Hatua 26 za Kufuata Katika Kuanzisha Biashara Ndogondogo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hatua 26 za Kufuata Katika Kuanzisha Biashara Ndogondogo

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Jpinduzi, Nov 12, 2011.

 1. Jpinduzi

  Jpinduzi Senior Member

  #1
  Nov 12, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 136
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  1. Hatua ya kuamua kuingia katika biashara
  Kuamua kuingia katika biashara ni majumuisho ya utayari wa kisaikolojia, kiakili, kiuchumi na kukabiliana na hatari au vitisho vyote vitakavyojitokeza kwenye biashara
  1. Hatua ya kuchanganua uwezo na udhaifu wako
  Maeneo manne ni muhimu yapatiwe taarifa halisi na kuchukua hatua ili uweze kumudu kufanya biashara husika
  [TABLE]
  [TR]
  [TD][/TD]
  [TD="width: 197, bgcolor: #EEEEEE"]Mazingira wezeshi[/TD]
  [TD="width: 197, bgcolor: #EEEEEE"]Mazingira pingamizi[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 197, bgcolor: #EEEEEE"]Mazingira ya Ndani[/TD]
  [TD="width: 197, bgcolor: #EEEEEE"]
  UwezoUwezo wako katika kuendesha biashara mfano: utaalam, vitendea kazi, kiwanja nk.
  [/TD]
  [TD="width: 197, bgcolor: #EEEEEE"]
  UdhaifuUdhaifu wako katika kuendesha biashara mfano: ukosefu wa utaalam, vitendea kazi, kiwanja nk.
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 197, bgcolor: #EEEEEE"]Mazingira ya Nje[/TD]
  [TD="width: 197, bgcolor: #EEEEEE"]
  FursaKuwepo kwa sera nzuri, katiba nzuri, hali ya hewa nzuri, mwitikio wa jamii nk
  [/TD]
  [TD="width: 197, bgcolor: #EEEEEE"]
  VitishoKutokuwepo kwa sera nzuri, katiba nzuri, hali ya hewa nzuri, mwitikio mbaya wa jamii nk
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  1. Hatua ya kupata mafunzo
  Baada ya kujua udhaifu wako, pata mafunzo
  Mfano:- Ya kupata ufundi au kubadili mitizamo
  Kupata utaalam wa kiufundi katika biashara husika
  1. Hatua ya kupeleleza mazingira utakayofanya biasha ili kujua:
  i) Fursa nzuri zilizopo
  ii) Vitisho au hatari zitakazoikabili biashara yako (vihatarishi vya biashara husika kama vile sera mbovu, barabara mbovu, hali ya hewa mbovu nk)
  1. Hatua ya kuchagua biashara gani ufanye
  i) Kutengeneza bidhaa (Manufacturing)
  ii) Kuuza bidhaa (Trading)
  iii) Kutoa huduma (Service)
  Kutengeneza bidhaa (Manufacturing)
  Kutengeneza bidhaa ni kutumia rasilimali watu na malighafi ili kutengeneza bidhaa ya kuuza kwa mlaji au mchuuzi. Bidhaa ni kama vyakula, vyombo, nk
  Kuuza bidhaa (Trading)
  Kuchuuza bidhaa zilizotengenezwa hapo juu no. A(a)
  Kutoa huduma (Service)
  Kutumia ujuzi wako au wa wengine katika kuwahudumia watu na shida zao kwa malipo. Mfano kufundisha, kutibu, kusafirisha, kutumbuiza nk
  1. Hatua ya utafiti wa soko (Market Survey)
  i) Ukubwa wa soko
  ii) Mgawanyo wa soko
  iii) Aina ya soko/masoko
  iv) NK
  1. Kuamua aina ya mfumo wa biashara utakayofanya
  Fuatilia maelezo ya kila mfumo ukitilia maanani faida na hasara za kila mfumo. Unaweza pia kumtumia mshauri wa masuala ya biashara kukushauri kulingana na mazingira yako utakayofanyia biashara.
  i) Mtu mmoja (sole proprietor)
  Faida yake
  Kuanzisha ni rahisi
  Maamuzi hupitishwa kwa haraka kwa hiyo hakuna urasimu
  Hasara yake
  Biashara ikipata shida mmiliki anahusika na hasara kama vile ya ufilisi nk

