Hatimaye Zawadi za BSS (2009) zawekwa Wazi

Mbonea

JF-Expert Member
Jul 14, 2009
640
20
Friday October 09, 2009 10:56 AM BT
Hatimaye zawadi za mshindi wa shindano la Bongo Star Search siku ya jana ziliwekwa wazi na Chief Judge wakati akiongea na waandishi wa Habari kwenye ukumbi wa Habari Maelezo.
press.jpg

Hatimaye zawadi za mshindi wa shindano la Bongo Star Search siku ya jana ziliwekwa wazi na Chief Judge wakati akiongea na waandishi wa Habari kwenye ukumbi wa Habari Maelezo.

Akizitaja zawadi pamoja na tarehe na ukumbi zitakapofanyika fainali za mwaka huu, Chief Judge Madame Rita alisema mshindi wa Mwaka huu atajinyakulia jumla ya shilingi Milioni 25 (Tsh 25,000,000/-) wakati mshindi wa Pili ataondoka na Tsh 5,000,000/- na yule watatu ataondoka kibindoni na Tsh 3,000,000/- na Tsh 500, 000/- toka Shear Illusion na wa Nne ataondoka na Tsh 1,500,000/-, Wakati yule wa tano ataondoka na Tsh 1,000,000/-.

Madame Rita aliongeza zaidi ya kuwa kutakuwa na burudani pia toka kwa wasanii wakubwa hapa Bongo kama AY, Shaa, Baby Madaha, Feisal na Abubakary Mzuri.

"Kama nilivyowaambia tumeboresha zaidi zawadi za washindi na kila mwaka ndio zinazidi kukuwa, Asante kwa Sponsor's wetu wote kwa kuiwezesha Bongo Star Search mwaka huu" alisema Chief Judge.

Washiriki watakaopanda jukwaani kugombea kitita hicho ni Jackson George (Tanga), Peter Msechu (Kigoma), Pascal Cassian (Mwanza), Kelvin Mbati (Dar) na Beatrice William (Mwanza).

Chief Judge alitumia Fursa hiyo kuwashukuru Sponsor's wa BSS 2009 ambao ni Vodacom Tanzania, Kilimanjaro Premium Lager, Family Health na Kilimanjaro Drinking Water.

Zaidi ya Kuonekana Live kwenye Tv kwa mara ya kwanza kabisa katika historia ya shindano hilo litaonyeshwa LIVE kupitia kwenye tovuti yao hapa hapa Dar411.com

Kwa kujipatia tiketi yako mapema unatakiwa ufike kwenye vituo vifuatavyo, Maduka ya Shear Illusion, Steers (Samora), Zizzou Fashion, Manywele (Kinondoni) na Best Bite Namanga.
 
Huh..! Kumbe kuna mambo mazuri pale ndo maana wale vijana wanafight kivile! Hongera waandaaji na wabunifu wa vitu vya jinsi hii, maana mlikuwa na uwezo wa kukaa na hela zenu na kuzila wenyewe na watoto wenu. Kweli mnajitoa sana maana gharama za maonyesho yote tunayotazama siku za jumapili zinaonyesha wazi kuwa ni kubwa! Mliopo Dar nadhani mtafaidi sana fianal hii, acha sisi tukasimike mihogo ya mfungo wa mwakani!
 
Bila shaka mkuu... Uzuri ni kwamba sponsors wameongezeka n ushindani ni mkubwa.
 
Pia nina wasiwasi kam mshindi wa tanO atapata hiyo laki moja uliyoiandika hapo juu kwenye bandiko! Nadhani labda ulimaanisha 1,000,000/=. Just an IMAGINATION.
 
Pia nina wasiwasi kam mshindi wa tanO atapata hiyo laki moja uliyoiandika hapo juu kwenye bandiko! Nadhani labda ulimaanisha 1,000,000/=. Just an IMAGINATION.
Sorry! Ni Million moja mkuu
 
Muda wa kuonyesha mpambano huo ni saa ngapi mkuu? maana wengine tunakaa mbali na Dar hutuwezi kuja ukumbini........nijulishe pls..
 
Maadam Rita hongera kwa kupewa zawadi ya jina la mtoto wa mshiriki mmojawapo
toka kule kwa wanachapa ya ng`ombe.
HONGERAAAAAAAAAA
 
Back
Top Bottom