Hatma ya Warioba mikononi mwa JK | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hatma ya Warioba mikononi mwa JK

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Jun 13, 2009.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Jun 13, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,928
  Likes Received: 83,491
  Trophy Points: 280
  Mashtaka dhidi yake yaiva
  Na Saed Kubenea

  MwanaHALISI

  SERIKALI inakamilisha taratibu za kumfikisha mahakamani Waziri Mkuu mstaafu, Jaji Joseph Warioba, MwanaHALISI limegundua.

  Waziri mkuu huyo wa zamani ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mwananchi Gold Limited (MGL) ya Dar es Salaam.

  Jaji Warioba anatakiwa kufikishwa mahakamani kujibu tuhuma juu ya matumizi ya mabilioni ya shilingi ambayo kampuni yake ilichukua kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

  Taarifa zilizopatikana juzi usiku zilieleza kuwa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU) ilikuwa tayari imewasilisha jalada la uchunguzi kwa Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) kwa hatua za mwisho.

  Tuhuma zinazomkabili Warioba zipo katika maeneo mawili. Kwanza, ni kama fedha zilizotoka BoT zilipitia mkondo sahihi na halali; na pili, kama fedha hizo zilitumiwa kama ilivyotarajiwa.

  Taarifa zilizopo zinaonyesha kuwa MGL ilichukua dola 5,512,398.55 (sawa na Sh. 6 bilioni) kutoka BoT.

  Ni upatikanaji wa sehemu ya kiasi hiki cha fedha na utata katika matumizi yake ambavyo vinaweza kumfikisha Warioba mahakamani wakati wowote kutoka sasa.

  Pamoja na kuwa mwenyekiti wa bodi, Warioba pia ana hisa katika Kampuni ya Mwananchi Gold Ltd.

  Hisa zake zinapitia kwenye kampuni ya familia yake inayoitwa Umoja Entertainment Limited.

  Wengine wenye hisa ni Vulfrida Mahalu kupitia kampuni ya familia yao iitwayo VMB Ltd.; Yusuf Mushi kupitia kampuni ya Y.M. Limited na CCM Trust ambayo taarifa zinaonyesha kuwa inamilikiwa na Warioba na Mushi.

  Makampuni haya manne ndiyo yanaunda kampuni ya Mwananchi Trust Limited yenye hisa 1,123 katika Mwananchi Gold Limited.

  Kwa mujibu wa nyaraka za Wakala wa Usajili wa Makampuni na Biashara (BRELA), wenye hisa wengine katika Mwananchi Gold Limited, ni BoT yenye hisa 500, Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) lenye hisa 375 na Chimera Company Limited (ya raia wa Italia) yenye hisa 500.

  Habari za kuaminika kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) zinasema mipango ya kumfikisha Warioba mahakamani tayari imekamilika.

  Warioba ndiye aliongoza Tume ya Kuchunguza Rushwa (Tume ya Warioba), iliyoundwa na Rais Benjamin Mkapa mara baada ya kuingia madarakani Oktoba 1995.

  Kampuni ya Mwananchi Gold Limited, ilianzishwa na serikali kwa lengo la kusafisha dhahabu inayochimbwa nchini.

  Lengo la Serikali la kuingia ubia katika kampuni hiyo lilikuwa kununua dhahabu kutoka kwa wachimbaji wadogo ambapo matarajio yalilenga uuzaji wa asilimia 85 ya dhahabu katika bei ya soko la dunia.

  Hata hivyo, miezi miwili iliyopita, Warioba alinukuliwa akimweleza mwandani wake kuwa ana nyaraka zote zinazohusu matumizi ya fedha zilizoingia kwenye Mwananchi Gold Limited na kwamba haki yake ya kujieleza ikizingatiwa, atajieleza “vizuri tu.”

  Mapema mwaka huu, Waziri wa Sheria na Katiba, Mathias Chikawe aliwaambia waandishi wa habari kuwa, “Kama Warioba hana kosa, hofu ya nini?”


  Alikuwa akijibu madai ya Warioba kuwa anasumbuliwa sana na anatishiwa kukamatwa na kushitakiwa. Alisema, “Kama wanataka kunikamata si wanikamate?”

  Lakini taarifa za kuaminika zinasema Chikawe “alimuuma sikio” raia mmoja wa Tanzania anayeishi nje ya nchi akisema, “Lazima Warioba atafikishwa mahakamani.”

  Aidha, Jaji Warioba alipoulizwa juzi Jumatatu, kuhusu hatua ya kufikishwa mahakamani wakati wowote sasa alisema, “Ah, sijui wanataka nini, maana mambo haya nimeshaeleza na naona kama yameisha.”

  Naye DPP, Eliezer Feleshi alipoulizwa na gazeti hili kuhusu taarifa hizi, aliuliza haraka, “Wewe amekwambia nani haya?”

  Alipoambiwa ni taarifa kutoka vyanzo vya habari vya gazeti, alisema yeye yuko safarini na kuongeza, “Basi nitafute keshokutwa Jumatano (leo).”

  Ofisa mmoja mwandamizi wa TAKUKURU ameithibitishia MwanaHALISI kwamba kesi ya Mwananchi Gold Limited ipo mbioni kukamilika.


  Naye Msemaji wa Wizara ya Sheria na Katiba, Omega Ngolle alipoulizwa juu ya mipango ya kumfikisha Warioba mahakamani, alisema yupo nje ya ofisi kikazi.

  “Nipo Shinyanga kikazi; mafaili yapo ofisini. Haya mambo ya lini Warioba atafikishwa mahakamani, siwezi kuyajua ndugu yangu. Nakuomba uwasiliane na DPP Feleshi, atakueleza,” alisema Ngolle.

  Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Edward Hosea, hakupatikana jana kuzungumzia suala hilo.
   
 2. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #2
  Jun 13, 2009
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Naona Kubenea hapa kashindwa tu kuandika kwamba "alimwambia wana JF". JF iko mbele daima.

  Warioba hana haja ya kuogopa, kama hajaiba pesa za umma basi atasafisha jina lake mahakamani.
   
 3. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #3
  Jun 13, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,928
  Likes Received: 83,491
  Trophy Points: 280
  Kwa jinsi ninavyomfahamu Warioba, huyu Mzee hana chembe ya ufisadi katika damu yake na sidhani kama ana kesi yoyote ya kujibu hapa. Badala ta kuwafikisha mahakamani akina Rostam na mapapa mafisadi wenziye wanataka kwenda kumshupalia huyu Mzee ambaye hana kosa lolote. Tusubiri tuone hili sakata litaendaje.
   
 4. P

  Pakacha JF-Expert Member

  #4
  Jun 13, 2009
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 816
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Watanzania mnapaswa kuwa na tabia nzuri. Sasa kama watu wamestaafu ya nini kuwazonga? Majina sijui Mkapa, Warioba, Salim, Mwinyi achaneni nayo. Kule UK Tony Blair (pamoja na ujasiri wake) hatajwi tena hii leo.
   
 5. Offish

  Offish Senior Member

  #5
  Jun 13, 2009
  Joined: Aug 14, 2008
  Messages: 172
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Another smokescreen kwa sababu mafisadi kama RA hawahitaji ushahidi wa kutafutwa kwa miaka nenda miaka rudi kufikishwa mahakamani. Serikali inafanya kila liwezekanalo kuwasahaulisha watanzania ufisadi wa akina RA, EDO, et al kwa kujipendekeza kwa mashitaka yaliyokosa nguvu kama haya ya Waryoba...
   
 6. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #6
  Jun 13, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Wanachofanya ni kujaribu kumchafulia jina tu jaji Warioba. Nakubaliana na kauli ya Mtanzania hapo juu 100%
   
 7. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #7
  Jun 13, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Kama ni kweli basi Mahakamani pawe ndipo mahala pekee ka kuyajulia haya .Hebu pelekeni huko kesi iungurume.

