Hatimaye uasi waanza kuzaa matunda rasmi ndani ya CCM

Sitachoka

JF-Expert Member
Nov 17, 2011
3,030
1,303
Mwalimu Nyerere alitabiri kuwa ili chama hiki kiweze kuanguka ni lazima kitagawanyika. Mkutano wa juzi umedhihirisha hilo; kwanza hata wale waliobebwa kuja mkutanoni, walikuja kwa imani juu ya 'waasi'
kwamba pengine tumaini limerejea! Nani anabisha kuwa Dr. Pombe Magufuli si muasi dhidi ya taratibu na mazoea mabovu yaliyozoeleka katika serikali ya CCM; nani anabisha kuwa Nape Nnauye si mmoja ya waasi aliyekana dhulma ndani ya UVCCM kiasi cha kutolewa kafara, lakini nani anabisha kuwa huyu si
mmoja ya waliotajwa kutaka kujiengua CCM kuanzisha CCJ.

Nani anakataa kuwa Stephen Wasira hakuwa muasi aliyeondoka ndani ya CCM miaka ile na kuwa mmoja wa waasisi wa mageuzi kwa kujiunga na NCCR- Mageuzi na hata akashinda uchaguzi mwaka 1995. Nani
anabisha kwamba Dr. Mwakyembe hakuasi dhidi ya chama na serikali kiasi cha kuongoza mashambulizi
yaliiangusha serikali mwaka 2008 na baadaye kujiunda katika kundi la mitume 12 walizunguka nchi
nzima kwa hoja dhidi ya ufisadi. Hebu niambieni si ni huyu bwana licha ya koswa koswa zote alizopitia bado ameendelea kutikisa serikali na chama kiasi cha hata 'wao' kuona kumuacha nje ni hatari kuliko akiwa ndani!

Tuliambiwa alikuwa mmoja wa walianzisha chama cha CCJ. Leo waasi wamekisimamisha chama na kukiokoa na aibu ya zomea zomea pale wa "swaumu" a.k.a glory temple. Unaweza kuona jinsi wanavyojisifu kuwa waliweza kujaza watu wengi, swali linakuja, ni nani alijaza watu jangwani, ni hawa waasi au kukubalika kwa chama dume!
 
Hata hao waasi hawakujaza watu ni yale malori ndo yalifanya watu wajae pamoja na elfu tano posho, pia tshirt, kofia, kanga na vilemba vya bure pia chege na diamond na anaesubiria ubunge wa mezani bwana marlaw! In short at least watu walienda kwa hayo tu ila kama ingekuwa ukifika pale then upige kura ndipo ingedhihirika kuwa hata nusu ya wale walioenda na nguo za bure wasingechagua chama chao pamoja na posho!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom