Hatua kali zichukuliwe wauguzi wanaofanya mikakati ya upasuaji wajawazito ili wapige pesa Hospitali ya Butiama

Timber TZA

New Member
Jun 1, 2020
4
3
HATUA KALI ZICHUKULIWE WAUGUZI WANAOFANYA MIKAKATI YA UPASUAJI WAJAWAZITO ILI WAPIGE PESA HOSPITALI YA BUTIAMA

Mbunge wa Jimbo la Butiama Jumanne Sagini amemtaka mkurugenzi wa halmashauri hiyo kuchukua hatua kali kwa watoa huduma za afya watakaobainika wakifanya mikakati ya kuwazalisha kwa njia ya upasuaji wajawazito ili wapate fedha pindi watakapo nunua vifaa, katika Hopitali ya Wilaya ya Butiama mkoani Mara.

Hayo yamejiri kwenye Mkutano wake wa Hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Kibubwa Kata ya Butuguri mara baada ya Ziara ya Ukaguzi wa Miradi Mbalimbali, Sagini amesema kuwa hospitali hiyo ya Butiama imekuwa ikilalamikiwa mara nyingi kutokana na wauguzi kutoa lugha inayodhalilisha wagonjwa.

"Nitalifuatilia kwa ukaribu sana na kujua ukweli juu ya mgonjwa anayefika kuongezewa damu chupa moja lakini wao wanataka ulipe chupa tatu na usipofanya hivyo mgonjwa haruhusiwi kutoka hospitali. Pia wanaambiwa hakuna dawa lakini cha kushangaza ni kwamba pindi wanapotoka kwa lengo la kutafuta dawa hizo wauguzi wanawakimbilia ili kuwauzia dawa hizo na vifaa," ameeleza Sagini.

Awali kwenye mkutano huo wananchi wamewalalamikia wauguzi wa hospitali ya wilaya kwa kitendo cha kuficha madawa na kuwauzia wagonjwa hali inayopelekea kushindwa kutimiza wajibu wao.

Kwa upande wake Mwajuma Abdallah amesema kuwa kinachowavunja moyo ni pale wanapoenda kuchoma sindano za masaa, kwenye dozi wameelekeza uchomwe mchana badala yake wanachoma usiku na kusababisha kutumia gharama kubwa za usafiri kurudi nyumbani. ATTACH=full]1718814[/ATTACH]
_MG_6490.jpg
View attachment 1718815
 
Back
Top Bottom