Hatimaye wanafunzi wa kitanzania nchini msumbiji wahamishia makazi ubalozni nchini msumbiji

Nahami

New Member
Sep 8, 2011
3
0
Hatimaye sitofahamu inayo endelea kati ya WANAFUNZI na UBALOZI na SERIKALI kwa ujumla nchini msumbiji,wanafunzi hao waliamua kuhamishia makazi yaoubalozi wa Tz uliopo katikati ya jiji la maputonchin msumbiji, Wanafunzi hao wanadai mpaka sasa hawajajibiwa wala kutoa tamko lolote la kimaandishi toka wizara ya elimu ama bodi ya mikopo.Wanafunzi hao huku wakiwa na nyuso za hasira walidai kwamba wamechoka na ubabaishaji wa baadhi ya watendaji wa serikari na kwamba wanaomba waonane na waziri wa elimu na mkurugenzi wa bodi, wanafunzi hao walizi kuongeza kwamba pale hotelini walipo fikia wamefukuzwa na hawana pa kwenda zaidi ya hapo ubalozin.Wana JF jamani tuwasaidie wanafunzi hawa kwani wanadai kwamba hawana hata senti tano na bodi imewaambia hawatatumiwa hela zao kwani zimelipwa ktk deni la hapo wanapo kaa hotelini,jambo la kushangaza kama wamelipa kwanini wafukuzwe? inaonekana wazi hapo katikati kunamambo ya ubabaishaji. Jamani tuliangilie jambo hili kwa jicho pevu kwani wadogo zetu wanapata taabu
 
duh kumbe hadi wanaosoma ng`ambo nao wanafanyiwa kama sisi? hao kama vpi waanzishe maandamano ya kwenda ikulu ili serikali yetu iwajibike mapema ipasavyo.
 
Back
Top Bottom