Hatua za China za kuleta amani na mshikamano hazipaswi kupotoshwa kuwa ukandamizaji wa kidini au kikabila

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,034
6.jpg
Baadhi ya watu duniani wanahusisha uislamu na ugaidi, ufarakanishaji na vita, na vyombo vya habari hasa vya nchi za magharibi, vimekuwa vikipaza sauti za maoni hayo kuhusisha maeneo ya Mashariki ya Kati, Afrika Kaskazini, Afghanistan na kwengineko.

Lakini wachina waislamu, wanaamini kuwa picha hii mbaya kuhusu Uislamu haiendani na hali halisi, kwani uislamu ni dini ya amani, na ni msingi wa ustaarabu tofauti ambao umeenea kwa zaidi ya miaka 1,500 iliyopita, kila kona ya ulimwengu ikiwemo China.

Tangu enzi na dahari, waislamu wa China wamekuwa wakiishi kwa masikilizano na wachina wa makabila na dini nyingine, na waislamu wa China pia wanaendesha mambo yanayohusu dini yao bila kuzuia. Mwaka 1953 China ilianzisha Shirikisho la Kiislamu la China ambalo linasimamiwa na waislamu wenyewe, na inapohitajika serikali inatoa miongozo au maelekezo kuhusu mambo yanayohusu dini hiyo na taifa.

Kuna makabila madogo 10 nchini China ambayo yana waumini wengi wa dini ya Kiislamu, na jumla yao inakadiriwa kuwa zaidi ya milioni 20, wengi wakiwa wanatoka makabila ya Wauighur, wakazakh na wahui wanaoishi mkoa wa Xinjiang pamoja na mikoa ya Ningxia, Qinghai na Gansu, wote wakiwa na uhuru wa kuamini dini.

Nimetembelea baadhi ya mikoa hiyo, na hivi karibuni nilitembelea mkoa wa Xinjiang, na kubahatika kuongea na mashehe wa misikiti pamoja na waislamu wa kawaida. Wote wanasema kwamba wanaendesha shughuli zao bila ya kubughudhiwa au kukerwa na yeyote.

Hivyo nashangaa na kujiuliza maswali mengi pale ninapoona vyombo vya habari vya magharibi vinapokosoa na kutoa habari za kupotosha kwamba serikali ya China inakandamiza dini ya Kiislamu.

Tukiwa kama waandishi, tunasahau kwamba maneno yanazaliwa mdomoni na kufia masikioni, lakini kuna baadhi yanakwenda kuzama mioyoni, na kusababisha jeraha kubwa ikiwemo chuki na hasira. Kauli hizi za uchochezi kutoka vyombo vingi vya habari haswa vya magharibi vinavyoandika habari kwa upendeleo na bila kutafuta ukweli wa mambo kwa kuvutia tu mteja wao ambaye ni msomaji, huwa vinawachukiza waislamu duniani.

Vyombo vya habari vya magharibi mara kwa mara vimekuwa vikiulenga zaidi mkoa wa Xinjiang na kudai kwamba lengo la China ni kutokomeza Uislamu nchini China. Na baadhi ya wanasiasa wa nchi hizo za magharibi, wanatumia fursa hii kama njia ya kujipatia mafanikio ya siasa za kijiografia.

Waswahili tuna msemo maarufu kwamba “Usipoziba ufa utajenga ukuta”. Bila shaka nchi yoyote ile inapaswa kuchukua hatua haraka na mapema pale tu inapoanza kuona dalili mbaya ya jambo lolote, na kwa hili naisifu China kwani huwa inajaribu kuung’oa mche mbaya pale unapoanza kuchomoza tu, kabla ya kukua na kuleta majanga. Ndio maana baadhi ya nchi zimekuwa zikisumbuliwa sana na ugaidi pamoja na vikundi vyenye misimamo mikali. Hii inatokana na kulea tatizo hadi mwisho linashindwa kutatuliwa.

Hatua za China katika kuhakikisha nchi inakuwa tulivu na watu wake wote wanashikamana na kuwa kitu kimoja, hazina lengo la kukandamiza dini au kabila lolote. Ni kweli watu wana haki ya kuwa na maoni na mitazamo yao, lakini badala ya kutoa madai yasiyo na ukweli, ni vyema kwanza wakatathmini historia ya China, na jinsi inavyotaka kuhakikisha amani inatawala nchini pamoja na watu wake kufanya shughuli za kidini huku wakifuata sheria za nchi.
 
Tatizo lililopo ni kuwa kinyume na mstari wa mwisho kabisa wa hoja yako, shida huwa inakuja pale ambapo waislam(uislam?) Wanapogoma kufuata sheria za nchi na badala yake wanataka nchi ifuate sheria zao regardless,ukiona mahali waislam wanaishi kwa utulivu ujue wamebanwa mbavu sawasawa!!
 
Kuna aina ya Waislamu wakiwa wengi nchi yoyote wanaleta sheria zao na kutaka ndio zitumike kwenye locality. Wanataka tamaduni za Kiarabu na nchi nyingine za Kiislamu ndio zitumike kwa sababu ya ufahari na kuziona timilifu. Sasa hayo mambo huwezi wapelekea nchi zenye utamadunia wa miaka zaidi ya 3000 kama China na Japan

Ndio maana wataendelea kuvutana wale wa Uighur na serikali ya China. Hata Myanmar (Burma) ina Waislamu wa Rohingya walitaka kuleta utaratibu wao tofauti, kilichotokea rais wake aliyetoka kuchukua tuzo ya amani ya Nobel tena aliyedumu ni mtetezi wa haki za binadamu kwa miaka zaidi ya 20 aliwatimua watu kama milioni kasoro wakawa wakimbizi miaka ya 2010s. Na nchi nzima ilimkubalia, tena raia walimsaidia hiyo kazi

India pale Waislamu wabishi wanaodhiaki imani nyingine 'za uongo' walikuwa wanachinja ng'ombe mbele ya Wahindu wanaoamini ng'ombe ni Mungu. Wanataka ustaarabu wao ndio utumike, we unaazaje mvalisha Mhindi kanzu na kikofia kile kwa ushawishi wa nguvu. Matokeo yake Wahindu wakawa wakorofi na usiombe mapigano yazuke, aisee Wahindu wanapiga balaa

Nani anaweza toa ustaarabu wa Kimasai kwenda kuulazimisha pale Qatar, Iran au Kuwait
 
labda iwe ktk maandiko tu lkn waislamu hawako hivyo!
Ogopa watu wanakwenda kulipua na kuua wengine tena bila hatia! Tena wakiamini watakwenda mbinguni!
 
Back
Top Bottom