  ii) Ushirika (>watu wawili) (partnership)
  Faida yake
  Kuanzisha ni rahisi
  Maamuzi hupitishwa kwa haraka kwa hiyo hakuna urasimu
  Hasara yake
  Biashara ikipata shida wamiliki wanahusika na hasara kama vile ya ufilisi nk
  Mikataba inayoingiwa na mmoja wa washirika huwabana na wengine wasiohusika
  iii) Kampuni ya umma au mashirika ya umma (public companies)(zaidi ya watu wawili bila kikomo)
  Faida yake
  Utambulisho wa kisheria
  Ukomo wa ufilisi upo kwenye kampuni husika na sio wenye hisa
  Ni rahisi kuvutia mitaji mikubwa kupitia masoko ya hisa
  Hasara yake
  Haina usiri hivyo ni hatari kwani washindani wa biashara husika wanaweza kutumia taarifa hizo kujipanga
  Muda na rasilimali muda kupotea kwa shughuli za kihasibu na kazi za makaratasi
  iv) Kampuni ya binafsi yenye ukomo wa hisa (private companies limited by shares) (watu wawili hadi 50)
  Faida yake
  Utambulisho wa kisheria
  Ukomo wa ufilisi upo kwenye kampuni husika na sio wenye hisa
  Kazi za makaratasi ni chache ukilinganisha na makampuni ya umma
  Mlolongo wa taratibu za kisheria ni chache ukilinganisha na makampuni ya umma
  Hasara yake
  Gharama katika kuanzisha tofauti na biashara binafsi
  Huruhusiwi kuuza hisa katika masoko ya hisa
  Kampuni li lazima angalau iwe na wakurugenzi, katibu na mhasibu
  Ni lazima ifanyiwe ukaguzi wa mahesabu kila mwaka

  v) Kampuni ya binafsi yenye ukomo wa udhamini (private companies limited by guarantees) (watu wawili hadi 50)
  Faida yake
  Utambulisho wa kisheria
  Ukomo wa ufilisi upo kwenye kampuni husika na sio wenye hisa
  Kazi za makaratasi ni chache ukilinganisha na makampuni ya umma
  Mlolongo wa taratibu za kisheria ni chache ukilinganisha na makampuni ya umma
  Hasara yake
  Gharama katika kuanzisha tofauti na biashara binafsi
  Huruhusiwi kuuza hisa katika masoko ya hisa
  Kampuni li lazima angalau iwe na wakurugenzi, katibu na mhasibu
  Ni lazima ifanyiwe ukaguzi wa mahesabu kila mwaka
  vi) Jumuiya (association)
  Faida yake
  Utambulisho wa kisheria
  Inavutia wahisani
  Ni ya watu wachache waliokubaliana
  Hasara yake
  Ukiritimba katika kupitisha maamuzi
  Ugomvi wa mara kwa mara
  Haina kinga kwa waazilishi
  vii) Vyama vya ushirika
  Faida yake
  Utambulisho wa kisheria
  Inavutia wahisani
  Ni ya watu wachache waliokubaliana
  Hasara yake
  Ukiritimba katika kupitisha maamuzi
  Ugomvi wa mara kwa mara
  Haina kinga kwa waazilishi
  viii) Mashirika yasiyo ya kiserikali
  Faida yake
  Utambulisho wa kisheria
  Inavutia wahisani
  Ni ya watu wachache waliokubaliana
  Hasara yake
  Ukiritimba katika kupitisha maamuzi
  Ugomvi wa mara kwa mara
  Haina kinga kwa waazilishi
  • Ukishachagua mfumo mzuri wa biashara yako, unatakiwa kuanza mchakato wa kuisajili katika mamlaka ya usajili wa makampuni inayoitwa BRELA ambayo ofisi zake zipo Jengo la shirika –Dar es salaam
  1. Hatua ya kuchagua sehemu ya biashara
  i) Kama ni sheli itabidi iwekwe kando ya barabara yenye magari mengi
  1. Hatua ya kuchagua technolojia
  i) Teknolojia itasaidia kujua
  a) Aina ya watumishi
  b) Aina ya vitendea kazi mashine /mitambo
  Mfano kilimo cha maksai na kukamua kwa mashine
  ii) Teknolojia nzuri ni lazima iwe na sifa zifuatazo
  a) Ni rahisi kutumiwa
  b) Iwe rahisi kupata msaada kama mafundi nk
  c) Iwe inaendana na tamaduni husika
  d) Iwe ni rafiki wa watu na mazingira
  e) Iwe na gharama ndogo za uendeshaji
  f) Inaendelezeka
  1. Hatua ya kununua mashine na vifaa
  Mashine na mitambo mingine itategemea sana uchaguzi wa teknolojia hapo juu 8(i)
  Mashine zote na mitambo ni lazima kuzingatia yaliyotajwa hapo juu 8(ii)
  1. Hatua ya usajili wa biashara
  i) Hii hufanywa mara nyingi kwenye manispaa husika. Leseni kwa wafanya biashara ndogondogo ni bure (biashara ndogondogo ni ile ambayo mauzo yake hayazidi Shs 20 milioni kwa mwaka)

