Hatma ya Bajeti ya Nishati na Madini - Taarifa kwa Umma | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hatma ya Bajeti ya Nishati na Madini - Taarifa kwa Umma

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by n00b, Aug 10, 2011.

 1. n00b

  n00b JF-Expert Member

  #1
  Aug 10, 2011
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 952
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 60
  Leo tarehe 10 agosti 2011 mbunge wa Ubungo (John Mnyika) aliomba muongozo wa spika bungeni kwa mujibu wa kanuni 68 (7) kutaka serikali itoe maelezo kwanini ahadi ya waziri mkuu ya kuzishirikisha kamati za bunge katika kuandaa mpango wa dharura wa umeme na maelezo kuhusu nishati na madini haijatekelezwa na kutaka muongozo kuhusu utaratibu gani utatumika kuendeleza mjadala tarehe 13 Agosti.

  Ukirejea majibu yaliyotolewa utabaini kwamba serikali inakusudia ‘kufunika kombe mwanaharamu apite' kuhusu bajeti ya nishati na madini; rejea hapa chini tamko lake la tarehe 8/8 kuhusu hatma ya bajeti ya wizara ya nishati na madini:   
 2. M

  MPadmire JF-Expert Member

  #2
  Aug 10, 2011
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 2,628
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  Serikali ya Tanzania haina pesa kabisa, serikali imefulia sana.

  Serikali imekopa mpaka kwenye benki !! !!! ...!!! HAIJAWAHI TOKEA TOKEA KIPINDI CHA MWINYI.

  Sasa hela zitatoka wapi walete umeme?

  Nasikia NSSF ndo watatoa hela za miradi ya umeme.

  NSSF wanatumia pesa za wafanyakazi sekta binafsi. na wafanya kazi sekta binafsi hawawezi kukopeshwa na taasisi yoyote kwa sababu hawana dhamana. (Hata Bayport, PRIDE e.t.c) hawawezi kukopesha sekta binafsi.

  HELA za NSSF zinahujumiwa kwa sababu Sekta binafsi hawana mtetezi, TUCTA wako kimyaaaa???!!!

  Angalia NSSF imejenga Machinga Complex, na bado wanataka kununua Magenerator wazalishe umeme wa dharura.

  Ila mfanyakazi mwenye hela NSSF hawazi kupata dhamana ya Mkopo NSSF.

  Hivyo hii serikali ni legelege, Bajeti ua Nishati na Madini italetwa Vilevile na maelezo kibao na ahadi nyingi sana. Mchakato mchakato na 10% moyoni
   
 3. t

  tusichoke JF-Expert Member

  #3
  Aug 10, 2011
  Joined: Apr 2, 2011
  Messages: 1,286
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  <br />
  <br />
  Kama serikali ingekuwa makini hivi sasa tungeshaona juhudi fulani katika uzalishaji umeme ,wiki tatu zimekatika hali iko vilevile wabunge wa ccm wameshawekwa sawa kupitisha bajeti isiyo na tija ndio maana serikali haina shaka.Kwa upande mwingine watanzania tuondoe matumaini ya bei ya mafuta kushuka kwani ili yashuke bei ni lazima kodi ipunguzwe.kwa aina ya serikali anasa tuliyonayo haitashusha kodi ,VASCO DAGAMA NDIO ANAYEONGOZA KWA ANASA KILA SIKU ANASAFIRI TUUUU,IT IS TOO MUCH,akumbuke na huo ni ufisadi mkubwa.
   
Loading...