Khlala
Senior Member
- Dec 21, 2012
- 170
- 118
Wasalaam
Naombeni msaada wa kisheria kwa namna gani naweza kumchukulia hatua cameran ambaye amepatiwa kazi ya kupiga picha na video kwenye tukio la harusi/sendoff lakini akakiuka maadili kwa kusambaza mitandaoni baadhi ya matukio yaliojiri ambayo hayakuwa ya kawaida (unintentional scenario) bila ridhaa ya mhusika hali inayosababisha msononeko wa mawazo kwa familia ya mtendwa.
Iko hivi, siku ya tarehe 2/12/2021 kulikuwa na tukio la send off kumuaga dada yetu. Sasa wakati wa kumkabidhi alichaguliwa kaka yetu kwa ajili ya kufanya tukio hilo la kumkabidhi binti kwa waoaji. Kutokana na tukio la hivi karibuni la kufiwa na shangazi yetu na pia mama yake na kijana anayeoa amefariki na kuzikwa jumapili ya wiki iliyopita (28/11/2021) hivyo bado hali ya huzuni ilikuwepo hali ambayo inaweza ikawa ilichangia mnenaji kujitambulisha kama kaka wa marehemu badala ya kaka wa bibi harusi.
Baada ya tukio lile hali iliwekwa sawa kwa kulitolea ufafanuzi na hadhira yote ilielewa kilichotokea na ikapita.
Lakini katika hali ya kusikitisha mpiga picha alienda studio na kutengeneza clip ambayo imesambaa dunia nzima hali ambayo imeleta taharuki hasa kwa familia na bibi harusi ambaye ndo tu ametoka kufunga ndoa yake.
Sasa basi mimi kama mmoja wa wanafamilia ambao tumeguswa na hili tunaomba mchango wa mawazo hasa ni kwa namna gani tunaweza kumshughulikia mtu huyu ambaye ametengeneza clip na kuisambaza bila ridhaa ya wahusika.
Mwenyewe amekiri kufanya hivyo na pia clip ina nembo/jina la biashara ya wapiga picha.
Naomba kuwasilisha