Hatua ya BOT kuhakikisha riba inayotozwa na mabenki inashuka, inahusu na riba ya mkopo ya wafanyakazi itayotolewa na Mabenki ya Biashara?

Nilikwenda benki moja nikaambiwa mpaka sasa hawajapokea taarifa rasimi juu ya hilo na Meneja wa Benki akaonyesha wasiwasi kuhusu hatua hii ya BOT kama kweli itatekelezwa.
Kwa hiyo inawezekana hii ilikuwa ni siasa kama siasa nyingine?
 
Nimesoma taarifa ya BOT inayoongelea kushusha riba kwa wakopaji katika mabenki ya kibiashara lakini nimeshindwa kuelewa kama punguzo hilo litagusa mikopo inayotolewa na mabenki kwa wafanyakazi


Nauliza hivi kwasababu taarifa ya BOT inaongelea punguzo kwa sekta binafs pamoja na sekta ya kilimo.Sasa najiuliza mikopo ya wafanyakazi ni sehemu ya hiyo mikopo ya sekta binafsi iliyotajwa katika taarifa hiyo?

Waandishi wa habari kama waajiriwa, walishindwa kuuliza hata jambo linalowagusa wao wenyewe kama wafanyakazi?

Kama punguzo hilo halihusu wafanyakazi, je BOT watakuwa wametenda haki kwa wafanyakazi wa nchi hii?

Tukumbuke mikopo ya wafanyakazi riba zake katika mabenki ya biashara hufikia asilimia 16 mpaka asilimia 17.

Au ndio mpaka watumishi walalamike kisha Mama aunde kamati ya kumshauri juu ya hili?

Taarifa ya BOT kuhusu punguzo hilo la riba kwa sekta binafsi inapatikana pia kupitia uzi huu hapa chini:


IMG-20211109-WA0093.jpg


IMG-20211109-WA0094.jpg
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom