Katika muda wa miezi michache iliyopita, ukitafuta maneno “Fort Detrick” kwa kutumia Google, hakuna chochote cha maana kilichoonekana, na hata baadhi ya watu katika nchi za magharibi, hasa Marekani kwenyewe wengi walikuwa hawajui kama Marekani ilikuwa na maabara ya virusi inayoitwa Fort Detrick, na kwamba maabara hiyo imeleta madhara makubwa kwa watu wengi, wanyama na hata mazingira.
Watu wenye akili wanajua kuwa kwenye dunia ya sasa ya uhuru wa habari kitu chochote kile, iwe ni kibaya au kizuri, kinaweza kupatikana kwenye mtandao wa internet. Kuna mambo mengi tu mabaya ya kutisha na haya kustahili kuwepo kwenye internet, lakini mambo hayo yapo. Kwa hiyo hali ya kutopatikana kwa habari yoyote kwenye internet kuhusu maabara ya Fort Detrick, ilifanya watu wenye akili watambue kuwa kuna jambo linafichwa kiasi kwamba hata mambo yanayohusu maabara hiyo yamefutwa au kuzuiwa kwenye internet.
Mwanzoni msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Zhao Lijian, mara kwa mara alionekana kuitaja maabara hiyo kila alipozungumzia suala la virusi vya Corona. Baadhi ya watu waliona kama ni mzushi, lakini sasa kile ambacho amekuwa akikisema kimeonekana kuwa na mantiki na kimeanza kuonekana kwenye vyombo vikubwa vya habari.
Wiki hii tovuti ya shirika la habari la Uingereza BBC, imeandika makala kuhusu maabara hiyo. Japo kuwa makala hiyo imejaa propaganda, lakini kuandikwa kwa habari hiyo ni hatua nzuri ya kufungua mjadala kuhusu hatari iliyoletwa na maabara hiyo kwa usalama wa afya ya binadamu. Mwandishi wa makala hiyo anaonekana kujua mambo mengi kuhusu makala hiyo, lakini ametumia maneno “historia yenye utata kuhusu maabara hiyo” bila kusema ni utata gani. Lakini kama nilivyosema mwanzo, wenye akili wakisoma hilo neno “utata” wanajua maana yake ni nini.
Ajabu ni kuwa makala hiyo pia imesema maabara hiyo ilikuwa inafanya utafiti kuhusu virusi vya Ebola na virusi vya ndui. Inashangaza kidogo kuona kuwa maabara iliyokuwepo tangu miaka ya 50, inatajwa kuwa ni maabara ya kutafiti virusi vilivyoibuka muda mrefu baada ya hapo na watu wengi mwaka 2014-2016 kwenye eneo la Afrika Magharibi. Na ugonjwa wa ndui uliotajwa kwenye makala hiyo pia ni ugonjwa ambao mwaka 1977 Shirika la Afya Duniani lilitangaza kuwa umetokomezwa.
Jambo linalotia moyo ni kuwa jambo hilo ambalo lilikuwa siri, sasa linaanza kujadiliwa na vyombo vikubwa vya habari ambayo vinaheshimika katika nchi za magharibi. Makala nyingine iliyoandikiwa na tovuti ya Politico ya Marekani, imeonekana kuvutia ufuatiliaji zaidi baada ya kueleza mambo ya kutisha yaliyofanywa kwenye maabara hiyo. Makala hiyo imesema kemikali za ajabu zilikuwa zikitengenezwa na kufanyiwa majaribio kwa wafungwa katika magereza ya Marekani, na nyingine hata kutumiwa na jeshi la Marekani kwenye uwanja wa vita, na kusababisha madhara makubwa ambayo hadi leo yanaendelea kutesa watu.
Makala hiyo imesema tafiti za ajabu kwenye maabara hiyo zilionekana kufanyiwa majaribio zaidi kwa wazungu maskini na wafungwa wenye asili ya Afrika, na barani Ulaya wafungwa walikuwa wakifanyiwa majaribio.
Kama makala ya tovuti ya politico ingetolewa kwenye tovuti ya China, basi habari hiyo ingepuuzwa au kutajwa kuwa ina malengo ya kisiasa. Jambo la kutia moyo kwa sasa ni kuwa mjadala umeanza kufuatiliwa polepole, na anachokitaja mara kwa mara msemaji wa wizara ya mambo ya nje kuwa kinatakiwa kupatiwa majibu, inaonekana kuwa ni kweli kinahitaji majibu.