Hatma ya Dk. Slaa kujulikana kesho

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,007
Wakili Tundu Lissu aliwaaibisha waliofungua kesi hii dhidi ya Dk Slaa, hivyo kama sheria zikifuatwa Dk Slaa atashinda na walalamikaji kuamriwa kumlipa gharama zote za kesi hiyo. Kama mjuavyo katika sheria za Tanzania chochote kinaweza kutokea, kuna uwezekano Jaji kishapigwa pochi la hali ya juu na chama cha mafisadi ili wamuangushe Dk Slaa, maana kwao utakuwa ni ushindi mkubwa sana hasa ukitilia maanani mafanikio makubwa ya Dk Slaa katika ya kufunua uozo wa BoT, mikataba feki na ufisadi mwingine unaowahusu mafisadi ndani ya CCM na SIRIKALI

Hatma ya Dk. Slaa kujulikana kesho

2008-05-14 16:08:31
Na Mwandishi wetu, Jijini

Hatma ya ubunge wa Mheshimiwa Dk. Wilbroad Slaa wa Jimbo la Karatu, CHADEMA, juu ya kuendelea na wadhifa huo ama la itajulikana kesho baada ya Mahakama Kuu Kanda ya Arusha kutoa hukumu ya kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa ubunge wake.

Hukumu hiyo inatarajiwa kutolewa mishale ya saa 6:00 na Jaji Robert Makaramba, ambaye juzi aliahidi kutoa hukumu hiyo kesho baada ya mawakili wa mashitaka, Bw. Mpaya Karama na Hezron Mwaluko kukamilisha hoja zao.

Awali, mawakili hao walipinga hoja za wakili wa Dk. Slaa, Bw. Tundu Lissu, ambaye aliiomba mahakama kuwapa adhabu kali kwa kukubali kwao kutumika kufikisha mahakamani hapo nyaraka za kugushi ili kuipotosha mahakama.

Kesi hiyo inatokana na makada watatu wa CCM, wakiongozwa na Joseph Haimu, kufungua kesi ya kupinga ushindi wa Dk. Slaa.

Walifungua kesi hiyo kwa madai kuwa taratibu za uchaguzi zilivurugwa na msimamizi ikiwemo kutohesabu vizuri kura na kwamba kama zingehesabiwa kwa umakini, mgombea wa CCM, Bw. Patrick Tsere angeibuka mshindi.

SOURCE: Alasiri
 
Wakili Tundu Lissu aliwaaibisha waliofungua kesi hii dhidi ya Dk Slaa, hivyo kama sheria zikifuatwa Dk Slaa atashinda na walalamikaji kuamriwa kumlipa gharama zote za kesi hiyo. Kama mjuavyo katika sheria za Tanzania chochote kinaweza kutokea, kuna uwezekano Jaji kishapigwa pochi la hali ya juu na chama cha mafisadi ili wamuangushe Dk Slaa, maana kwao utakuwa ni ushindi mkubwa sana hasa ukitilia maanani mafanikio makubwa ya Dk Slaa katika ya kufunua uozo wa BoT, mikataba feki na ufisadi mwingine unaowahusu mafisadi ndani ya CCM na SIRIKALI
Kamanda huyo Jaji ni Jirani yako nini? Naona umeshajua kuwa hata toa hukumu nzuri kwa slaa...

Kama hali ndio hii kuna haja gani ya kuwa na Mahakama, slaa alikuwa na haja gani ya kuweka wakili iwapo anajua/anategemea kuwa Jaji siku ya kuhukumu atapendelea?
 
Kungekuwa na sheria bongo zinazolinda maslahi ya nchi na siyo yale ya chama cha mafisadi na mafisadi unadhani mafisadi waliohusika na EPA, Richmonduli, ununuzi wa Rada, kujimilikisha Kiwira Coal Mining katika mazingira ya kifisadi, kujimilikisha mgodi wa Buhemba katika mazingira ya kifisadi wangekuwa wako huru wakiendelea kula maraha ya utajiri wao wa haramu? Usijifanye hujui kama Bongo hakuna sheria, sheria zilizokuwepo ni za kulinda mafisadi na siyo maslahi ya nchi na Watanzania
 
Na yule jambazi rafiki ya fisadi Lowassa, nani yule? Nyari nadhani. Si aliachiwa baada ya waziri mkuu kukutana chemba na jaji mkuu wa kesi hiyo? Ndiyo bongo hiyo bwana.
 
