Hatua gani za kufuata kama mtu unataka kununua kiwanja ama nyumba

kinundu

JF-Expert Member
Oct 12, 2016
2,029
2,129
Habari zenu ndugu zangu, ninatamani kujua hatua mbali mbali za kuzifuata ili uuziwe kiwanja ama nyumba kiuhalali bila ya kutapeliwa...

Tunajua ni nyumba nyingi na viwanja vingi hapa Tanzania havijapimwa na havina hato miliki vile vile watu wana nunua hivyo hivyo na mwishoe utasikia jamaa katapeliwa..

Unaweza kuta hicho kiwanja labda muhusika alitumia kukupea pesa bank, ama kiwanja kina mgogoro wa kifamilia ama kiwanja kipo eneo ambalo hapo baadae inatakiww kupitishwe barabara si mnajua tena maswala ya mipango miji..

NAOMBA KUJUA HATUA GANI ZIFUATWE ILI NIWEZE KUPATA NYUMBA AMA KIWANJA KISICHO NA KASORO YOYOTE..

Kuna mtu alinunua nyumba ya familia flani na kwenda kuandikishana na kuilipia mahakamani... Lakini hadi sasa mnunuzi hana mamlaka kwenye ile NYUMBA coz ya mgogoro kesi imefunguliwa mahakamani mke mdogo wa marehemu mwenye nyumba ambaye alikua anaishi hapo kakata rufaa..

NAOMBENI HATUA HIZO WAKUU HIYO STORY HAPO JUU KAMA MTAPENDA NITAWAPA KALIPIA KILA KITU ILA HANA MAMLAKA NA HIYO NYUMBA NA KIWANJA..
 
Naamu ngoja waje walio tafuta viwanja na mashamba kwa jasho na wala sio wale wakurithi.
 
Inatokea Kama bahati tu kupata eneo/nyumba ambavyo havina mgogoro ktk nchi yetu, na hiyo haijalishi umepita mahakamani kwa wanasheria au wapi na hi ni kutokana na usiri uliogubikwa ktk suala zima la manunuzi eidha ya muuza au mnunuzi.
Kuna mambo hayako sawa, Mosi unauziwa eneo la wazi na mtu bnafsi m/kiti wa mtaa anatia saini na anapokea %. hapohapo jirani anapatikana nae anasaini, na kwa vile m/kiti na jirani wapo basi na mwanasheria bila kujilidhisha nae anamwaga wino.... Malizia mwenyewe nini kitatokea mbeleni .....
 
Swali zuri mkuu kuna jamaa yetu wa humu jf aliuziwa msikiti huko Bunju.
 
Inatokea Kama bahati tu kupata eneo/nyumba ambavyo havina mgogoro ktk nchi yetu, na hiyo haijalishi umepita mahakamani kwa wanasheria au wapi na hi ni kutokana na usiri uliogubikwa ktk suala zima la manunuzi eidha ya muuza au mnunuzi.
Kuna mambo hayako sawa, Mosi unauziwa eneo la wazi na mtu bnafsi m/kiti wa mtaa anatia saini na anapokea %. hapohapo jirani anapatikana nae anasaini, na kwa vile m/kiti na jirani wapo basi na mwanasheria bila kujilidhisha nae anamwaga wino.... Malizia mwenyewe nini kitatokea mbeleni .....
Hivi unaweza jiteteaje?
 
Back
Top Bottom