  1. Hatua ya kuandika Mchanganuo wa Biashara (Business Plan)
  • Baada ya kufanya hayo yote sasa ni wakati mzuri wa kuandika mchanganuo wa biashara yako
  • Mchanganuo wa biashara ni maelezo ya kina ambayo inaonyesha biashara yako ilikotoka, inakokwenda, hali ya masoko, sekta, kifedha na uongozi wa biahara yako. Ni taarifa muhimu ya kuwavutia wawekezaji na watoa mikopo kama mabenki
  Mambo muhimu ya kujua katika kuandika Mchanganuo wa Biashara
  1. Muhtasari wa biashara yako
  2. Historia na maelezo ya biashara yako
  3. Maelezo ya bidhaa au huduma ya biashara yako
  4. Mchanganuo wa masoko
   1. Ukubwa wa soko
   2. Mgawanyo wa soko
   3. Aina ya soko/masoko
   4. Mchanganuo wa ushindani
    1. Watoa huduma au wauza bidhaa kama yako
    2. Udhaifu wao
    3. Uwezo wao
    4. Mkakati wa utekelezaji
     1. Uongozi na usimamizi wa kazi
     2. Uchambuzi wa madhaifu, nguvu, fursa na hatari zinazokabili biashara yako
     3. Mkakati wa Uzalishaji
     4. Mkakati wa kuuza
  1. Mpango wa fedha
   1. Uchambuzi wa mahitaji ya mtaji
   2. Wapi utatoa mtaji
   3. Matumizi ya mtaji
   4. Makisio ya Mauzo
   5. Uchambuzi wa kurudisha gharama (break even analysis)
   6. Makisio ya faida au hasara
   7. Makisio ya mzunguko wa fedha katika biashara yako (cashflow)
   8. Makisio ya oanisho la mali na madeni ya biashara yako (balance sheet)
   9. Ulinganifu wa sehemu mbalimbali za biashara (business ratios)
   10. Viambatanisho
    i. Lesseni
    ii. Cheti cha ulipaji kodi
    iii. Cheti cha usajili
    iv. Taarifa mbalimbali za biashara yako ambazo hazikupata nafasi ndani ya mchanganuo huu
    v. nk
  1. Hatua ya kupanga juu ya pesa.
  Kutafuta mikopo kwa kufuata utaratibu wa taasisi za fedha husika
  Taasisi nyingi huhitaji yafuatayo
  1. Dhamana ya mkopo
  2. Uzoefu wa biashara husika
  3. Mchanganuo wa biashara
  4. Maombi ya mkopo
  1. Hatua ya ufahamu wa kiufundi.
  Hii ifanywe ili mwenye biashara apate ufahamu wa kiufundi juu ya biashara yake hasa kutoka kwa taasisi husika au mshauri wa biashara (consultant).
  1. Hatua ya kujua vyanzo vya nishati:
  Kama ni umeme hakikisha iko sawa na umeme utakidhi matakwa ya biashara.
  Kama ni mafuta uhakikishe mafuta inapatikana na bei haitaadhiri bei ya bidhaa
  1. Hatua ya kuweka vifaa: (Machines installation)
  Wataalam husika wafanye hii kazi
  1. Hatua ya kuajiri wafanyakazi.
  Wafanyakazi wako wengi mtaani, lakini kumpata mtu atakayekidhi matakwa ya biashara yako kwa maana ya ubora na kufikia lengo la uzalishaji inahitaji usambazaji wa taarifa kwa upana zaidi na kwa maeneo maalum ambayo unategemea wafanyakazi watoke. Mfano vyuoni, makanisani nk
  Unashauriwa pia kutumia marafiki na ndugu wa karibu ili upate mfanyakazi ambaye ni bora zaidi
  1. Hatua ya kujua upatikanaji wa malighafi
  Malighafi bila ubishi ni kiungo muhimu kwa biashara yeyote inayohusisha bidhaa. Vyanzo vya kupata malighafi ni muhimu ijulikane na iwe ya uhakika.
  1. Hatua ya uzalishaji mali
  i) Uzalishaji wa majaribio , Kuuza kwa majaribio kutoa huduma kwa majaribio muda – miezi 2-6, nk
  ii) Kuanza biashara rasmi
  1. Hatua ya kuhakikisha bidhaa yako hainakiliki
  i) Kutunza siri ya unavyozalisha au kutoa huduma tofauti na wengine
  ii) Tunza vizuri siri zingine za biashara yako
  1. Usalama wa biashara yako
  i) Epuka majengo ambayo ni rahisi kuwaka moto, kubomolewa na wezi, wizi katika pesa za mauzo, utapeli wa bidhaa katika kununua na kuuza nk.
  1. Hatua ya kuuza (Selling)
  - Kufikia wateja (fikiria utamfikiaje mteja wako wa kwanza – maelezo zaidi yatakuwepo katika mchanganuo wa biashara)
  - Kusambasa huduma/bidhaa
  - Kuweka bei
  - Kutangazia biashara
  - Promosheni nk.
  1. Hatua ya Utafiti wa soko (Market Research)
  - Hii ifanywe kila mara ili kujua kama wateja wamebadilika au bado Ili kujua kama wanapenda huduma/bidhaa zako au la.
  - Kujua biashara yako imekamata asilimia gani katika soko
  - Kupata maoni ya wateja ili kuboresha biashara/huduma/bidhaa
  Namna ya kufanya utafiti
  i) Utafiti wa kuendelea
  Kila mteja anaponunua bidhaa, ajaze fomu maalum ya maoni. Mfano ya jinsi alivyohudumiwa, bei ya bidhaa, usindikaji, ubora nk
  ii) Utafiti maalum
  Huu ufanywe wakati wa kutoa vivutiuo maalum au promosheni maalum.
  Mteja wa promosheni ajaze fomu maalum ya maoni. Mfano ya jinsi alivyohudumiwa, bei ya bidhaa, usindikaji, ubora nk
  1. Hatua ya kusimamia na kuthibiti biashara:
  Hii ni kuhakikisha kuwa biashara inakwenda kama ilivyobuniwa /pangwa.
  1. Hatua ya kutathmini biashara.
  Hii ni kujua kama biashara imekwenda kama ilivyobuniwa /pangwa.
  Mambo ya kuangalia
  1. Mapato na matumizi
  2. Bajeti iliyiopita
  3. Matokeo ya utaifit/wa soko
  1. Hatua ya kufanya maboresho/mabadiliko
  Unaweza kumuajiri au kumtumia mtaalam wa sekta hiyo kufanya taadhmini ya biashara yako.
  Fanya sawa sawa na matokeo ya tathmini/utafiti
   