Guys, let's be optimistic as we wait for the verdict

people are trying to be realistic, yaliyotabiliwa na Babu ndo yanayotarajiwa kujili.

hicho chama cha mafisadi kiko makina kwa kuandaa mabomo na kumpa mtu ili ayalipue tu. tayari wanajua matokeo ya kesi na tayari wameanza kusherehekea.

any way let us wait. but also plan for the revenge when things goes as babu said.
 
Sioni umuhimu wa kusubiri hukumu hii iwapo Majaji wa JF wameshatoa hukumu zao...
 
Sioni umuhimu wa kusubiri hukumu hii iwapo Majaji wa JF wameshatoa hukumu zao...

Usiwe extrmist na wana JF nadhani wanabodi wametoa mawazo yao na hisia zao ambazo haziathiri maamuzi yanayosubiriwa kutoka court.

Hata mie kwa utashi na ufuatiliaji wangu wa kesi ile, nampa ushindi dr. slaa kutokana na mazingira na ushahidi uliotolewa mbele ya mahakama. ila ukikumbuka namna ambavyo mahakama ya rufaa ilivyopangua kesi za Hon. Mwalusanya basi tegemea chochote kutoka kwa majaji a kizazi hiki....
 
Baada ya maelezo yako mazuri hebu jikumbushe kuhusu sahihi yako
Utashi wa Kisiasa, Unaiangamiza NCHI
 
We believe haki itatendeka. I don't trust kwamba kote kumeoza. Huko mahakamani pia kuna watu wenye uchungu na nchi yao na wana kiu ya haki kabisa kama sisi. I hope this is not just hope!
 
ni mengi wameyapanga CCM kuhakikisha dk slaa anatoka bungeni, na kesho wanakwenda kuyatimiza tu...ila iko cku uonevu huu utakwisha, na si siku nyingi kutoka hiyo kesho.
 
We believe haki itatendeka. I don't trust kwamba kote kumeoza. Huko mahakamani pia kuna watu wenye uchungu na nchi yao na wana kiu ya haki kabisa kama sisi. I hope this is not just hope!

kitila mkumbo...
amini usiamini kesho jamaa wanakwenda kukamilisha kumtoa slaa bungeni.
na hata uchaguzi ukirudiwa wameshapanga njia zoooote za kumshinda...huo ndo ukweli ambao haukwepeki.
hao watu wa mahakama unaowasema ni wazi kuwa wana njaa sana so haiwezekani kuwa upande wa slaa ambaye ni mtu safi asiye na historia ya rushwa.
 
Tumeona mifano ya viongozi wengi tu wa upinzani wakiburuzwa mahakamani. Lakini ni wachache sana ambao nimeona wakitumikia vifungo jela au wakilipishwa fine kutokana na kauli zao walizotoa kuhusu viongozi wa serikalini.

Hivyo nina kila sababu ya kuamini kuwa haki itatendeka.
 
Watchu talkin' bout Zero?
 
Watchu talkin' bout Zero?

It is as straight as it is. Maelezo yanatosha. Kwamba sio mara ya kwanza kwa kiongozi wa upinzani kufikishwa mahakamani. Mifano iko mingi ya viongozi mbalimbali waliofikishwa mahakamani. Mifano michache ni Mtikila na Mrema. Lakini sijawahi kusikia viongozi hawa wakitumikia vifungo, au wakipigwa fine ya mamilioni ya shilingi eti kwa kuwa wamewakashifu viongozi wa serikali. Naamini Dr. Silaa atapitia kwenye mkondo huo huo.

Ni siasa tu.
 
Hizo kesi zinakuwa hazina masirahi kwa CCM, Mtikira ameshakaa ukonga kwa mwaka mzima, mrema afungwi kwakuwa nakuwa amesema ukweli na baadae wanafuta kesi zao na kumwachia. lakini lets hope Dr. siraa bado yuko bungeni.
 
Back
Top Bottom