Hatimaye wanafunzi wote wa UDOM kitivo cha sayansi na jamii wamerudishwa nyumbani

Imeshazoeleka hiyooo<BR>ndo alternative pekee waliyonayo serikalini kupitia wakuu wa vyuo<BR>few days akili zikiwarudi watawarudisha tu
 
Tatizo lao walitakiwa wachanganye zao na za Mh. Lema kabla haajafanya decision.. sasa ona Lema alivyowaponza yeye anakula kuku kwa mrija. taarifa za juu kwa zinasema jamaa wamewachoka na mtakaa nyumbani mwaka mzima
acha kuwatisha madogo bana.
 
Kuwafukuza wanafunzi sio solution ya tatizo. wanachokidai ni kitu cha msingi sana utasomaje chuo bila field.
wakati wakitoa posts za kazi sifa ya kwanza ni working experience not less than 3yrs, sasa itakuwaje wakati hata field hakwenda.
Big up UDOM school of social science.
 
Halima mdee big up,huyo Azan Zungu walisema anauza madawa ya kulevya leo ndo tumejuaa kweli na bangi anatumia,kama anasema wanafunzi wanatafuta umaarufu je Kawambwa na Pinda walipoahidi field hewa wao wanataka nini?
 
dah haya maisha!c juzi tu tena kwa mbwembwe tele mkatoka mbele na kumchangia Jk fomu ili agombee urais?leo kawasahau ndg zangu mmefukuzwa wengine hata nauli za kurudi makwenu hakuna!lol poleni bwana!shule na siasa weee kama maji na mafuta
 
Halima mdee big up,huyo Azan Zungu walisema anauza madawa ya kulevya leo ndo tumejuaa kweli na bangi anatumia,kama anasema wanafunzi wanatafuta umaarufu je Kawambwa na Pinda walipoahidi field hewa wao wanataka nini?
majambaz ccm achanana nao.
 
WANAFUNZI 400 wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) jana walipewa saa nne waondoke chuoni hapo kutokana na kukithiri kwa vurugu zilizokuwa wakizifanya. Uamuzi wa uongozi kukifunga chuo hicho na kuamuru wanafunzi kuondoka eneo la chuo, utawafanya wanafunzi hao kukosa masomo kwa kipindi kisichojulikana kuanzia jana. Makamu Mkuu wa UDOM, Profesa Idris Kikula, alisema jana kuwa, uamuzi wa kukifunga chuo hicho una lengo la kuepusha baadhi ya wanafunzi na majanga yanayoweza kujitokeza kutokana na baadhi yao kukaidi amri ya kusimamisha mgomo wao. “Tumefunga chuo na tumewapa muda wa saa nne wawe wameondoka chuoni hapa kuanzia saa tatu asubuhi,” alisema Profesa Kikula.

Akifafanua juu ya uamuzi huo, Makamu Mkuu huyo wa Chuo, alisema wanafunzi wa mwaka wa pili na wa tatu ambao wanachukua kozi ya Sayansi ya Jamii, waliitisha mgomo tangu Jumatatu kwa lengo la kuilazimisha Serikali kuwapa posho za mazoezi kwa vitendo. “Uongozi wa Chuo umeshangazwa na hatua hii, kwani suala hilo lilishajadiliwa tangu Desemba mwaka jana na kupatiwa ufumbuzi kuwa Serikali itatoa posho hizo kwa muda muafaka na mimi niliongea nao wakakubali kuwa hakuna haja ya kufanya mgomo,” alisema. Profesa Kikula alifafanua kuwa wanafunzi wanatakiwa waende kwenye mafunzo kwa vitendo katikati ya mwezi ujao, hivyo kwa sasa ni mapema kuilazimisha Serikali kuwapa posho hizo.

