Hatma ya Wtanzania iko mikononi mwa Chadema na sio tena Ccm,ccm imesoma Peoples pewer | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hatma ya Wtanzania iko mikononi mwa Chadema na sio tena Ccm,ccm imesoma Peoples pewer

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by abdulahsaf, Feb 25, 2011.

 1. a

  abdulahsaf JF-Expert Member

  #1
  Feb 25, 2011
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  CHADEMA inatisha
  • Wafanya maandamano makubwa ya kihistoria jijini Mwanza

  na Sitta Tumma, Mwanza


  [​IMG]
  MAELFU ya wakazi wa jiji la Mwanza na viunga vyake, jana walilazimika kusimamisha shughuli zao na kujiunga katika maandamano makubwa na ya kihistoria, yaliyoongozwa na viongozi wa chama kikuu cha upinzani nchini CHADEMA, huku mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe, akitoa msimamo mkali kuwa chama chake sasa kimedhamiria kuwakomboa Watanzania kutoka katika hali ngumu ya maisha na mgawo wa umeme, ikiwa serikali ya Rais Jakaya Kikwete haitachukua hatua za dharura kulinusuru taifa.
  Maandamano hayo yaliyoongozwa na Mbowe na Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Willbrod Slaa, yalianzia katika shule ya Nyakato Buzuruga na kupita barabara za Pamba, Kenyatta, na Makongoro zilizo katikati ya jiji hili na kuhitimishwa katika viwanja vya Furahisha kulikofanyika mkutano mkubwa wa hadhara.
  Mbowe alipata wakati mgumu kutoa hotuba yake kutokana na maelfu ya watu kumkatisha mara kwa mara wakitaka Rais Jakaya Kikwete ajiuzulu pamoja na mawaziri wake wa Ulinzi, Dk. Hussein Mwinyi, na Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, kwa sababu ya kushindwa kusimamia majukumu yao vizuri.
  Alisema uzembe na ufisadi ndio uliolifikisha taifa katika mgawo wa umeme na hali ngumu ya maisha kwamba hivi sasa Watanzania wameingizwa kwenye ufisadi mpya kutokana na serikali kuamua kutenga sh bilioni 400 kwa ajili ya kukodi mitambo ya kuzalishia umeme.
  “Bilioni 400 zimepangwa na serikali ya Kikwete kwa ajili ya kukodi mitambo ya kuzalisha umeme na kila mwezi sh bilioni 23 zitalipwa...huu ni ufisadi mkubwa na mauaji kwa Watanzania,” alisema Mbowe.
  Akiwageukia polisi na maofisa wa usalama wa taifa walioamiminika uwanjani hapo, Mbowe aliwataka wakafikishe salamu kwa Rais Kikwete na CCM yake, kwamba CHADEMA sasa imedhamiria kulikomboa taifa kutoka kwenye makali ya maisha.
  Alionya kuwa kama Rais Kikwete hatachukua hatua za dharura kulinusuru taifa basi yaliyotokea katika nchi za Misri, Tunisia na Libya kwa wananchi wenyewe kuamka na kuing’oa serikali madarakani, yanaweza pia kutokea Tanzania.
  Wakati wakitoa msimamo huo, umati ulisikika ukisema “tufanye sasa hivi, tuko tayari kwenda Ikulu hata sasa hivi” lakini alisema wataendelea kuwasha moto wa mabadiliko nchi nzima na kwamba Rais Kikwete wataenda naye hatua kwa hatua kuangalia kama anachukua hatua za kunusuru nchi au la.
  “Rais Kikwete tunakwenda naye kwa stepu, tutawasha moto wa maandamano nchi nzima, tukimaliza tutaangalia kama atakuwa amechukua hatua. Tunampa siku tisa,” alisema Mbowe na kushangiliwa.
  Dk. Slaa aliyekuwa wa kwanza kuhutubia katika mkutano huo, alisisitiza sana msimamo wa chama hicho kumpa Rais Kikwete siku tisa za kuhakikisha anaondoa kodi kwenye maeneo yote yaliyosababisha bei za vyakula na bidhaa mbalimbali kupanda na kufanya maisha ya wananchi kuwa magumu.
  Katibu Mkuu huyo aliyekuwa pia mgombea urais kupitia uchaguzi mkuu uliopita hakusahau kuzungumza makovu ya uchaguzi huo ambapo alisisitiza kuwa kura zake zilichakachuliwa.
  “Tunajua walichakachua kura zangu, ila hatupotezi muda kwa sasa, twende kwenye kazi hadi kieleweke,” ambapo wananchi waliitikia tena wakisema “iwe kama Misri, Libya” na kusisitiza kuwa wako tayari kwa hilo muda wowote wakati huo.
  Aidha, katika hotuba yake hiyo iliyotumia takriban dakika 45 hivi jukwaani, Dk. Slaa alisisitiza kuwa Rais Kikwete aliwajua vizuri sana wamiliki wa kampuni ya Dowans tangu awali.
