HORSE POWER
JF-Expert Member
- Feb 22, 2015
- 2,212
- 1,552
Habari wanajf!
Kwa muda mrefu sasa kilio kikubwa cha Watanzania wengi hapa nchini ni UFISADI.Ufisadi ni kikwazo kikubwa cha maendeleo ya nchi yetu.Wengi wamepiga kelele juu ya suala hili kama wanahabari,NGOs,vyama vya siasa n.k.Kwa hakika Watanzania walitangaza vita na ufisadi.Ni dhahiri Watanzania walitangaza vita dhidi ya adui yao hatari kabisa kwa ustawi wao na vizazi vyao.Lakini vita yoyote lazima iwe na JEMEDARI wa kuongoza mashambulizi dhidi ya adui,kwa bahati mbaya jemedari wa kuongoza vita hii ALIKOSEKANA.Kwa kweli HAKUWEPO maana sote ni mashahidi sina haja ya kulizungumzia hili.
Bahati ilioje sasa tunae jemedari wa kuongoza vita hii.Tena jemedari huyu amedhamiria hasa kushinda vita hii kwani dalili ziko wazi.Bado safari ni ndefu mno lakini hatuna budi SOTE tushike silaha ili tushinde vita hii ngumu.Mafisadi hawa na jeshi lao wana ngome nyingi,kila mmoja awe 'jasusi' ili kutambua ngome zao tayari kabisa kwa kunyukwa na kusambaratishwa.Tumpe ushirikiano jemedari wetu,tumlinde na tumuombee.
Naomba kutoa hoja!