Hatimaye Starz Yarejea Toka Morocco

Amavubi

JF-Expert Member
Dec 9, 2010
30,140
13,215
1.jpg
Wachezaji wa Yanga, Toka Kushoto Canavaro, Kiemba (mpya 2013/14) na Chuji
 
4.jpg
Vicent Barnabas naye hana raha kwani alipogwa benchi la ufundi, Kapombe anakula posho yake ya Buku 5
 
5.jpg
Bartez anatamani hata asipande hilo basi, kwa Juma atasubiri sana
 
6.jpg
Kama uli note, Ulimwengu hakufurahia kabisa kutolewa mapema......hapa hana raha kabisa...........
 
3.jpg
SAMAATTATTAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAA, mizigo yote yako? oohhhhpps mingine umetoka nayo Cpngo DR, zawadi kwa ndugu
 
Kocha wa Timu bali matokeo ya Taifa(Taifa Stars), Kim Poulsen amesema refa wa mechi ya Taifa Stars na Moroccoiliyopigwa Marrakech Jumamosi kusaka tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Dunia Brazil mwakani aliuwa mchezo kwa kutoakadi nyekundu kwa mchezaji Aggrey Morris.
Akitoa maoni ya mchezo huo, Poulsenalisema alisikitishwa na jinsi refa huyo alitoa adhabu kali ambayo haiendani nakanuni za FIFA.
Aggrey Morris alioneshwa kadi nyekundubaada ya kugongana na Abderazak Hemed Allah ambaye aliifungia Morocco bao la kwanza katikadakika ya 37.
"Hakuwa nasababu ya kumuonesha Morris kadi nyekundu kwani tayari alishawapa Moroccopenalti, alisema Poulsen huku akiongeza, "FIFA imeshawaonya marefa mara kadhaadhidi ya kuua mchezo kwa namna hii ya kutoa adhabu kali kupita kiasi."
Poulsenalisifu wachezaji wake na kusema licha ya kucheza pungufu walipambana uwanjanina kufanikiwa kupata bao kupitia kwa Amri Kiemba. Morocco walishinda kwa 2-1.
"Kamatungecheza kumi na moja hadi mwisho nina uhakika tungeshinda mechi hii lakinirefa aliiua mechi na huwezi kufanya hivi katika mechi ngumu kama hii," alisemaPoulsen.
Kocha huyoalisema kupata goli la ugenini unapochez na timu ngumu kama Morocco ni jambo lakujivunia hasa mnapokuwa pungufu uwanjani.
Alisisitizakuwa sasa wanaelekeza nguvu zote katika mechi shidi ya Ivory Coast Jumapiliijayo. "Mambo ya Morocco yamekwisha sasa tunafikiria namna ya kushinda mechi yaJumapili.
Tanzaniaiko katika kundi C inayoongozwa na Ivory Coast yenye pointi 10, Tanzania 6,Morocco 5 na Gambia 1.
Taifa Starsimerejea Jumatatu alfajiri kutokea Marrakech Morocco na itaendelea na kambi yawiki moja ili kujiandaa na mechi dhidi ya Ivory Coast.
Nahodha waTaifa Stars, Juma Kaseja alisema wachezaji walicheza kwa ari kubwa nawalifurahishwa na jinsi watanzania walijitokeza kwa wingi.
"Tulipatafaraja kubwa sana kuwaona watanzania wengi uwanjani…mambo ya Morocco yameishasasa tuangalie Ivory Coast," alisema.
Meneja waBia ya Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe ambaye bia yake inadhaminiTaifa Stars, alisema wacezaji walijitahidi hasa ikizingatiwa walicheza pungufuna hata wakafanikiwa kufunga bao moja.
"Katikahali kawaida, wachezaji wengine wangekata tamaa lakini bao hili moja linaoneshakuwa wachezaji walikuwa na ari ya kupata ushindi," alisema Bw Kavishe.
Alisema waokama wadhamini wana imani kubwa na Taifa Stars na kwamba wanaamini hii nisafari ya mafanikio ambayo ilianza mwaka mmoja uliopita tangu Bia yaKilimanjaro Premium Lager ianze udhamini huo.
 
Back
Top Bottom