Hatimaye uandikishaji umefikia hatua ya nyumba kwa nyumba

Kingjr2

JF-Expert Member
Sep 8, 2018
644
1,271
Tunapoendelea na kumbukizi ya miaka 20 ya kifo cha Baba wa Taifa, huko Morogoro mjini tunaarifiwa kwamba wajumbe wa serikali za mtaa wanapita nyumba kwa nyumba kuorodhesha watu wote wenye umri wa kupiga kura, kuanzia miaka 18 na kuendelea

Hii ni confirmed information kutoka kwa wahusika wenyewe (wajumbe), Wamepewa maelekezo kuorodhesha wakaazi wote halafu baadae kufanya ulinganifu, nani kajiandikisha na nani hajajiandikisha.

Najiuliza tu wanalenga nini? Kwamba wakikuta kwenye orodha hayumo wanamuongezea jina lake au wanamchukulia hatua za kutojiandikisha!!?

Tupeni update huko kwenye mitaa yenu mambo yakoje, Morogoro kwa baadhi ya mitaa kinachoendelea ni hicho
 
Inamaana siku ya kupiga kula watapita tena mtaani mbona mambo ya ajabu haya
 
Tunapoendelea na kumbukizi ya miaka 20 ya kifo cha Baba wa Taifa, huko Morogoro mjini tunaarifiwa kwamba wajumbe wa serikali za mtaa wanapita nyumba kwa nyumba kuorodhesha watu wote wenye umri wa kupiga kura, kuanzia miaka 18 na kuendelea

Hii ni confirmed information kutoka kwa wahusika wenyewe (wajumbe), Wamepewa maelekezo kuorodhesha wakaazi wote halafu baadae kufanya ulinganifu, nani kajiandikisha na nani hajajiandikisha.

Najiuliza tu wanalenga nini? Kwamba wakikuta kwenye orodha hayumo wanamuongezea jina lake au wanamchukulia hatua za kutojiandikisha!!?

Tupeni update huko kwenye mitaa yenu mambo yakoje, Morogoro kwa baadhi ya mitaa kinachoendelea ni hicho
Hta huku kishapu mwendo ni huo.
 
Ni jambo jema, mikoa mingine waige!

Natamani waje kwangu ili niwape ukweli wao, tena nitatumia lugha ya kiungwana kabisa na mifano halisi ninayo. Kwenye hili umma usiogope lolote maana hamna kosa lolote kutokupiga kura hasa kutokupiga ukiwa na sababu zenye mashiko na ushahidi juu. Iwapo umma utaogopa kuwapa ukweli wao sisi kama taifa tutaendelea kuchezewa na wanasiasa, na hili hata viongozi wa upinzani tumewaambia kabisa kupiga kura ni kushiriki dhambi mbaya ya demokrasia.
 
Back
Top Bottom