 2. BIG X

  BIG X JF-Expert Member

  #2
  Nov 12, 2011
  Joined: Nov 4, 2011
  Messages: 777
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Asante mjomba.
   
 3. CONSULT

  CONSULT JF-Expert Member

  #3
  Nov 12, 2011
  Joined: May 8, 2011
  Messages: 223
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 45
  Hongra sana kwa ujuzi/uchambuzi wako lakini mashaka yangu kwa taratibu hiyo hutapata biashara ya kufanya ''TOO MUCH ANALYSIS IS PARALYSIS '' ''Ukimchunguza kuku Hutamula''
   
 4. king'amuzi

  king'amuzi JF-Expert Member

  #4
  Nov 12, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 613
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  thanx mkuu
   
 5. M

  Mrdash1 JF-Expert Member

  #5
  Nov 13, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 1,379
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Ahaa haaa si bora na wewe ungetoa tathmini yako au at least ukosoe objectively pale ambapo umeona mtu mzima amekosea
   
 6. HAZOLE

  HAZOLE JF-Expert Member

  #6
  Nov 13, 2011
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 1,333
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  safi.
  good theory. mdogo mdogo tutafika tu
   
 7. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #7
  Nov 13, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,154
  Likes Received: 2,406
  Trophy Points: 280
  safi mkuu kwa info
   
 8. Chiwa

  Chiwa JF-Expert Member

  #8
  Dec 28, 2011
  Joined: Apr 17, 2008
  Messages: 1,388
  Likes Received: 716
  Trophy Points: 280
  naomba idhini yako nifundishie wengine japo good job natumia ya kizungu inasumbua
   
 9. Mangandula

  Mangandula Senior Member

  #9
  Dec 29, 2011
  Joined: Nov 30, 2011
  Messages: 186
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Asante mkuu, ombi langu ni kuwa naomba barua ya mfano ya mchanganuo wa biashara niwekee ktk pm.
   
 10. Jpinduzi

  Jpinduzi Senior Member

  #10
  Jan 5, 2012
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 136
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  fundisha tu mkuu wala haina shida.gudluck!
   
 11. Jpinduzi

  Jpinduzi Senior Member

  #11
  Jan 6, 2012
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 136
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  uSIJALI MKUU NIMESHAKUWEKEA
   
 12. lembu

  lembu JF-Expert Member

  #12
  Nov 1, 2017
  Joined: Dec 31, 2009
  Messages: 576
  Likes Received: 491
  Trophy Points: 80
  Hello wana JF
  Kwa wanaotaka version iliyoboreshwa ya haya mafunzo na mafunzo mengine ya ujasiriamali na uongozi unaweza kufuata link hii hapa
  Hizi ni notes zangu nimeziandaa mwenyewe bila kuiga popite japo kuna watu wengi sana wamekopi hizi nondo na kuzifanya za kwao bila idhini yangu
  Asanten na karibuni
  Hatua 26 za Kufuata Katika Kuanzisha Biashara Ndogondogo
   
 13. Samcezar

  Samcezar JF-Expert Member

  #13
  Nov 1, 2017
  Joined: May 18, 2014
  Messages: 1,927
  Likes Received: 1,401
  Trophy Points: 280
  Nimependa msemo wako. Too much analysis is paralysis!
   
 14. mwampepe

  mwampepe JF-Expert Member

  #14
  Nov 2, 2017
  Joined: Sep 14, 2015
  Messages: 216
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 45
  Thanks
   
 15. lembu

  lembu JF-Expert Member

  #15
  Nov 2, 2017
  Joined: Dec 31, 2009
  Messages: 576
  Likes Received: 491
  Trophy Points: 80
  Huu msemo halisi unaandikwa hivi
  "TOO MUCH ANALYSIS LEAD TO PARALYSIS"
  Imenukuliwa VIBAYA
  Huu msemo unalenga hasa kwa mradi au biashara inayofanyiwa uchambuzi yakinifu mara nyingi bila utekelezaji

  Njia rahisi ya kukosoa mafundisho hapo juu, ni hivi, mtu achukue hatua moja halafu kwa ujasiri aseme hii hatua sio muhimu au haifai na atoe sababu.
   
Loading...