  Kuwataja wastaafu sasa ni sawa tu kama walifanya mabaya ila kama hawakufanya ya kuiba basi akina Blair hawatajwi ndiyo sababu
   
 8. FairPlayer

  FairPlayer JF-Expert Member

  #8
  Jun 13, 2009
  Joined: Feb 27, 2006
  Messages: 4,166
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Unajua inabidi wengine watolewe kafara ili magazeti yaandike ipungue kasi ya kutajwa KAGODA na RA. Akipelekwa Warioba mahakamani itakuwa GUMZO kwahiyo mtasahau Richmonduli, Kagoda na Mambo ya RA.

  Takukuru imekuwa kama Idara ya miscommunication ya MAFISADI na Mtandao. Angalia Kesi ya Liyumba, pale hamna kesi wala nini, ndo maana Kweka ameshaachiwa huru; Kinachofanyika ni kuelekeza masikio ya WADAnganyika pengine.

  Kaeni macho.

  FP
   
 9. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #9
  Jun 13, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135

  Mkuu hii ni janja ya mafisadi kutaka kuhamisha mjadala juu yao! Yaani wanataka wananchi tuelekeze masikio na akili zetu kwa Warioba tuwaache waendelee kuchota kupitia TIB! kwa danganya toto ya Kilimo kwanza?

  Safari hii hadanganywi mtu tutawafatilia mpaka bafuni... na tutawapigia kelele tu za mwizi huyooooo!!

  Yaani hata mkituibia hamtazila kwa raha.. kuna siku zitawatokea puani!
   
 10. Tiba

  Tiba JF-Expert Member

  #10
  Jun 13, 2009
  Joined: Jul 15, 2008
  Messages: 4,511
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  Mkuu Pakacha,

  Tony Blair hatajwi tajwi kwa kuwa hakuacha madudu nyuma yake kama hawa kina Mkapa. Sijui kama kuna mwenye tatizo kubwa sana na Mzee Mwinyi!!!

  Tiba
   
 11. Kevo

  Kevo JF-Expert Member

  #11
  Jun 13, 2009
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 1,332
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Suala la kimfikisha Warioba mahakani siyo la kuzua mjadala hapa na suala la yeye kuwa msafi ni yeye mwenyewe anajua hivyo baasi kama nimsafi basi usafi wake utaonekana na kama ni fisadi atajulikana na uzuri mmoja yeye mwenyewe ameshasema ana ushahidi sasa kinachowaumiza kichwa wana JF nini hasa?au kisa RA na EDO hawajafikishwa mahakani ndio na yeye asifikishwe mahakamani?tha does not justify anything.
  Tujue huhyu ni waziri mkuu mstaafu na anijua the system vyema,kama anataka kujilinda ana uwezo huo,na kama hataki basi na haki iachwe ichukue mkondo wake!
   
 12. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #12
  Jun 13, 2009
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Una ushahidi wowote wa ufisadi wa Rostam?
   
 13. Chiwa

  Chiwa JF-Expert Member

  #13
  Jun 13, 2009
  Joined: Apr 17, 2008
  Messages: 1,388
  Likes Received: 726
  Trophy Points: 280
  Ni kweli tunachanganyana sijui kama naweza kuwa mwanasiasa mbaya sana hii
  tatizi dola tulionayo imebebwa na mafisadi na nguvu wanayo wana uwezo wa kufanya chochote
  kuna akati nawaza kama ingewezekana tuache yaliyopita na tuanze upya tuone itakuwaje
  nchi inaendeshwa kama duka la mpemba(family business ,family decison)
  na uhakika iko siku mambo yatakuwa mabaya kuzidi kongo
  watu wamechoka kupitiliza
  sisi ambao kwa sasa tumeamua kuja kuishi kijijini tunaona shida zao na hawana la kufanya
  nachoshukuru kwa sasa wameanza kuelewa kuwa walikuwa wanadanganywa
   
 14. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #14
  Jun 13, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0

  - Hii tu ndio hoja ya msingi, mengine yote ni haya haya tu ya kawaida JF.

  Respect.

  FMEs!
   
 15. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #15
  Jun 13, 2009
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Mzee Mwinyi nae alifanya madudu mengi sana wakati wake; huo ndio ulikuwa wakati wa debt-conversion pale BOT na Idris Rashid akiwa kinala wa hiyo "EPA" ya enzi za Mwinyi. Hapo ndipo wakina Subash Patel " FISADI PAPA" alipokomba mali zetu toka BOT na kujenga hotel za Whitesands na Sea Cliff [ Mzee Mwinyi alikuwa silent partner kwenye hizi hotel kabla ya kuuza hisa zake!!] Madudu ya Mwinyi ndiyo yaliyomfanya Mwalimu kusema " IKULU SIO MAHALA PA KUFANYIA BIASHARA"
   
 16. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #16
  Jun 13, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  sidhani kama kuna kesi hapo, kombe linafunikwa tu na mwanaharamu atakapopita tutarudi kwenye maisha kama kawaida
   
 17. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #17
  Jun 13, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Kusema mtu hana chembe ya ufisadi bila kujibu yaliyoandikwa kwenye Mwanahalisi hutueleweshi vizuri. Pangua hoja moja baada ya nyingine, hapo utaeleweka. Otherwise mwanga zaidi utapatikana mahakamani kama Warioba atashtakiwa.
   
 18. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #18
  Jun 13, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Nauliza tu, kwani wanaonewa?
   
 19. Pundamilia07

  Pundamilia07 JF-Expert Member

  #19
  Jun 13, 2009
  Joined: Oct 29, 2007
  Messages: 1,433
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Ukifanya 'flashback' ya michango ya baadhi ya wanaJF juu ya kupambana na ufisadi, unaweza kuona hawako objective kabisa katika mapambano hayo. Endapo kuna ushahidi wa kumfikisha mahakamani mtu yeyote mwenye tuhuma za ufisadi, nadhani tunapaswa kupongeza juhudi hizo na si vinginevyo. Inajulikana wazi kuwa kwa mtu yeyote yule kufikishwa mahakamani haimaanishi kwamba ana makosa, mahakamani ndiyo mahali pekee kwa mtu kwenda kujisafisha kama ni msafi na kama atatiwa hatiani basi ajutie yale aliyoyafanya. Ninashauri kuwa tusiangalie sura ya mtu bali tujali yaliyomo.

  Mzee Warioba asiwe na hofu hata kidogo kwani akumbuke kufikishwa mahakamani si lazima apatikane na hatia. Nadhani anakumbuka sakata la Waziri wa zamani Nalaila Kiula ambaye alishauri Kiula ashitakiwe kwa makosa yaliyohusu rushwa, lakini Kiula hakupatikana na hatia na akaachiwa huru na mahakama.
  Mzee Warioba jitayarishe na wewe ukajitete huko, usijaribu kutafuta haya mambo yaishie chini-chini kwani hatutakuelewa kabisa tena kama Mwenyekiti wa Kamati ya Rushwa ya awamu ya tatu.
   
  Last edited: Jun 14, 2009
 20. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #20
  Jun 13, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Pundamilia,
  Sisi wote hapa JF si watoto wadogo. Na katika vita ya ufisadi tunajua kinachoendelea.
  Haiingii akilini kabisa kwamba watajwa wote waliohusika na EPA, yale manyangumi, hakuna hata mmoja umesikia anachunguzwa na Takukuru. Lakini wale ambao wamekuwa mstari wa mbele kuzungumzia ufisadi, akiwemo Jaji Warioba, ndio "wanatafutiwa" mashtaka mahakamani upesi upesi kuonyesha kuwa kasi na ari mpya ya JK inafanya kweli. Sisi si watoto wagodo hata kidogo.
   
Loading...