Hatma ya Jerusalem: Tanzania yapingana na Trump UN

Mkuu kwani sheria za AU zinasemaje pia kuhusu Morocco kuikalia kimabavu Sahara Magharibi ?

Kama Sheria za UN hazitambui Israel kuikalia Yerusalemu, kulikuwa na haja gani kwa hiyo kura kupigwa katika mkutano wa UN?

Tanzania tutapata faida gani kuiunga mkono Morocco dhidi ya Sahara Magharibi?

Narudia kusema tena hapa, katika hili la Kuipinga Israel, Tanzania tumekosea kwa 100%, tumekuwa kama mapimbi vile, badala ya kuitumia kama fursa ya kuweza kutoboa kiuchumi sisi tumefuata upepo wa mgogoro usiotuhusu.
Kuhusu suala la Morocco na Sahara Magharibi, AU na Tanzania ni tamaa, maslai binafsi na rushwa ilitumika hakuna jingine hapo.
Kumbuka Marekani ndio taifa linalochangia fedha nyingi umoja wa mataifa na duniani hivyo ana ushawishi mkubwa wa kuweza kushawishi baadhi ya nchi kuwa upande wake kwa lazima, vitisho au nchi hizo kufanya maamuzi ya uoga na wa kimaslai kama ambayo wewe ulipenda na ungependa Tanzania ifanye.
Tumeona Rwanda, Malawi na Uganda hazijapiga kura. Hii inamaanisha nini? Ni "uoga tu na maslai mbele".
Huwezi kusema jambo halikuhusu wakati wewe ni mjumbe na mwanachama wa umoja huo. Kutotambua sheria zilizowekwa kwa kisingizio cha hili halinihusu na lile ni sawa ni unafiki wa kiwango cha juu na kutotaka kutambua ukweli. Moja ya majukumu ya UN ni kulinda amani, kudhibiti migogoro na vita. Na maamuzi ya Marekani ni kiashiria tosha kabisa cha kujua na kuona hali ya hatari mbeleni. Hivyo kunyamaza na kutokemea ni hatari na ni uvunjifu wa sheria za kimataifa.
 
Tumechemsha na sijui nani alitoa huo ushauri wakati Uganda, Rwanda , S. Sudan zilitoka ukumbini ambayo ni busara kubwa tu. Hivi TZ inajua inapokea kiasi gani cha misaada including global fund kutoka Marekani? MAAMUZI HAYA NI MACHAFU na hakika yatatugharimu sana
 
Tanzania inakuwa inexperience kuliko hata S. Sudan iliyopata uhuru juzijuzi?. Ni kwa nini hawakumshauri mwakilishi wetu akaenda kichwa kichwa kupiga kura? Hapa tumepingana na maandiko kwa mara nyingine!!
 
Kwa nini tusingeomba ushauri wa kina kabla ya kupiga kura? hii kuchagua makada ku assume position nyeti ilihali uwezo hawana inaanza ku back fire. Hii ni aibu sana na adhari yake tutaiona
 
Mwanzo mgumu! Trump kaonyesha njia nchi nyingine zitafuata taratibu tu achana na mambo ya ndani ya Jumuiya ya UN
 
Wawakilishi wetu wasingepiga kura kabisa. Ingesaidia mambo mengi. Kenya hawakupiga kura.
 
Tunawang'ang'ania waarabu hakuna walichotusaidia wala hawawezi. Tunaacha kuwa karibu na watu wenye akili. Bure kabisa
Wewe najua unaposema waarabu unaongelea Islam. Hivi unajua waarabu unaowaita wewe na wayahudi wote asili yao ni ndugu?.Hivi unajua gharika lililotokea kwa Noah ilikuwa ni Iraq? Hivi unajua wasraeli wengine na majority sio wakristo?.Hivi unajua YESU(ISS BIN MARIAM ) hakuleta ukristo ila alileta INJILI?.Mgogoro wa Israel na Palestina ni mpana sana kabla ya kuzaliwa YESU?
 
Tz ingekuwa neutral ingependeza. nchi changa hizi kujiingiza kwenye migogoro ya mashariki ya kati, tena ya miaka nenda rudi iliyoanza kabla TZ yenyewe haijazaliwa haina tija.
Kwanini tuwe neutral! Nchi INA maamuzi yake, tena nadhani Trump aliharibu zaidi alipotishia kuzinyima misaada
 
Wapendao kujua,
nchi 128 zimepinga azimio la Trump kuitambua jerusalem.

Nchi 9 zimemuunga mkono Trump

nchi 35 hazikupiga kura.

Ajabu ni kuwa nchi kama Canada ilitegemea kusimama na marekani lakini wame abstain,


--uingereza kwa kukwepa kuiudhi marekani ilitegemewa isipige kura,lakini wamepiga kura kulaani azimio la marekani.

Nchi zilizoiunga mkono marekani ni 9,

-Guetmalla
-hondura
-israel
-marshal island
-Nauru
-palau
-Togo
-macnesia
-na US yenyewe


very insgnificant countries
Vinchi vingine hapa ni vya wabuya madawa ya kulevya halafu ni vidogo kama ncha ya kalamu
 
Kuna watu humu wananishangaza mno,,
kama ndo kizazi hiki kina akili za hivi we are doomed,

poleni.

Ila ningekuwa mimi ndo kiongozi wa palestina wala haingekuwepo sababu ya kupigizana kelele,
kwani jerusalemu kuna madini gani pale,

jerusalem inazidiwa thamani na Nyarugusu yetu,
waachieni huo mji tuone wanafaidi nini,yanini kuuana miaka 1000 na ushee kwa sehemu ambayo siyo productive bana?
 
Kuna watu humu wananishangaza mno,,
kama ndo kizazi hiki kina akili za hivi we are doomed,

poleni.

Ila ningekuwa mimi ndo kiongozi wa palestina wala haingekuwepo sababu ya kupigizana kelele,
kwani jerusalemu kuna madini gani pale,

jerusalem inazidiwa thamani na Nyarugusu yetu,
waachieni huo mji tuone wanafaidi nini,yanini kuuana miaka 1000 na ushee kwa sehemu ambayo siyo productive bana?
 
Mji mkuu wa Israel ni Tel Aviv
Tel Aviv ulifanywa mji mkuu kwasababu tu ya chokochoko zilizokuwa zinaendelea. Lakini Jerusalem ndio mji mkuu halali wa Israel. Hapo ndipo, Bwana Mungu wa Israel, Muumba wa mbingu na nchi alipopachagua ili kuliweka Jina lake hapo Milele. Na hivyo ndivyo itakavyokuwa. Kura za wanadamu hazitaamua.
 
Wapendao kujua,
nchi 128 zimepinga azimio la Trump kuitambua jerusalem.

Nchi 9 zimemuunga mkono Trump

nchi 35 hazikupiga kura.

Ajabu ni kuwa nchi kama Canada ilitegemea kusimama na marekani lakini wame abstain,


--uingereza kwa kukwepa kuiudhi marekani ilitegemewa isipige kura,lakini wamepiga kura kulaani azimio la marekani.

Nchi zilizoiunga mkono marekani ni 9,

-Guetmalla
-hondura
-israel
-marshal island
-Nauru
-palau
-Togo
-macnesia
-na US yenyewe


very insgnificant countries
Big up hizo nchi zilizoiunga Marekani mkono. Hizo ndizo nchi zenye akili.
 
Tunawang'ang'ania waarabu hakuna walichotusaidia wala hawawezi. Tunaacha kuwa karibu na watu wenye akili. Bure kabisa
issue siyo waarabu tu Tanzania inajikita kwenye UN resolution on middle east amabazo zinautambua mji wa Jerusalem kama ni wa wote yaani wapalestina na Israel
 
Tanzania inakuwa inexperience kuliko hata S. Sudan iliyopata uhuru juzijuzi?. Ni kwa nini hawakumshauri mwakilishi wetu akaenda kichwa kichwa kupiga kura? Hapa tumepingana na maandiko kwa mara nyingine!!
Hili zigo Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje atalibeba maana yeye ndiye aliongea na vyombo vya habari siku Trump alipodeclare Jerusalem ni capital ya Israel. Busara ilikuwa ni kuwa neutral hukubali hukatai. Huu muziki wataucheza kwelikweli. Trump ana mapungufu yake lakini inapokuja imani yake ya kikristu hasiti kusema. Amewakataza watu wake kusema Happy Holidays amesema ni Merry Xmass kulingana na imani.
 
Back
Top Bottom