Hatimaye! Unaweza kufanya malipo mtandaoni kwa M-Pesa

Wakubwa mi nimejaribu kutumia kwenye alliexpress inazingua tu daah, sjui niconnect tu na equity
 
Screenshot_20190724-122243.png


Hapo pa kujaza na Card holder na surname selewi nijaze nini please wajuzi
 
simamajuu,
Card yako ina jina gani? Maana yake weka jina ambalo likitumika kusajiri hiyo Card, kama unaitwa Masau bwire jaza kama umeazima kwa jirani weka jina lake
 
Yap, na mm ninanunua huko huko ebay ingawa delivery inachelewa sometimes.
Mkuu naomba nisaidie kidogo katika manunuzi pale unapotakiwa kuonyesha njia ya kupokelea mzigo mbona inalimit tu post adress badala hata ya dhl
 
Makato makubwa mnoooo. Ukifanya malipo ya 1M unakatwa karibu lak 2
BancABC kwa kushirikiana na MasterCard, wamezindua huduma mpya iitwayo M-Pesa-Mastercard ni ya kwanza na ya kipekee Tanzania itakayomuwezesha mteja wa M-Pesa kuweza kulipia huduma na bidhaa mitandaoni katika tovuti mbali mbali Duniani zinazopekea malipo kwa MasterCard. Kupata huduma hii ya Virtual Card piga *150*00# chagua lipa kwa M-Pesa, chagua M-Pesa MasterCard, kutengeneza kadi yako. Utapata Card Number, Expiration date pamoja na CVV Number ndani ya sekunde chache tu!

===
Kwa mtu yeyote aliyewahi kufanya manunuzi ya kitu chochote bila kuinuka kitini ama kutoka nyumbani kwake anaweza kuelezea urahisi na wepesi wa kufanya manunuzi mtandaoni, lakini hii imekuwa ni ndoto kwa Watanzania walio wengi, mpaka sasa ambapo Mastercard wameungana na Vodacom na BancABC kutengeneza kadi ya kwanza itakayowezesha manunuzi mtandaoni – M-Pesa Virtual Card.

“Huduma ya M-Pesa kutoka Vodacom ina wateja Zaidi ya milioni 8.2 huku ikiwa na Zaidi ya wakala laki moja waliotapakaa nchi nzima, hii inawezsha upatikanaji wa uhakika wa huduma za kifedha, lakini imekuwa ni ngumu pale linapokuja suala la kulipia manunuzi mtandaoni haswa kupitia tovuti za kimataifa. Uzinduzi na ufanyaji kazi wa Virtual Card kupitia M-Pesa utaleta mapinduzi katika kuwezesha Watanzania kufanya manunuzi mtandaoni na kuondosha vikwazo ikiwamo kuwa na akaunti ya benki na pia hatari ya mteja kuweka taarifa zake za kibenki mtandaoni,” alisema Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Plc Hisham Hendi.

Inategemewa kwamba uunganisho wa intaneti kwa bara la Afrika itaongezeka sana ikiwa ni matokeo ya upatikanaji wa simu janja (Smartphone) na pia ukuaji wa utoaji huduma yenye kasi zaidi ya intaneti kutoka kwa watoa huduma kama Vodacom. Ongezeko hili la upatikanaji wa huduma ya intaneti litaongeza uhitaji wa maudhui ya kidijitali, mitandao ya kijamii, M-Commerce, elimu ya mtandaoni na pia malipo mtandaoni kurahisishwa na kuongezewa usalama zaidi.

Kadi hii itawawezesha wateja wa M-Pesa kufanya malipo ya aina yeyote kwa tovuti za kimataifa au za hapa nyumbani, ama kwa kutumia zana (App) yeyote ambayo inatumia na Mastercard kwa malipo, bila kuhitajika kuwa na akaunti ya benki au kadi ya mkopo (Credit Card). Wateja wanaweza kutengeneza virtual card kupitia menyu ya M-Pesa ama kupitia App yetu ya M-Pesa (huduma hii tutaiongeza hivi karibuni) na kuijaza pesa kupitia mfumo wetu wa M-Pesa. Kadi hii inakuwa tayari kwa matumizi mara tu baada ya kujazwa pesa.


Kaimu Mkurugenzi wa Vodacom Tanzania, Hisham Hendi (Kati), Raisi wa Kusini mwa Sahara wa Mastercard, Raghay Prasad (kushoto) na Mkuu wa hazina na kitengo cha soko la kimataifa wa Banki ABC, Barton Mwasamengo (kulia) wakionesha ushirikiano kati ya M-Pesa na Mastercard uliozinduliwa jana jijini Dar es Salaam.

Chanzo: Michuzi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom