Jun 15, 2021
6
14
Katika ulimwengu huu ambao ujasiliamali umehubiriwa sana kila mmoja anataka kuwa boss, kila mtu anawaza kuanzisha biashara yake, kuna biashara nyingi zinaanzishwa kila siku lakini kuna biashara nyingi zinakufa kila siku. Ni biashara chache sana ndio zinafikia hatua ya tano, nyingi huishia hatua za nyuma. Kila hatua ina mazuri na changamoto zake, jambo la hatari ni kwamba, changamoto zilizo katika kila hatua zinatosha kuiangamiza biashara hiyo kama hazitazingatiwa.

HATUA YA KWANZA: KUWEPO KWENYE SOKO​

Katika hatua hii, biashara inapambana kupata wateja na kufikisha bidhaa au huduma kwa wateja. Mmiliki anafanya kila kazi muhimu ikiwa ni pamoja na kusimamia wasaidizi wake. Hiki ni kipindi kigumu sana, kwa sababu soko linaweza kukupa picha tofauti na matarajio yake kwa sababu ni kipindi ambacho unatamani soko likukubali lakini soko linasita kwa sababu halina imani kubwa na wewe. Kuna biashara nyingi huishia hapa na mitaji mingi hupotelea hapa.​

HATUA YA PILI: KUISHI KWENYE SOKO​

Biashara iliyovuka hatua ya kwanza itaingia hatua ya pili. Hii nayo ni hatua yenye changamoto nyingi, hapa mfanya biashara anawaza je ataweza kufanya mauzo ya kutosha kulipa gharama za uendeshaji wa biashara na kuhakikisha biashara inakua na huduma zinaboreshwa? Hii ni hatua ambayo bado biashara haina uwezo wa kubeba mzigo mkubwa wa gharama, ni muda wa kujiimarisha kwa kutanua wigo wa masoko ili kupata mauzo makubwa yatakayoipa biashara yako stability. Usipokuwa makini unaweza kufunga biashara au kukaa hatua hii kwa muda mrefu sana.

HATUA YA TATU: HATUA YA MAFANIKIO​

Katika hatua hii, biashara imepata stability nzuri, faida nzuri inapatikana na mambo mengi yanaenda vizuri. Changamoto anayopata mmiliki katika hatua hii ni kuamu je, aendelee na hali iliyopo ili aundelee kukusanya faida au ajaribu kutoka hapo na akue na kuwa kampuni kubwa. Shida ni kwamba, kitendo cha kukua zaidi kitanyonya pesa na mali za kampuni kwa kiasi kikubwa jambo ambalo ni risk kubwa. Maana kama mipango yako haitafanikiwa kampuni itafilisika. Kwa upande mwingine, kama mipango ikifanikiwa, ukuaji huo utawezesha kupata faida kubwa na kuifanya kampuni iingie katika hatua ya nne.


HATUA YA NNE: BIASHARA INAPAA

Hii ni hatua nzuri kwa kuambiwa lakini ni hatua ngumu sana kwa mmiliki wa biashara. Hii ni kwa sababu biashara ikishafikia hatua hii pesa haitoshi kwa sababu ya mambo yanayoambatana na ukuaji huo. Mmiliki atalazimika kuajiri na kugawa majukumu kwa wakuu wa idara ili yeye ajikite kwenye mikakati ya ukuaji na si shughuli za kila siku. Madaraka yatashushwa chini (decentralization) ili kuwezesha maamuzi kufanyika katika ngazi za brach, kampuni itakuwa na wafanyakazi wengi na changamoto za mambo ya utawala na fedha zitaongeza. Katika hatua hii mmiliki wa kampuni, kwa kupenda au kutopenda anaweza kuondolewa kwenye utawala na wawekezaji ili kusaidia ukuaji unaokusudiwa ufikiwe.​


HATUA YA TANO: UKOMAVU WA RASILIMALI​

Hii ni hatua ya mwisho katika ukuaji wa kampuni. Jambo kubwa katika hatua hii ni kukusanya na kuweka pamoja faida na mazuri yote yaliyopatikana kutokana na ukuaji na kutunza mazuri yaliyopatikana kutoka mwanzo, Katika hatua hii kampuni itakuwa na uwezo mkubwa kifedha, wafanyakazi bora, mifumo imara na soko kubwa. Vitu hivi vikitumika vizuri kampuni itakuwa na uwezo wa kukamata soko na kuwa kampuni kubwa ambayo itafanya biashara mahali popote kwa viwango vya hali ya juu na kwa ushindani mkubwa.​


Je unajua biashara yako iko hatua gani? Na je unajua ni nini unatakiwa kufanya na nini hutakiwi kufanya kulingana na hatua ya biashara yako?

Wasiliana nasi kwa ushauri.
 
Back
Top Bottom