BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,820
- 287,889
Wakili Tundu Lissu aliwaaibisha waliofungua kesi hii dhidi ya Dk Slaa, hivyo kama sheria zikifuatwa Dk Slaa atashinda na walalamikaji kuamriwa kumlipa gharama zote za kesi hiyo. Kama mjuavyo katika sheria za Tanzania chochote kinaweza kutokea, kuna uwezekano Jaji kishapigwa pochi la hali ya juu na chama cha mafisadi ili wamuangushe Dk Slaa, maana kwao utakuwa ni ushindi mkubwa sana hasa ukitilia maanani mafanikio makubwa ya Dk Slaa katika ya kufunua uozo wa BoT, mikataba feki na ufisadi mwingine unaowahusu mafisadi ndani ya CCM na SIRIKALI
Hatma ya Dk. Slaa kujulikana kesho
2008-05-14 16:08:31
Na Mwandishi wetu, Jijini
Hatma ya ubunge wa Mheshimiwa Dk. Wilbroad Slaa wa Jimbo la Karatu, CHADEMA, juu ya kuendelea na wadhifa huo ama la itajulikana kesho baada ya Mahakama Kuu Kanda ya Arusha kutoa hukumu ya kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa ubunge wake.
Hukumu hiyo inatarajiwa kutolewa mishale ya saa 6:00 na Jaji Robert Makaramba, ambaye juzi aliahidi kutoa hukumu hiyo kesho baada ya mawakili wa mashitaka, Bw. Mpaya Karama na Hezron Mwaluko kukamilisha hoja zao.
Awali, mawakili hao walipinga hoja za wakili wa Dk. Slaa, Bw. Tundu Lissu, ambaye aliiomba mahakama kuwapa adhabu kali kwa kukubali kwao kutumika kufikisha mahakamani hapo nyaraka za kugushi ili kuipotosha mahakama.
Kesi hiyo inatokana na makada watatu wa CCM, wakiongozwa na Joseph Haimu, kufungua kesi ya kupinga ushindi wa Dk. Slaa.
Walifungua kesi hiyo kwa madai kuwa taratibu za uchaguzi zilivurugwa na msimamizi ikiwemo kutohesabu vizuri kura na kwamba kama zingehesabiwa kwa umakini, mgombea wa CCM, Bw. Patrick Tsere angeibuka mshindi.
SOURCE: Alasiri