  Alisema kama Rais Kikwete, Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja na Rostam wanataka Dowans ilipwe basi watoe fedha zao mifukoni na sio kutumia fedha za umma kujilipa wenyewe kupitia kampuni ya Dowans.
  Aidha, Dk. Slaa aliwaambia wananchi waliofurika katika viwanja hivyo kuwa mmiliki wa Dowans ni Rostam Aziz kwani ndiye aliyehusika kubadili mkataba wa kampuni tata ya Richmond, kwa kuwatuma watu wawili Marekani kubadili mkataba huo ili uweze kumilikiwa na Dowans. Majina ya waliotajwa tunayahifadhi.
  “Rostam Aziz alifanya mawasiliano yote na serikali katika hatua za kubadilisha mkataba wa Richmond kuwa wa Dowans, sasa Kikwete atakataaje na atakwepaje kwamba haijui Dowans na mmiliki wake? Ina maana Rostam alifanya mawasiliano haya na serikali ya nani kama si ya Kikwete?”
  “Rostam alituma watu wawili ambao ni (….) kwenda Marekani kubadili mkataba wa Richmond kwenda Dowans...na ujanja huu umekuwa ukifanywa sana katika nchi na Kisiwa cha Costa Rica ambako huwa wanauza makampuni kwa mtu yeyote anayehitaji kumiliki kampuni! Tuliambiwa na kamati ya kina Mwakyembe kwamba kampuni ya Richmond inafanya kazi ya Stationary,” alisema Dk. Slaa.
  Wabunge wa CHADEMA nao waliwasha moto
  Mbunge wa Jimbo la Ubunge, John Mnyika, ambaye pia ni Waziri Kivuli wa Nishati na Madini alisema kupanda kwa gharama za bidhaa kumesababishwa na tatizo la mgawo wa umeme unaoendelea ambao kwa namna moja ama nyingine unawanufaisha wakubwa wachache ndani ya serikali.
  Aidha, Mnyika aliwakumbusha wananchi wakumbuke kauli za wakubwa akiwemo Rais Kikwete kuhusu ujio wa kampuni ya Dowans kwamba hawamfahamu mmiliki na hapahapo aliwataka viongozi hao sasa watoe maelezo baada ya kumwona.
  Mbunge wa Kawe, Halima Mdee alisema kuwa wakati wa CCM kutawala umefika mwisho na kuwataka kuwapisha ili waweze kufanya kazi.
  “Kama wananchi mtakubali mabadiliko yanawezekana …leo hii tuko Mwanza kwa ajili ya kuiondoa CCM madarakani pamoja na kudai kuwa kufanya kwetu maandamano kuna maana kuwa hatuna kazi,” alisema Mdee.
  Mbunge wa Nyamagana Ezekiel Wenje alisema kama mikoa ya Kanda ya Ziwa, ndiyo yenye rasilimali na utajili mkubwa kwa nini wananchi wake wapigike kimaisha, aliwataka wananchi hao kuanza mapambano ya kuhakikisha wanauaga umaskini.
  “Kama dhahabu, almasi, samaki na malighafi nyingine zinapatikana katika ukanda wetu na kuchukuliwa na watu wachache …kwa nini tusibadilike na kuwa na nguvu moja ya kukataa, sasa tuanze kazi ya kujikomboa,” alisema Wenje.
  Mbunge wa Ilemela, Highness Kiwia, aliwataka wananchi hao kutoa wasiwasi kuhusu hatma ya mgogoro wa ardhi ambao unaendelea na kuahidi kuwa Waziri wa Ardhi na Makazi, Anna Tibaijuka, atalitatua mwezi Mei mwaka huu.
  Alisema ingawa CCM mkoa wa Mwanza umemfungulia mashtaka kuwa alishinda kwa wizi wa kura, nguvu ile ile iliyompa ushindi wa kishindo, ndiyo itakayoleta maendeleo ndani ya miaka mitano.
  Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, alimtaka Rais Kikwete kuchukua tahadhari kutokana na mwenendo mzima wa mambo unavyoendeshwa ndani ya serikali yake.
  Akisisitiza kauli hiyo, Lema alisema kama jiji la Mwanza limeweza kufanya mkutano na maandamano ya amani, kwa nini katika jiji la Arusha, hali ya hewa ilichafuliwa na viongozi wake?
  Alisema, “JK akiona wenzake wananyolewa , yeye atie maji ..ndugu zangu, namaanisha kuwa JK anatakiwa kuwaangalia viongozi wenzake kule Misri, Tunisia na sasa Libya wanavyofanywa na nguvu ya umma.” Aidha, Lema aliendelea kusisitisa kauli yake aliyoitoa bungeni kuwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, alisema uongo kuhusu tukio la Januari 5 mwaka huu kule Arusha na kwamba ukweli upo. Huku akishangiliwa kwa kuongea kwa lugha ya kisanii, Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi, maarufu kama Mr. Sugu, alisema kama jimboni kwake, Manzese, Nyamagana na kwingineko wanalia njaa, kwa nini CCM isiondoke?
   

