Hatua gani nichukue endapo Hakimu au Jaji hatendi haki kwa kuchelewesha shauri Mahakamani?

Peasant educator

JF-Expert Member
Mar 13, 2020
209
187
Salam wadau,

Nataka kufahamu hatua za kuchukua ukiona hakimu hatendi haki au anachelewesha hukumu kwa makusudi (kutoa ruling ya shauri mahakamani). Kuna hatua zozote za kufata au kureport au ndo hakimu (judge) analindwa na katiba hata kama anafanya kazi kinyume na maadili ya kazi yake either kwa kula rushwa au/na kushinikizwa na kiongozi wa Serekali?

Naomba mchango wenu, nawasilisha.
 
Hakimu na Jaji ni watu wawili tofauti sasa basi; Kama ni hakimu wa mahakama ya mwanzo peleka lalamiko mahakama ya wilaya iliyopo hiyo mahakama ya mwanzo, kama ni Hakimu wa mahakama wa wilaya peleka lalamiko kwa jaji mfawidhi wa mahakama kuu iliyopo hiyo wilaya, kama ni jaji peleka lalamiko kwa jaji mfawidhi wa hiyo mahakama kuu katika mahakama hiyo hiyo ambayo kesi yako ipo.
 
Pole mtoa hoja kwa hali ya sasa kisheria kwa nchi yetu tutaishi na mfumo huu hadi ile generation shujaa itakapo kuja kubadilisha hali hii na hii issue ingekua rahisi mno kama nchi ingekuwa na taasisi imara na zenye kujitegemea maana ungekua na uwezo wa kumkataa judge kusikiliza kesi yako(labda judge ana personal interest kuhusu case yako na hili litasababisha asiamue kwa haki)au ungeweza kumripoti kwenye bodi husika na kama utaishi na kushuhudia judge's wakiomba nafasi hizi(sio kuteuliwa na no 1)kutakuwa na unafuu mkubwa mno.
 
Hakimu au jaji unaweza kumkataa kama una sababu za msingi. Na hakuna hakimu au jaji anatang'ang'ania kesi kama utakua na sababu za msingi za kumkataa.
 
Nadharia ipo hivyo, na ndicho huyu bwana anachotakiwa kukifanya, kumtaka hakimu/jaji ajitoe, ila kivitendo haipo hivyo, nyakati hizi wanakataa kujitoa hasa kwa kesi za serikali, mfano hoja ni upendeleo katika maamuzi nk wanasema kama hujaridhika una nafasi za kukata rufaa na sio kumtaka yeye ajitoe. Kwa nyakati hizi mahakama imepoteza sana imani kwa wanaoitumia.
 
Hakimu na Jaji ni watu wawili tofauti sasa basi; Kama ni hakimu wa mahakama ya mwanzo peleka lalamiko mahakama ya wilaya iliyopo hiyo mahakama ya mwanzo, kama ni Hakimu wa mahakama wa wilaya peleka lalamiko kwa jaji mfawidhi wa mahakama kuu iliyopo hiyo wilaya, kama ni jaji peleka lalamiko kwa jaji mfawidhi wa hiyo mahakama kuu katika mahakama hiyo hiyo ambayo kesi yako ipo.
Judge kwa kiswahili sijui...
 
Umeona neno "sababu za msingi" au umeamua tu kujibu. Sababu za msingi zako ukizitoa zitapimwa. Mahakama sio kijiweni utake hakimu au jaji ajitoe eti unasema nimesikia au nimehisi. Au useme simpendi tu nataka ajitoe. Lazima utoe sababu za msingi na uwe na uthibitisho wa hiko unachokisema.

Hakimu au Jaji hatakiwi kujitoa kwasababu tu upande mwingine umemtaka kufanya hivyo bila kuwa na sababu za msingi na zenye uthibitisho
 
Kwa mfano sababu za huyu bwana anazozitoa kwamba ameona hakimu/Jaji hatendi haki, ameonaje au amelala akaota? Lazima awe na uthibitisho kwenye hilo analoona inabidi upande wa anaempelekea lalamiko nae aone.

Anaposema hukumu au uamuzi unachelewesha bila sababu za msingi. Ni sababu gani ambazo sio za msingi. Inabidi aziseme na upande anaempelekea lalamiko aone sio za msingi kwa maana mahakamani hakuna kesi yake tu kuna mamia wanasubiri kuhudumiwa.

Anaposema kuwa amekula rushwa, je anauthibitisho upi? Ametoa taarifa TAKUKURU? Au alioteshwa rushwa imeliwa.

Kwahiyo sababu zake ziwe za msingi na ziwe na uthibitisho. Ingekua watu wanawakataa mahakimu na majaji bila sababu zenye mashiko kesi zisingeisha huko mahakamani kila mmoja akiamka asubuhi anaenda kumkataa hakimu au jaji.
 
Umeona neno "sababu za msingi" au umeamua tu kujibu. Sababu za msingi zako ukizitoa zitapimwa. Mahakama sio kijiweni utake hakimu au jaji ajitoe eti unasema nimesikia au nimehisi. Au useme simpendi tu nataka ajitoe. Lazima utoe sababu za msingi na uwe na uthibitisho wa hiko unachokisema. Hakimu au Jaji hatakiwi kujitoa kwasababu tu upande mwingine umemtaka kufanya hivyo bila kuwa na sababu za msingi na zenye uthibitisho
Nafikiri umenielewa vibaya mpaka kufikiri kuwa nimeamua tu kujibu. Nasema umenielewa vibaya kwa kuwa nilichojibu ni kuunga mkono hoja yako ila nikaongeza na uhalisia wa vitendo kwa nyakati hizi.

Busara ni kuwa hakimu au jaji akituhumiwa upendeleo, hata kama hakuna uthibitisho wa huo upendeleo ni vyema ajitoe, lakini uhalisia ndio hawajitoi wakiwa wanakomaa kutaka uthibitisho wa sababu hizo kama wewe unavyoelekeza.
 
Sawa ndugu katika haki
 
Vijana wanasema sheria ziwe kwa Kiswahili!!!
Mwalimu aliposema kiingereza ni kiswahili cha dunia maana yake ni kuwaaambia watanzania kuwa tunahitaji kiingereza kuchangamana na dunia kama tunavyohitaji kiswahili kuchangamana na waswahili wenzetu.

Ikiwa elimumsingi ni hadi kidato cha nne nani ananyimwa haki kwa kgezo cha lugha
 
Hakimu na Jaji ni watu wawili tofauti sasa basi; Kama ni hakimu wa mahakama ya mwanzo peleka lalamiko mahakama ya wilaya iliyopo hiyo mahakama ya mwanzo, kama ni Hakimu wa mahakama wa wilaya peleka lalamiko kwa jaji mfawidhi wa mahakama kuu iliyopo hiyo wilaya, kama ni jaji peleka lalamiko kwa jaji mfawidhi wa hiyo mahakama kuu katika mahakama hiyo hiyo ambayo kesi yako ipo.
Mku kama ni CMA nipeleke wapiti?
Asante siku njema
 
Ila hakikisha una hela,kwa mifumo yetu ya Sheria ilivyooza,ukishindana na Hawa watu,utaumia,Tena Kama unaishi Kijijini!,ni balaa,Hakimu,mwendesha mashitaka,Mkuu wa kituo,wote Wanakula pamoja,wakiamua kukufiksi,utaumia,unaweza ukakimbia na kuhama Kijiji/mkoa
 
Umeona neno "sababu za msingi" au umeamua tu kujibu. Sababu za msingi zako ukizitoa zitapimwa. Mahakama sio kijiweni utake hakimu au jaji ajitoe eti unasema nimesikia au nimehisi. Au useme simpendi tu nataka ajitoe. Lazima utoe sababu za msingi na uwe na uthibitisho wa hiko unachokisema.

Hakimu au Jaji hatakiwi kujitoa kwasababu tu upande mwingine umemtaka kufanya hivyo bila kuwa na sababu za msingi na zenye uthibitisho
Kwa jaji anayejielewa, kile kitendo cha kutuhumiwa tu ni sababu tosha ya kujitoa kwenye kesi hata kama sababu hazijashiba vizuri. Hii ndio sababu inaelezwa kuwa, haki inapaswa ionekane ikiwa inatolewa.
 
Ila hakikisha una hela,kwa mifumo yetu ya Sheria ilivyooza,ukishindana na Hawa watu,utaumia,Tena Kama unaishi Kijijini!,ni balaa,Hakimu,mwendesha mashitaka,Mkuu wa kituo,wote Wanakula pamoja,wakiamua kukufiksi,utaumia,unaweza ukakimbia na kuhama Kijiji/mkoa
Ilo ni matatizo Tanzania, bado kuna upungufu kwenye hizi taasisi
 
Back
Top Bottom