Hatimaye Yamenikuta

Rugberna

Senior Member
Jun 5, 2015
154
212
Ni miaka 12 sasa tangu tulipokutana kwa mara ya kwanza,baada ya urafiki wa miaka 3 nikaamua kumueleza hisia zangu,,akasema mambo ya mapenzi mpaka tumalize shule kwa sasa tuendelee kuwa marafiki tu, kwa sababu alikuwa kila kitu kwangu nilikubali alichokisema na urafiki ukaendelea,kwetu pakawa kwao na kwao pakawa kwetu kila aliyetujua hakuuamini urafiki wetu kuwa ni wa kawaida tu.Miaka ikapita hatimaye tukamaliza kidato cha 6 na hapo tukaanza rasmi mahusiano yetu.Nilikiwa mwanaume wa kwanza kwake,na hapo ndipo aliponikamata kabisa kwani ata pale nilipokuwa najipoza wakati naendelea kumsubiri huyu nikaachana napo,amebaki peke yake.Msichana wa kwanza kumpenda na natamani awe wa mwisho.
Baada ya miaka yote hiyo lile tatizo ambalo mwanzoni tuliliona la kawaida limekuwa kubwa.Dini inaenda kututenganisha,niliona ni rahisi kwangu kubadili dini sababu nimekuwa kwenye misingi ya dini yake kwa muda mrefu,(shule pia ilichangia kwani nimesoma boarding katika shule za dini tangu primary adi advance) lakini kila nikikumbuka mzee alivyotengwa na familia yake baada ya kubadili dini kisa bi mkubwa na huu ugomvi uliotokea siku ya kifo chake akili yangu inagoma kabisa.Sijui natokaje hapa..
 
hahaahhaha! namkumbuka wangu miaka 3 nikasema poa nabadiri dini ila kiutani nikasema ujue kuoa ni wa 4 ntatimiza hilo.hahahaha ikawa mwanzo wa ugomvi.

Mwanzoni unaliona kama jambo dogo, ila kubadiri dini ni mziki mkubwa sana
 
Mwanzoni niliona rahisi tu lakini sasa nataka kufanya uamuzi hii reaction inayotokea sikuwahi kuitarajia
 
Hizi dini 2 kubwa,sitaki kuzitaja ili kuepusha comments zenye misingi ya kidini
Mkuu mbona binafs sion mahal patakapo leta shida ukisema we ni mwisilam na yeye ni RC au kinyume chake?

Nb.mwanaume kubadili dini kwenda ya mwanamke ni tatizo,mwanamke ndio wanasema hana dini so mwambie aje kwenye dini yako..ukipofuka mapema kwenye mapenz utaumia baadae kijana

Ila na wewe sikiliza moyo wako unavyosema mm nmechangia kama wengine!
 
Tatizo ndugu japo bi mkubwa anasema ananisupport kwa lolote nitakaloamua lakini wajomba wanagoma na sisi watu wa Pwani mjomba ana sauti kubwa
Labda mjomba wako kwa kweli kwan we mtoto wa nje ya ndoa??? Kama jibu ndio hapo sawa, lakini nikuulize walikuchangia anything kwenye maisha yako??? Mpaka unafika hapo wao walikua na msaada wowote??? Mimi ni wa pwani mwenzio lakini kwenye swala la kua na mwenza wangu maisha hapo waniachie mwenyewe jaramba langu nihangaike nalo,
 
Mkuu mbona binafs sion mahal patakapo leta shida ukisema we ni mwisilam na yeye ni RC au kinyume chake?

Nb.mwanaume kubadili dini kwenda ya mwanamke ni tatizo,mwanamke ndio wanasema hana dini so mwambie aje kwenye dini yako..ukipofuka mapema kwenye mapenz utaumia baadae kijana

Ila na wewe sikiliza moyo wako unavyosema mm nmechangia kama wengine!
Hawa wanaume wa sasa wengi wao maamuzi yao wanayajua wenyewe wanashindwa kusimama kama mwanaume yani,
 
Kuna mtu anaefungisha ndoa zilizoshindikana ana cheo cha 'DC' hakuna cha biblia wala qur an mtashika katiba ya Nchi.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom