SautiYaMnyonge
JF-Expert Member
- May 13, 2018
- 439
- 742
Kwa siku za hivi karibuni kumeibuka kundi la vijana wadogo maarufu kama Panya Road wakijihusisha na uhalifu wa kuvunja nyumba za watu na kuiba vitu vya ndani kama radio, tv, pesa na vinginevyo. Aidha limekuwa likiwadhuru na kuwajeruhi watu kwa vitu vyenye ncha kali. Wakike kwa wakiume wamekumbana na kadhia hii.
Kundi limezua hofu na mashaka makubwa kwa raia wema hususani wanaorejea majumbani nyakati za usiku wakitoka makazini mwao pamoja na wale wanaokwenda makazini nyakati za mchana huku nyumba zikiwa hazina uzio wala walinzi.
Dar es Salaam kama mji wa kibiashara ni lazima suala la uhakika wa ulinzi na usalama likawa kipaumbele cha kwanza. Hili linawezekana kwa sisi raia au jamii kutoa ushirikiano wa kutosha kwa vyombo vya dola hususani jeshi la polisi kupitia kwa viongozi wa mitaa katika maeneo yetu, wajumbe/mabalozi na vikundi vya ulinzi shirikishi.
Ukitazama wahusika katika kundi hili la Panya Road ni vijana/watoto jambo linalotoa ujumbe mpana kuwa wazazi/walezi/viongozi wa dini/jamii hatukutimiza wajibu wetu wa malezi kwao kikamilifu. Vile vile ni kiashiria kuwa serikali inapaswa kujenga mazingira rafiki na wezeshi kwa makundi mbalimbali katika jamii yaweze kujitafutia kipato kwa njia halali kwa maana ya kurahisisha mazingira ya ufanyaji shughuli za kiuchumi.
Swali ni kuwa kundi hili lipo na linaendelea kufanya uhalifu kwenye jamii toka eneo moja kwenda jingine. Ikiashiria kusambaa kwake, Je jamii na jeshi la polisi tunashindwa kulidhibiti na kurejesha hali kuwa shwari?? Unashauri nini mwana jukwaa kama njia ya kusaidia mawazo ya kukabiliana na kundi hili baya kwa mustakabali wa usalama hapa Dar es Salaam!
Karibu sana.
#DarUsalamaKwanza #PanyaRoadSasaBasi