Hatma ya Dk. Slaa kujulikana kesho

Hizo kesi zinakuwa hazina masirahi kwa CCM, Mtikira ameshakaa ukonga kwa mwaka mzima, mrema afungwi kwakuwa nakuwa amesema ukweli na baadae wanafuta kesi zao na kumwachia. lakini lets hope Dr. siraa bado yuko bungeni.

kwa kuongezea ni kuwa mrema huwa hafungwi kwa sababu ni CCM.
 
Wakimtoa Slaa Bungeni, Serikali ya Kiwete itkuwa imepata ushindi kuliko hata walioupata desemba 2005. Nadhani Mwaluko na Kamara wanajua kabisa kuwa walikuwa wanatetea uongo. Wameshavuna chao toka CCM na nina wasiwasi kama malipo yalifanywa na DC au hao wakereketwa (or should we call them Wakeketwa). But whatever they do, Slaa will remain a hello not only to the voters in Karatu lakini kwa Watanganyika na Watanzania kwa ujumla.
 
Kamanda huyo Jaji ni Jirani yako nini? Naona umeshajua kuwa hata toa hukumu nzuri kwa slaa...

Kama hali ndio hii kuna haja gani ya kuwa na Mahakama, slaa alikuwa na haja gani ya kuweka wakili iwapo anajua/anategemea kuwa Jaji siku ya kuhukumu atapendelea?

Mkuu mahakama zetu zinaendeshwa sijui niseme kisiasa?

Atakaye fika Karatu kesho atatupa habari.

Unajua nilipofika Mjini Bukoba wakati inasomwa hukumu ya Rwakatare kwanza mji mzima ulifurika Polisi wa kila aina may be wengine walichukuliwa mikoa ya jirani. Halafu kila polisi alikuwa na silaha nzito, nzito kiasi kwamba kila mwananchi aliyekuwa mjini angeweza kukabiliwa na polisi wake. Yale yale ya Mugabe.

Sasa hukumu yenyewe Jaji aliingia na ndege ya kukodi, baada ya kufika mjini wakati huo ni pata shika, alisoma hukumu mithiri ya ya Kivuitu wakati anamuweza Kibaki madarakani. Na alipo maliza kusoma hukumu huku ndege inamsubiri alielekea uwanja wa ndege wakati pata shika ya kamata kamata zikiendelea mjini.

Wakati hayo yote yanatokea kila mwana CCM alikuwa akifanya fujo inavyowezekana lakini aliyekuwa anatwangwa mabomu alikuwa ni yule anayetaka kuhoji kilichotokea.

Kejeli za kila aina ziliendelea huku, nikiona mgombea wa CUF akitishiwa kuwa anaweza kufirisiwa hata kale kauwezo alikonako.

Mimi wakati nikiwa Mgeni Mji huo niliona muhubiri wa dini akihubiri lakini pia anachanganya siasa, sikuvumilia nilitaka nimkabe hili nimpeleke polisi. Kabla sijafanya hivyo nikatonywa kumbe ni diwani wa CCM anafanya hivyo hili wapinzani waweze kukamatwa.

Kila mwananchi alirahani hukumu iliyotolewa hakuna aliyetegemea alichokiona. Mimi mpita njia nilibaki kujiuliza kama kweli hukumu kama inaweza kutolewa hata mtu wa kijijini akaweza kuhoji uhalali, halafu kutumika kwa nguvu kuna ulazima gani?

Lakini pia nilishihudia vijana ambao walikuwa tayari hata kufanyiwa chochote wakidai kuwa hawawezi kuvumilia kunyangwanywa haki yao. Wengine hata walikuwa wakidiriki kuattack polisi.

Sasa katika hili lolote linaweza likatokea, Lakini tunategemea hata wakubwa wa nchi wanapenda maendeleo ya Tanzania.

 
Jamani tupatieni matokeo ya hiyo kesi au bado hukumu inasomwa? unajua Jaji akiamua kumwangusha mpinzania baada ya kuwa amekuwa compromised na Chama fulani, anaandika hukumu ndeeeefu! Wabunge wema tunawapoteza bila sababu, mzee wetu wa Kagera walimbwaga bila sababu! na aliwahi kusema Bungeni kuwa wote wameingia kwa rushwa (Lakini ukweli unauma na hivyoa he paid for speaking the truth).
 
We believe haki itatendeka. I don't trust kwamba kote kumeoza. Huko mahakamani pia kuna watu wenye uchungu na nchi yao na wana kiu ya haki kabisa kama sisi. I hope this is not just hope!

Finally, this hope has been translated into reality!
 
Back
Top Bottom