Hatua ambazo Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imezichukua hadi sasa katika kukabiliana na ugonjwa wa Corona ni kama ifuatavyo:-

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,806
11,968
1. Serikali imezifunga skuli zote za maandalizi, msingi, sekondari, vyuo Vikuu pamoja na madrasa

2. Ndege za kutoka Italia na sehemu nyengine zenye maambukizi ya Corona zimezuiwa

3. Serikali imezuia mikusanyiko inayokutanisha watu wengi kwa wakati mmoja ikiwemo mikutano, makongamano, semina, warsha, michezo ya ligi kuu, ligi za kanda pamoja na burudani za ngoma na shughuli za harusi

4. Serikali iliwataka watu wote wanaoingia nchini kutoka nchi zilizoathirika na maradhi hayo kufuata utaratibu wa kujitenga kwa hiari kwa muda wa siku 14

5. Serikali inakataza na inakemea vikali utumiaji wa bandari zisizo rasmi kwa ajili ya kuchukua abiria na mizigo.

6. Masoko yote kutoa huduma kuanzia asubuhi hadi saa 12 jioni.

7. Serikali inalaani vikali vitendo vya wafanyabiashara kutumia ugonjwa huu kwa faida zao kwa kupandisha bei za vifaa vya kinga, bidhaa na huduma nyengine

8. Kufungwa kwa baa zote na maeneo mengine yote ya starehe

9. Serikali inazuia safari zote za nje ya nchi kwa watendaji wake na iliwashauri wananchi kwa wakati huu kuepuka safari zisizo za lazima za nje ya Zanzibar

10.Serikali inawataka wananchi wote kuacha kusikiliza taarifa zisizo rasmi na badala yake wasikilize taarifa rasmi zitakazotolewa na Serikali.

11.Serikali inashauri wananchi wanaokwenda masokoni na maeneo mengine ya kutafuta huduma kuepuka mikusanyiko na baada ya kupata huduma warudi majumbani.

12.Serikali inawataka wananchi kupunguza msongamano katika hospitali zetu badala yake watu wasiozidi wawili wataruhusiwa kumuona mgonjwa kwa siku na inashauriwa wananchi watumie vituo vya afya vilivyokuwa karibu nao ili kuepuka msongamano katika hospitali kuu.
 
Back
Top Bottom