Hatma ya GNU Zanzibar: Karama itaamua badala ya hekima, Chaguzi ndogo zinafichua dhamira

KISHADA

JF-Expert Member
Oct 18, 2012
2,224
3,290
Mada inahusika

Hili la GNU ni mwiba kwa Watawala. CCM inawakwaza kuitekeleza Katiba inayotaka GNU, huku wakivurugana.

Utekelezaji wake unategemea Karama na wala si Lazima. Hekima ni mwiko.

Naam. Hii GNu ya Dk Mwinyi mwisho wake unaonekana kwa macho ya karibu. Nia njema au mbaya itaonekana kwenye maamuzi Magumu.

Pengine matukio ya vifo vya walioshikilia majimbo ya Pemba, Mungu alivipangilia kuonesha rangi Halisi. Imekuwa mkosi kwa Dr Mwinyi.

UCHAGUZI WA PANDANI
jimbo lilikuwa la ACT, kuliripoptiwa figisu balaa kwenye uchaguzi mdogo mpaka kuleta msuguano wa ndani kwenye GNU. Taarifa zilidokeza Viongozi kuekeana misimamo ndipo haki ikatendeka. CCM walidinda na kukemeana kwamba Maagizo ya Chama ni kushinda. Ilikuwa ni mvutano wa Legacy ya chama 2020 dhidi ya maridhiano. Maridhiano yalishinda kwa shingo upande.

Jimbo la Konde.
Hapa sasa msumari umegota. GNU ilishatikiswa kwa kuonekana Mawaziri wa Chama Tawala na Upinzani kujibizana hadharani. Si hayo tu, Mkuu wa Mkoa kupanda jukwaa la CCM na kuhakikisha kutumia nafasi yake ya Mwenyekiti wa Usalama wa Mkoa bila kukemewa wala bubudha.

Kilichotokea jana tarehe 18 Julai, 2021 ni shida dhidi ya maridhiano. Kauli za Viongozi wa ACT haziashirii mwisho mwema.

Uchaguzi ulienda vyema licha ya kasoro na malalamiko madogo madogo. Ujumuishaji ndio tatizo. Fomu hazikujazwa vituoni licha ya kura kujulikana. Ubabe wa NEC na Polisi ulikuwa dhidi ya GNU na Hulka ya Dk Mwinyi.

Matokeo yamewashangaza wengi. Hiyo mbinu ya Kubalance ili kutumia uchochoro huo kumtangaza mshindi wa TUME kumeinajisi ladha ya Maridhiano.

Hebu Ona matokeo:
Sheha M Faki CCM 1796
Mohamed S. Issa ACT 1,373
Mohamed S Said CHADEMA 857
Salama K. Omary CUF 624

Matokeo hayo ni uchonganishi wa wazi dhidi ya GNU, wananchi na vyama husika.

Kwenye hilo jimbo CCM haina ubavu huo wa kura. Hata vyama vya Upinzani vimechonganishwa kwa kupewa kura wasizostahili dhidi ya ACT lengo ikiwa ni kuvuruga ili uchochoro upatikane.

Taarifa tulizonazo, mawakala wa hivyo vyama wanashangaa . Wamezipata wapi hizo kura wakati hesabu zao vituoni haziko hivyo?

HATMA
Nini hatma ya GNU? Karama zitaamua badala ya Hekima? Ndio mtazamo huo. CCM wanateseka na Katiba ya Zanzibar, Legacy ya kulazimisha ya CCM 2020 inaitesa Zanzibar ya GNU. Inatesa dhamira na inafichua undumilakuwili.

Nani mkweli wa maridhiano ya kweli? Chaguzi ndogo zimetibua dhamira na nia ovu.

Mungu hadhihakiwi.

Kishada
 
Hapo kwenye CHADEMA na CUF wamewaongezea kura kuwaaminisha watu
 
Hapo kwenye CHADEMA na CUF wamewaongezea kura kuwaaminisha watu
Kilichofanywa na NEC wanakijua wenyewe. Kura za vituoni waligoma kuziingiza kwenye fomu za Matokeo na kuondoka nazo kwa ubabe.

Yalipotoka matokeo kila mtu hakuamini.
 
Back
Top Bottom