VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,136
- 17,871
Imeripotiwa na kuthibitishwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Uyui mkoani Tabora Ndugu Gabriel Mnyele ameachia ngazi/amejiuzulu. Mwanasheria mbobezi Mnyele ameandika barua ya kujiuzulu nafasi yake hiyo kwa hiyari yake mwenyewe.
Ingawa hakukuwekwa wazi sbabu ya kujiuzulu kwake, wachambuzi wa mambo ya kisiasa nchini wanamuona Mnyele kama mtu aliyejitoa 'kusema kwa vitendo' kutoridhishwa na maelekezo na makatazo ya kikazi. Ameamua kuitendea nafsi yake.
Aliyewahi kuwa Waziri wa Nishati na Madini na Mbunge wa Kibaha, wakati akijiuzulu Bungeni Dodoma mwaka 2008, Dr. Ibrahim Msabaha aliwahi kutupa msamiati wa kabila lake la wazaramo: CHILONGOLA. Alimaanisha mtu anayeongoza njia/kiongozi wa msafara kutoka sehemu moja hadi nyingine.
Mnyele, kwa wale wanaolalamika ndanindani, amekuwa CHILONGOLA wao. Wangapi watamfuata na kutetea wanachokiamini? Wangapi wapo tayari kupoteza ukuu wa Mkoa,Wilaya na kadhalika na 'saluti' walizonazo? Tusubiri kuona.
Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam