Hatua za haraka zinahitajika kusimamisha vita (Civil War) Ngara

:Cry::Cry::Cry::Cry::Cry::Cry::Cry::Cry: hivi kweli hii ni nchi ya amani :noidea::noidea::yield:
 
Wafugaji Rwanda waua Watanzania sita Ngara



*Kamati ya Ulinzi na Usalama yasaka watuhumiwa

Na Theonestina Juma, Bukoba

WATANZANIA sita ambao ni wakulima wa Kijiji cha Murbanga Kata ya Mursagamba wilayani Ngara mkoani Kagera wamevamiwa shambani na kuua kikatili na
wafugaji wanaosaidikiwa kuwa ni raia wa Rwanda.

Tukio hilo lilitokea juzi usiku wakati wakulima hao wa Tanzania wakiwa wamepiga kambi katika eneo la pori lililoko katika kijiji hicho, kwa ajili ya kuandaa mashamba kwa kusubiri mvua za vuli na kulinda mazao yao yasishambuliwe na wanyama.

Habari za uhakika zilizopatikana kutoka wilayani humo na kuthibitishwa na Kaimu Kamanda wa polisi mkoani Kagera, Bw. Vitus Mlolere zinasema kuwa waliouwa ni wanaume.

Habari hizo zinadai kuwa katika tukio hilo, wafugaji hao ambao ni raia wa Rwanda (idadi haijafahamika) walipowakukuta watu hao katika mashamba yao ambako wamejenga vibanda vya muda kwa ajili ya kupumzikia, waliwakamata na kuwafunga kamba mikono kwa nyuma na kuanza kuwashushia kipigo kwa kutumia fimbo na marugu hadi kufa.

Wakulima hao walikuwa wanane, wawili kati yao walikimbia na kunusurika katika mauaji hayo.Miongoni mwa walionusurika mmoja alikimbia hadi kwa wananchi wanaoishi jirani na kutoa taarifa.

Kwa sasa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Ngara kwa kushirikiana na polisi kutoka Kituo Kikuu cha Polisi mjini hapa imepiga kambi katika pori hilo kufuatilia tukio hilo ikiwa ni pamoja na kuwasaka Wanyarwanda hao wanaosakidiwa kufanya mauaji hayo.

Kati ya waliouawa, watatu wametambulika kuwa ni Bw. Karabanye Daniel (70), Benedict Bashogongo (65) na Selestine Mawela (47).

Wakulima wa Kata ya Mursagamba kila mara wamekuwa wakizozana na wafugaji wa Kinyarwanda kwa kuacha mifugo yao kushambulia mzao yao kila kukicha.

Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Bw. Mlolere alisema kuwa atatoa taarifa za mauaji hayo leo.

Source Majira
 
Watu wanatoka nchi jirani na kukamata wananchi wetu,kuwafunga kamba,kisha kuwaua kikatili na viongozi wetu wa juu wamestarehe tuu na kunywa chai? kweli sisi ni mazoba. Na bado wako watu wakawaida kabisa miongoni mwetu wanasimama kidete kuitetea serikali hii kwa utendaji huu na uwajibikaji huu?
Nimekumbuka ile kauli wakati wa kampeni 2010 kuwa kuichagua CCM ni JANGA.
 
sisi tulikua na jamaa maarufu sana na mchapakazi i think never seen before, alikua diwani na meya bukoba vijijini hayati kachwamba,huyu mh.alijitaidi kuwabana wasio wajibika hasahasa polisi,walimu n.k,.akatuahidi kumaliza tatizo la wanyarwanda by then,lakini wanyarwanda wakasomba mifugo yao na kumpelekea,kama zawadi,mwisho wa riku aliwatetea wanyarwanda mpaka mahuti yanamkuta.viongozi wetu wako tiyari kutusaliti wazawa!
 
Taarifa za sasa ni kuwa RPC amethibitisha kuwa watu 6 ndio wameuawa! Kama tunavyojua pale serikali inapokuwa imefanya kosa, siyo rahisi kukubali. Always wanapunguza idadi ya waliouawa na/au kujeruhiwa. Taarifa zinasema walitumia mishale ya sumu, marungu na fimbo.

Shame on Kikwete and his poor governance!
 
ndio shukrani za kuwatunza kipindi cha vita! Babu (mbunge wa ngara) anasemaje?, sidhani kama ataongea make nasikia yeye pia ni damu ya rwanda!
 
Walioko Ngara au mwanza, Mbunge wa Ngara amesema nini? Au hayamhusu?
 
Yes
Keep watching ,tupo njiani kupata taarifa hii kwa ukweli,punde mnaweza kuona hata video hapa hapa.

belived watu 6 wameuawa katiika rabsha hizo.

tunakwenda kwa siri sana unajua hapa kagera kuna maeneo ni HATARI SANA kwa sisi kama waandishi kufika na kupiga picha nk

Subiri tu.

Tutapata lini picha kama ulivyotuahidi? Au umekwama? Pole kwa kazi ngumu.
 
Kila pembe ya Tanzania sasa kuna migogoro ya ardhi,si dar,mara,manyara,arusha,kagera n.k,tutarajie makubwa zaidi na hasahasa madhara!
 
Kila pembe ya Tanzania sasa kuna migogoro ya ardhi,si dar,mara,manyara,arusha,kagera n.k,tutarajie makubwa zaidi na hasahasa madhara!

Itabidi na watz tuanze kujiunga na jeshi ili tuweze kujihami. maana nchi yote inakaribia kuisha kwa kuuzwa kwa wageni! Tulikuwa tunawategemea polisi; sasa tumeona kazi ya polisi Arusha, Tarime, Manyara, na huko kusini. Usitegemee kulindwa na polisi au jeshi; Jilinde mwenyewe
 
ndugu wanajamii,
Nadhani hili swala tusilitazame kwa mtazamoa wa kisiasa. Hapa tunazungumzia maisha ya watu ambao wanaishi eneo moja na pia ni ndugu kasoro ni kuwa kuna mpaka kati yao. Pili, viongozi wanafanya kazi yao ikiwa ni pamoja na kuwapa watu ambao siyo watanzania vibali vya kuishi nchini. Kama mgeni amepewa kibali cha kuishi na kuishi kwenyewe ikawa ilielezwa kuwa ni kuishi kwa kufuga, then itakuwa ngumu kwa viongozi hao kuwanyang'anya vibali bila sababu maalum.
Tatu, je ukweli ulikuwa upi? Viongozi hawatakiwi kukurupuka na kusema au kuchukua uamuzi bila kujua ukweli wa tukio lenyewe. Wanatakiwa wapate ukweli wote ili wachukue uamuzi sahihi. Kwa mfano, mtu anaweza kujiuliza maswali: Je nani aliyeanzisha tatizo lililosababisha kutokea kwa vurugu zilizoleta maafa? Je, hakuna watanzania waliosababisha vurugu hizo pengine zingeweza kuzuiliwa?
Nne, nimesikiliza mmoja wa waliohojiwa akidai kuwa ng'ombe walikuwa ni chanzo cha vurugu baada ya wananchi kuchukua mifugo hiyo kwa sababu ilikuwa imeingia kwenye mashamba yao na kuwa kabla ya kupeleka malalamiko yao katika ngazi husika, walichinja ng'ombe wawili kwa kujipongeza. Je, kama huyu mwananchi kaeleza ukweli, watu hao walikuwa wamechukua uamuzi wa busara?
Ninachoomba Wanajamii, ni vizuri tukatoa michango ambayo inalenga kutafuta solutions za matatizo yanayojitokeza bila kuingia sana kwenye siasa. Siasa itakuwa nzuri iwapo utakuwa umewaza jinsi ya kujitatulia matatizo yanayokukabili.
Siku njema.
AA
 
Back
Top Bottom