Hatimaye waandamanaji Nigeria wafanikiwa kuivunja SARS

Guus

JF-Expert Member
Jul 16, 2013
1,131
823
Baada ya siku kadhaa za maandamano ya kutaka kuvunjwa kwa kilichokuwa Kikosi Maalumu cha Kuzuia Wizi (Special Anti-Robbery Squad maarufu kama SARS) nchini Nigeria, IGP wa Polisi jana Jumapili ametangaza rasmi kuvunjwa kwa kikosi hiko.

SARS, ambacho kilikuwa kitengo maalumu chini ya jeshi la polisi toka 1992, kwa muda mrefu kimekuwa kikilaumiwa kwa unyanyasaji, ukamataji pasipo kufuata sheria, utesaji na hata mauaji.

Maandamano ya sasa yakichagizwa na wasanii wakubwa wa muziki (kama anavyoonekana wizkid katika video), yalizuka baada ya video moja kusambaa ikiwaonesha askari wa SARS wakimpiga risasi hadi kumuua mwanamume mmoja katika jimbo la Delta ya Kusini.



1602497631541.png

 
Hayo yametangazwa na ofisi ya Polisi nchini humo.

Ujumbe wa ofisi hiyo kupitia mtandao twitter, unasema kuwa kikosi maalumu cha kukabiliana na waporaji kinachojulikana kama SARS kimevunjiliwa mbali mara moja.

20201012_100821.jpg
 
Unafuta Kimoja unaweka kingine kinachohitajika ni reform.. Ila Nigeria is ghetto kama Kenya tuu
 
Kusoma na kuelimika pia ndio kitu kikubwa kimewasaidia hawa Wanaigeria ,Wanaigeria wengi wasomi na wameelimika, Sasa wasanii wa Bongo kwa kweli tuwaache tuu waendelee kuvalishwa makofia ya kijani.
 
Kusoma na kuelimika pia ndio kitu kikubwa kimewasaidia hawa Wanaigeria ,Wanaigeria wengi wasomi na wameelimika, Sasa wasanii wa Bongo kwa kweli tuwaache tuu waendelee kuvalishwa makofia ya kijani.
Tatizo sio kuwa wasomi,tatizo ni kuwa pengine wana viongozi wasikivu zaidi wasio na misimamo ya kibabe.

Kiongozi akiwa mkorofi wewe uwe na digrii mia moja basi atawashinda tu kwa sababu ana dola.

Hivyo msisifie sana wasanii wakusifiwa hapo ni kiongozi.

Hata hapa tanzania kuna wasomi wengi sana ila tatizo liko pale pale..
..
 
Back
Top Bottom