Alisema kutokana na uamuzi wa wanafunzi kuandamana kinyume cha sheria Jumatatu hadi kwenye majengo ya Bunge, baadhi yao walikamatwa na uongozi wa chuo ulikubaliana kuwapa barua za kuwasimamisha masomo wanafunzi 400 ambao walishiriki maandamano hayo. “Habari za kusimamisha wanafunzi hao 400 zilisababisha taharuki miongoni mwa wenzao wakaanza kushambulia kwa mawe magari ya chuo na kuwapiga wanafunzi wengine ambao walionekana hawaungi mkono,” alisema. Katika hatua nyingine, Profesa Kikula alisema kuanzia leo, uongozi wa chuo utachapisha katika tovuti yake majina ya awamu ya kwanza ya ambao watatakiwa kurudi chuoni. “Kuna wanafunzi wengi tumewasimamisha, lakini hawana hatia, na baadhi yao walisaini makubaliano kuwa hawatashiriki mgomo, lakini hatukuwa na namna zaidi ya kuwasimamisha wote kutokana na hali ilivyokuwa,” alisema.

Baadhi ya wanafunzi ambao walizungumza na gazeti hili muda mfupi kabla ya kuondoka chuoni hapo, walilaani uamuzi huo na kutaka uongozi uwarudishe haraka masomoni. “Si haki kutoa adhabu hii kwa watu wote; viongozi wa mgomo wanajulikana, ni vyema uongozi wa chuo ungechukua hatua za kinidhamu dhidi yao,” alisema mwanafunzi ambaye hakutaka jina lake litajwe gazetini. Wanafunzi hao walikuwa wakidai kuwa walipewa ahadi tangu Februari ya kulipwa posho hizo Juni 7, lakini haikutekelezwa.

Rais wa Wanafunzi wa Chuo cha Sanaa na Lugha, Mwakibinga Phillipo, alisema chuo hicho kimefungwa kutokana na wanafunzi wake kushiriki maandamano juzi wakishinikiza wanafunzi wenzao waliosimamishwa chuo kurudishwa bila masharti. Philipo alisema, wanafunzi 374 wanasomea Uhusiano wa Kimataifa mwaka wa pili, na wengine 59 ni wa Kitivo cha Sayansi ya Jamii na ndio walisimamishwa juzi na kusababisha wenzao kuandamana wakiwatetea. Alisema, katika maandamano yao ya mwanzoni mwa wiki kupitia viwanja vya Nyerere hadi vya Bunge walikokutana na ulinzi mkali wa Polisi, wanafunzi 71 walikamatwa na na kuachiwa kwa dhamana iliyotolewa na Makamu Mkuu wa Chuo.

Habari Leo
 
jana baadhi ya wanafunzi wa Udom wamefunga chuo kwa mda usiojulikana na wengine kati yao kufukuzwa wakati wakidai madai yao ya msing ikiwemo pesa ya posho ya mafunzo kwa vitendo. Siku c nyng sana pia nlpata habari kuwa wanafunzi wa chuo hchohcho wa school ya informatics walifukuzwa nao kwa mda usio julikana. Sasa swal lang n je kufukuzwa kwa wasomi hawa n mkonn mrefu wa serikal ndio unaosababsha haya au n uongoy wa chuo wenyewe! Na je wanazan kwa kuwafkuza bila kutatua hoja yao ya msing ndio suluhsho?
 
Wanafunzi 9,000 Udom watimuliwa
ZAIDI ya wanafunzi 9,000 wa Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom) wamefukuzwa kwa muda usiojulikana kuanzia jana kwa madai ya kuhamasisha mgomo usio halali.Habari zilizopatikana mjini hapa zimeeleza kuwa wanafunzi hao ni wa Kitivo cha Sayansi ya Jamii na Sayansi Asilia. Walitakiwa kuondoka chuoni hapo kabla ya saa 8:00 mchana.

Baada ya amri hiyo, Polisi wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) walionekana wakiwa wanarandaranda katika maeneo ya chuo hicho.hali hiyo ilichangia pia kuharakisha wanafunzi hao kuondoka chuoni hapo wakihofia kukumbana na kipigo.

Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Idriss Kikula alithibitisha kufukuzwa kwa wanachuo hao na kusema kuwa suala la kuwarejesha litatokana na utaratibu watakaoupanga baadaye.

Kufukuzwa huko kumekuja siku mbili baada ya kuanzisha maandamano yaliyoshinikiza kujiuzulu kwa viongozi waandamizi wa Serikali, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Waziri wa Mambo ya Ndani, Shamsi Vuai Nahodha na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa kwa madai kwamba wamewadanganya kuhusu malipo yao ya masomo kwa vitendo.

“Ni kweli kabisa kuwa tumewasimamisha kwa muda usiojulikana. Tutawarudisha kwa muda ambao tutaona unafaa,” alisema Profesa Kikula na kuongeza mtindo utakaotumika ni wa kuchambua na kurudisha mwanafunzi mmoja mmoja.

Katika madai yao, wanafunzi hao walisema wanasoma bila ya kufanya mazoezi ya vitendo kama ilivyo kwa vyuo vingine.Madai mengine ni pamoja na mazingira mabovu chuoni hapo pamoja na kutosoma baadhi ya masomo ambayo wanachuo wengine wanasoma.

Msimamo wa wanafunzi
Wakizungumza mara baada ya agizo hilo jana baadhi ya wanafunzi hao walisema kuwa hawaoni tabu kufukuzwa wakisema wao ni waathirika wanaotumika kwa maslahi ya wengine.

Walisema kuwa kufukuzwa kwao ni kwa ajili ya kudai maslahi ambayo wamekuwa wakiyatafuta wakati wote bila ya mafanikio na kwamba kama itabidi itakuwa bora waondoke.

“Sisi tunaondoka na wenzetu wengine walishaondoka katika Kitivo cha Sayansi ya Kompyuta kwa hiyo kwa hali hii lazima chuo chote kitafungwa maana hali inakokwenda chuoni hapa ni siasa tupu,” alisema mmoja wa wanafunzi hao na kuongeza:

“Ni bora turudi nyumbani kwa kuwa huwezi kusoma bila ya kufanya mafunzo kwa vitendo. Ni bora tukae nyumbani tu,” alisema mmoja wa wanafunzi hao huku akiungwa mkono na wenzake.

Wanafunzi wa Kitivo cha Teknolojia ya Habari na Elimu Angavu walifukuzwa baada ya kugoma wakitaka walipwe fedha kwa ajili ya vifaa vya kujivunzia kwa vitendo.

Kufukuzwa kwa wanafunzi hao kulikuwa faraja kwa madereva wa teksi na pikipiki maarufu kama bodaboda ambao walifurika chuoni hapo kufanya kazi ya kuwasafirisha kwa malipo ya Sh10,000 kwa pikipiki na teksi Sh15,000

Source: Mwananchi
 
Serikali mbovu ya CCM wanashindwa kucontrol mambo madogo kama haya, ila bungeni mnalipana mabilioni ya hela na vijana wapo mtaani wanateseka kama hivi,mazafanta kabisa,hivi jamani hatuwaonei huruma vijana hawa na wenyewe wanatafuta maisha kwa ajili ya familia zao na watoto zao hapo baadae????
 
ZAIDI ya wanafunzi 9,000 wa Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom) wamefukuzwa kwa muda usiojulikana kuanzia jana kwa madai ya kuhamasisha mgomo usio halali.Habari zilizopatikana mjini hapa zimeeleza kuwa wanafunzi hao ni wa Kitivo cha Sayansi ya Jamii na Sayansi Asilia. Walitakiwa kuondoka chuoni hapo kabla ya saa 8:00 mchana.

Baada ya amri hiyo, Polisi wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) walionekana wakiwa wanarandaranda katika maeneo ya chuo hicho.hali hiyo ilichangia pia kuharakisha wanafunzi hao kuondoka chuoni hapo wakihofia kukumbana na kipigo.

Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Idriss Kikula alithibitisha kufukuzwa kwa wanachuo hao na kusema kuwa suala la kuwarejesha litatokana na utaratibu watakaoupanga baadaye.

Kufukuzwa huko kumekuja siku mbili baada ya kuanzisha maandamano yaliyoshinikiza kujiuzulu kwa viongozi waandamizi wa Serikali, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Waziri wa Mambo ya Ndani, Shamsi Vuai Nahodha na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa kwa madai kwamba wamewadanganya kuhusu malipo yao ya masomo kwa vitendo.

“Ni kweli kabisa kuwa tumewasimamisha kwa muda usiojulikana. Tutawarudisha kwa muda ambao tutaona unafaa,” alisema Profesa Kikula na kuongeza mtindo utakaotumika ni wa kuchambua na kurudisha mwanafunzi mmoja mmoja.

