Hatimaye Tout Puissant Mazembe 'Englebert' Yaleta Faraja Kwa Yanga

kovai tamil taiga

JF-Expert Member
Sep 28, 2013
1,045
1,425
Pamoja na Kusukumizwa Nje Ya Mashindano ya CL Ya CAF na kubakia Kuwa 'Wapenzi Watazamaji' huku ikiziacha timu Za Azam, Biashara na Simba zikiendelea kwa hatua inayofuata. Mashabiki na Wapenzi Wa Yanga wameonekana maeneo mbalimbali Ya nchi Wakisherehekea Ushindi walioupata TP Mazembe leo dhidi Ya Simba kwa Mkapa.

Ushindi huo umewakosha na kuwasahaulisha kabisa kuwa Inawabidi kusubiri tena mpaka 2022 Panapo majaaliwa Kushiriki tena michuano Ya CAF.

Pole nyingi ziende sio tu Kwa Yanga bali Kwa Bw. Damas Ndumbalo kwa Usumbufu Uliojitokeza Kutia Saini mkataba Wa 'Visit Kilimanjaro na Zanzibar' ilhali timu hiyo ikiwa haina uwezo wa Kuutendea haki Mkataba huo...!

Salute Kwao Bana Kongo Mazembe Kwa Faraja hii Kwa Yanga.
 
Hakuna Usawa hapo usijitoe akili.
Matokeo haya Yanawafanya Azam,Biashara na Simba Waongee lugha moja..! Mfano Nauli za ndege Kimataifa zikipanda zitawaathiri vipi?
Sasa Yanga watakuwa wanadiscuss 'Kimbinyiko Wakipandisha nauli Itakuaje? Au bei Ya wese ikipanda tufanyeje?
 
Pamoja na Kusukumizwa Nje Ya Mashindano ya CL Ya CAF na kubakia Kuwa 'Wapenzi Watazamaji' , huku ikiziacha timu Za Azam, Biashara na Simba zikiendelea kwa hatua inayofuata...
Mkuu, upo sahihi! Mi nipo Isaka Kahama Shinyanga. Lile goli walilofungwa Simba, lilishangiliwa sana, pale ukumbini nilipokuwa, na wale waliokuwa na huzuni dakika chache baada ya taarifa kuwa Yanga wameshafungwa. Ni kweli hayo matokeo yamewapa FARAJA YA MUDA!
 
Timu zilinazocheza mashindano ya kimataifa Tanzania.

Simba Sports Club
Azam football club
Biashara footbal club

Habari za michezo kwa sasa ni kuhusu hizi timu tatu.
Tuachane na Makelele fc
 
Zilongwa mbali zitendwa mbali maneno ya mzaramo, we rudi nyumbani ukate vitunguu subiri mwanaume akubebe tena mwakani.
Ngao ya jamii Tareh 25/9/2021. Mjiandae kisaikolojia na msimu huu Yanga kajipanga kweli kweli kwenye mashindano ya Ndani wachezaji wote wa kimataifa watakuwepo.

Tofauti na ilivyokuwa kwenye mechi ya Zanaco au za kimaifa kwa baadhi ya wachezaji wa Yanga kutocheza.Kazi ipo kwenye ligi Nyama pori mjiandae kisaikolojia mtaliwa Supu
 
Ngao ya jamii Tareh 25/9/2021.Mjiandae kisaikolojia na msimu huu Yanga kajipanga kweli kweli kwenye mashindano ya Ndani wachezaji wote wa kimataifa watakuwepo.Tofauti na ilivyokuwa kwenye mechi ya Zanaco au za kimaifa kwa baadhi ya wachezaji wa Yanga kutocheza.Kazi ipo kwenye ligi Nyama pori mjiandae kisaikolojia mtaliwa Supu

Ni mwaka wa nne mfululizo,maneno ni yale yale,hakuna jipya,tulishawazoea
 
Sasa ni muda wa kubadilisha hii slogan maana tumeichoka mwaka wa nne sasa maneno ni yale yale
Ngao ya jamii Tareh 25/9/2021.Mjiandae kisaikolojia na msimu huu Yanga kajipanga kweli kweli kwenye mashindano ya Ndani wachezaji wote wa kimataifa watakuwepo.Tofauti na ilivyokuwa kwenye mechi ya Zanaco au za kimaifa kwa baadhi ya wachezaji wa Yanga kutocheza.Kazi ipo kwenye ligi Nyama pori mjiandae kisaikolojia mtaliwa Supu
 
Back
Top Bottom