa mmeamini Vincent Nyerere nifamilia ya Mwlm?
  Kama baba yake amewanyoa nywele za kisogoni, zinauma mno. Mkapa ulimpiga Vincent kofi la jichoni ukamuuliza unaona? Amekutwanga kofi la sikioni je Mkapa umesikia?
   
 11. Eros

  Eros JF-Expert Member

  #11
  Apr 2, 2012
  Joined: Jan 13, 2012
  Messages: 316
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 60
  Umeyajua leo? nakumbuka jana ulikuwa unasubiri kura za vijijini.ulifikiri vijijini hawaelewi kinacho
  endelea nchini?MMEPOTEZA MVUTO KWA ULAFI WENU.WANANCHI WAMEJUA HAKI ZAO.
   
 12. MtamaMchungu

  MtamaMchungu JF-Expert Member

  #12
  Apr 2, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 3,696
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  In short, all of that is none of our concern. We've won and that's all that matters. Kelele kama hizi mtazipiga sana 2015, and even then it wont matter to us.
   
 13. M

  MKALIKENYA JF-Expert Member

  #13
  Apr 2, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 1,198
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 133
  Kwenye hiyo list nawaongeza hawa
  1.MKAPA
  2.MARY NAGU
  3.LOWASSA
  4.OLE MADEYE
   
 14. v

  vngenge JF-Expert Member

  #14
  Apr 2, 2012
  Joined: Apr 19, 2011
  Messages: 366
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Low hasa anakubalika kusimama kwake jukwaani kumeongeza kura nyingi sana vinginevyo hali ingekuwa ngumu zaidi. Kuumwa kwake kumeathiri sana, angeshiriki toka mwanzo nadhani tungesema mengine. Anafaa huyu jamaa apewe nafasi kupeperusha bendera 2015. Kilicho mcost Sioi ni ile tu baba yake kuwa ndo anamrithi na ubunge, kwa mazingira ya sasa watu wengi wasingekubali kwenye jimbo lolote pia suala la utata wa uraia nalo lilicount
   
 15. t

  tongi JF-Expert Member

  #15
  Apr 2, 2012
  Joined: Mar 18, 2012
  Messages: 451
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  unajua kusoma na kuandika, lakini hakuna ujumbe wowote wa maana kwenye maandiko yako
   
 16. t

  tongi JF-Expert Member

  #16
  Apr 2, 2012
  Joined: Mar 18, 2012
  Messages: 451
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  nyie ndio mnatumwa na lowassa, mtajijuu, chagueni yoyote yule 2015 ni cdm tu
   
 17. F

  FredKavishe Verified User

  #17
  Apr 2, 2012
  Joined: Dec 4, 2010
  Messages: 1,090
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Na sasa mtu anafungwa sikutokana na mistake ndugu
  One mistake two goals hahaha sio one goal tena hapa maana tumepiga uncle ben,lowassa,wassira,nape wote chakaza chakaza kama mnataka rematch hamjaamini yaliotoke
  Rematch jimbo la segerea
   
 18. Safety last

  Safety last JF-Expert Member

  #18
  Apr 2, 2012
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 4,224
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Ondoa upumbafu wako hapa kaongeeni na wajinga wenzenu
   
 19. Gracious

  Gracious JF-Expert Member

  #19
  Apr 2, 2012
  Joined: Jul 12, 2011
  Messages: 1,750
  Likes Received: 343
  Trophy Points: 180
  kuhakikishia Uchaguzi mdogo wowote utakaotokea Kuanzia sasa,CHADEMA watashinda zote hadi 2015.Hakuna sijui cha makosa yenu wala nini? Wewe ndo ulikua unajitapa hapa oooh,mtashinda.Kwa nini hukutoa maangalizo hayo kwenye timu yenu ya kampeni? Mkuu,this is an Indicator for your Information.Hata JK angeenda wembe ni uleule.

  Eti Ushindi kiduchu.Upi ni kiduchu kati ya huu na ule wa kwenu wa kuchakachua kule Igunga?

  Pole lakini.Najua umepata wakati mgumu hata kuandika thread hii.Umeonyesha ukomavu
   
 20. M

  Makupa JF-Expert Member

  #20
  Apr 2, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,742
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Mkuu uchambuzi umekwenda shule, ila naamini kabisa kuwa Lusinde ndio alichangia kwa silimia zaidi ya sabini ni kimsingi haitaji kuwa na shahada kugundua hilo. Lusinde anastaahili afukuzwe kwenye chama mara moja.
   
Loading...