Katika madai yao, wanafunzi hao walisema wanasoma bila ya kufanya mazoezi ya vitendo kama ilivyo kwa vyuo vingine.Madai mengine ni pamoja na mazingira mabovu chuoni hapo pamoja na kutosoma baadhi ya masomo ambayo wanachuo wengine wanasoma.

Msimamo wa wanafunzi
Wakizungumza mara baada ya agizo hilo jana baadhi ya wanafunzi hao walisema kuwa hawaoni tabu kufukuzwa wakisema wao ni waathirika wanaotumika kwa maslahi ya wengine.

Walisema kuwa kufukuzwa kwao ni kwa ajili ya kudai maslahi ambayo wamekuwa wakiyatafuta wakati wote bila ya mafanikio na kwamba kama itabidi itakuwa bora waondoke.

“Sisi tunaondoka na wenzetu wengine walishaondoka katika Kitivo cha Sayansi ya Kompyuta kwa hiyo kwa hali hii lazima chuo chote kitafungwa maana hali inakokwenda chuoni hapa ni siasa tupu,” alisema mmoja wa wanafunzi hao na kuongeza:

“Ni bora turudi nyumbani kwa kuwa huwezi kusoma bila ya kufanya mafunzo kwa vitendo. Ni bora tukae nyumbani tu,” alisema mmoja wa wanafunzi hao huku akiungwa mkono na wenzake.

Wanafunzi wa Kitivo cha Teknolojia ya Habari na Elimu Angavu walifukuzwa baada ya kugoma wakitaka walipwe fedha kwa ajili ya vifaa vya kujivunzia kwa vitendo.

Kufukuzwa kwa wanafunzi hao kulikuwa faraja kwa madereva wa teksi na pikipiki maarufu kama bodaboda ambao walifurika chuoni hapo kufanya kazi ya kuwasafirisha kwa malipo ya Sh10,000 kwa pikipiki na teksi Sh15,000.

domu.jpg

Wanafunzi wa Chuo cha Sanaa ya Lugha na Sayansi ya Jamii cha Chuo Kikuu cha Dodoma wakiwa katika pilika za kuhamisha mizigo baada ya uongozi wa chuo hicho kuwatimua jana. Wanafunzi hao walifukuzwa baada ya kuendelea na mgomo.
 
Sometimes students don't need these kinds of disturbances from the Administration, lakini kwa sababu kila kitu kinachukuliwa kama siasa wanafunzi hawa hawawezi kusoma tena! wanatimuliwa.
 
hapana kikula hajashindwa kuongoza. Tatizo wanasiasa wanatumia udom kujiongezea umaarufu. Mfano, juzi wazir wa elimu alitangaza kwenye vyombo vya habari kuwa amefanya mazungumzo na uongozi na kwamba suluhisho limepatikana na mgomo umekwisha. Lakini cha ajabu ni kwamba watu wametimuliwa wakati yeye kadai mgomo umekwisha. What a shame! Hali hyo imesababisha hata baadhi ya vyombo vya habari (TV) kushindwa kuripoti habari ya kufungwa kwa chuo wakati waziri alitamba kuwa mambo shwari. MI ningekua jk ningempi
 
The hell is being done by helsb not other wise cause it is not transparent,so far ,no follow up taken by coresponding minister as far as concerned.politics is impotant every where no awarenes without politics no respect wizout politics.
 
Mawaziri hawa wajiuzuru kwa kuudanganya umma. Hata hivyo mgt ya chuo iko kisiasa nayo haifai. Tunataka nchi iongozwe kitaalamu na si kisanii. Vinginevyo watawala wajue tumechoka.
 
tatizo siasa hadi katika elimu,wanategemea wataaluma wa ukweli watatoka wapi wakati wanatoa elimu ambayo haikidhi viwango.kwanza hata wao hawana aibu mana enzi zao wao wamepata elimu bora kabisa ila sisi hata hawatujali wanaona sifa kuwa na vyuo na shule nyingi bila ya kutoa elimu bora. Afadhali wasomeshe watu wachache lakini watoe elimu bora ambayo itatoa watu wenye tija katika taifa letu.
 
Back
Top Bottom