Hatua kali zichukuliwe kwa mabasi ya shule yanayozidisha abiria

marveljt

JF-Expert Member
Jan 11, 2017
1,503
1,479
Wizara ya usafirishaji,wizara ya elimu,wizara ya mambo ya ndani wafanye jitihada wakishirikiana na wananchi wote. Si ajabu kukuta basi la kubeba wanafunzi likiwa na wanafunzi zaidi ya kiwango chake.hiki kitu nimekiona dar,arusha,mwanza,shy n.k

Panatakiwa usimamizi mkubwa na endelevu,si ajabu kukita noah ina watoto zaidi ya 15+, hiace ina watoto 30+, coaster ina watoto 50+.

Jeshi la usalama barabarani kwa nini hamkamati hayo magari iwe asubuhi au jioni? Mbona baadhi ya mikoa daladala likisimamisha abiria hata mmoja mnawapiga faini? Leo hii wamemiliki wa mabasi ya shule wanaweka tinted ili isiwe rahisi kuona idadi ya walioko ndani. Ingefaa hayo mabasi yawe yanakaguliwa kwa mustakabali wa afya zao pamoja na maisha yao. Askari wa barabarani msikazanie bodaboda au magari ya watu binafsi ambapo inakuta kuna mtu mmoja au wawili. Angalieni hawa makumi na mamia
 
Kuna kipi cha kujifunza kutokana na ajali ya basi la watoto wa shule? Kwa idadi iliyotajwa hadi muda huu ilitakiwa wawe kwenye basi kubwa. Je hao watoto walikaaje ndani ya hilo basi? Je,polisi wa barabarani kutokea ffv/ mromboo arusha hadi karatu zaidi ya km 120 walikuwa wapi?
 
Back
Top Bottom