  Attached Files:

 2. luckyperc

  luckyperc JF-Expert Member

  #2
  Feb 25, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 496
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  hii ni mwanza tu......
  arusha mara ngapi ya haya....
  kilimanjaro jee.......
  Mbeya...........
  Dar vigeugeuu njaa.........
  tunasubiri ya shinyanga......

  HALAFU MKWERE KASHINDA KWA KURA MIL 6............!!!!!!!
   
 3. mchonga

  mchonga JF-Expert Member

  #3
  Feb 25, 2011
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,250
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  [​IMG]
   
 4. Mpevu

  Mpevu JF-Expert Member

  #4
  Feb 25, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 1,816
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Mkuu,
  Nimepapenda hapo kwenye BLUE
   
 5. nsimba

  nsimba JF-Expert Member

  #5
  Feb 25, 2011
  Joined: Oct 7, 2010
  Messages: 785
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  inatisha
   
 6. P

  Peter Kabelelo Member

  #6
  Feb 25, 2011
  Joined: Aug 9, 2009
  Messages: 26
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 5
  kwa hali hii ya maisha! Graduate anapata take home 332, 264.88tsh. Una mke na mtoto, ndugu nk. Nyama bei juu, mafuta ya chakula ndo balaa, sukari ndo kabisaa!! Hapo hujazungumzia umeme nk. Aibu mtu mzima unaanza kumkwepa mwenye nyumba. kwa kweli kila mtu anaguswa na hili, unless fisadi. hujamzungumzia mwalimu grade A. Tupo pamoja!! tu
   
 7. f

  furahi JF-Expert Member

  #7
  Feb 25, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 947
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  U know what? Naunga mkono kichwa cha habari si kwa sababu naipenda CHADEMA but kwa sababu ni kweli tupu. U know what, hata hao wakereketwa wa CCM wanavyoponda OOOH Mkiandamana ndio mgao utaisha? OOOH Mkiandamana ndio maisha yatakuwa mazuri? Amini nwaambieni, hao si kwamba wanaipenda CCM bali kwa kuwa CHADEMA imeshaonekana its the only hope basi wanaichallenge ili CHADEMA wafanye kitu kuinusuru nchi. Lakini kwa bahati mbaya sana CHADEMA haina uwezo wa kufanya mabadiliko kwani rasilimali zote ziko chini ya serikali. Inachoweza kufanya ni kuishinikiza serikali kufanya hayo mabadiliko. Na maandamano ni njia mojawapo ya kushinikiza.

  Nawasikitikia sana walioweka tiki kwenye kiboxi cha kijani siku ya tarehe 31/10/2010 kwani mmesalitiwa mno na itawauma mpaka siku mtakapoamua kufanya maamuzi sahihi. Mimi kwa upande wangu sina shaka coz kura yangu nilimpa Dr. wangu wa ukweli who is the President in my heart n soul. I dont regret hata kama waliiba, but am proud 2 say nilimpa......
   
Loading...