Hatimaye Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar wamepitisha bajeti ya wizara ya Ardhi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hatimaye Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar wamepitisha bajeti ya wizara ya Ardhi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Jul 12, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Jul 12, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  [​IMG]

  Na Juma Mohammed,MAELEZO Zanzibar Hatimaye Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar wamepitisha makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Ardhi, Makaazi,Maji na Nishati baada ya mjadala mkali wakati wa kuchangia bajeti hiyo.

  Wajumbe wengi waliochangia bajeti hiyo walitaka Serikali kutoa kauli kuhusu suala zima la mafuta na gesi asilia. Katika maelezo yake, Waziri wa Wizara hiyo, Ali Juma Shamuhuna amesisitiza msimamo wa SMZ kuyaondoa mafuta na gesi asilia katika orodha ya mambo ya Muungano. Katika majumuisho yake kwa Wajumbe wa Baraza , Waziri Shamuhuna alisema kwamba michango iliyotolewa na wajumbe itafanyiwa kazi ikiwa pamoja na kuahidi kutembelea maeneo mbalimbali yaliyoelezwa na wajumbe wakati wakichangia bajeti yake.

  Waziri Shamuhuna alisema matatizo ya maji yaliyoelezwa, Mamlaka ya Maji Zanzibar(ZAWA) itajitahidi kuyapatia ufumbuzi. Waziri huyo alisisitiza kwamba mara baada ya kumalizika kwa vikao vya Baraza la Wawakilishi atafanya ziara katika sehemu ambazo zinamatatizo ya maji. “Mheshimiwa Mwenyekiti, nimesema na ninaendelea kusema tena nikimaliza bajeti nitapita kwa wale wenye matatizo ya maji na transfoma nitakwenda na ikiwa uwezo upo tutayatatua” Alisema Waziri huyo. Akizungumzia suala la umeme, Waziri huyo alisema Serikali imejipanga katika kuisambaza nishati hiyo kwa wananchi wote wa Unguja na Pemba. Akifafanua hoja ya Mwakilishi wa Jimbo la Mkwajuni kuhusu kuvunjwa kwa Jengo la starehe club, Waziri Shamuhuna alisema jengo hilo halina daraja.

  Waziri Shamuhuna alisema “umekwenda Ufaransa halikutajwa kabisa, lililotajwa ni Mambo Msiige na tumepewa maelekezo” Alisema Jengo hilo halijaorodheshwa katika orodha ya Mji mkongwe na kwa hivyo halimo kwenye urithi wa ulimwengu unaotambuliwa na Shirika la Elimu,Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa(UNESCO). Awali, wakati wa asubuhi, Mwakilishi wa kuteuliwa na Rais Ali Mzee Ali aliapishwa kuwa Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi
  .
   
Loading...