Hatimaye sasa ni rasmi kuwa Mkuu wa Mkoa wa DSM Makonda amempata ‘ Mbabe ‘ wake ambaye ni Katibu Mkuu CCM Bashiru

MINOCYCLINE

JF-Expert Member
Apr 2, 2015
8,011
16,748
Kama kuna vitu ambavyo sikuwahi Kutegemea kuja Kuviona kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda ni kuwa Mpole mbele ya Katibu Mkuu wa CCM Dkt. Bashiru Ally Kakurwa huku akiwa ni Mtiifu Kwake isivyo kawaida yake na kuamini kuwa kumbe kila Binadamu huwa na Mbabe wake ambaye hata afanyeje huwa hakurupuki Kwake.

Katika hali isiyo ya kawaida Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kwa Kinywa chake huku akinukuliwa amesikika akisema kuwa amekubali Mapungufu yake ambayo mara kwa mara yamekuwa yakisemwa na Katibu Mkuu wake ( CCM ) Bashiru Ally na kwamba yupo tayari kubadilika na yote aliyoambiwa nae atayafanyia Kazi.

Ili kuonyesha kuwa Katibu Mkuu CCM Dkt. Bashiru Ally hatanii na wala hamwogopi Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ambaye anaogopwa na karibia 95% ya Viongozi Wakuu wa Serikali hii kuanzia na Namba Mbili ( Mwanamama ) na Namba Tatu ( Ukanda wa Korosho ) jana alipokuwa akifanya Ziara Kinondoni / Kawe hasa pale Ukumbini Mbezi Beach alimwambia kuwa anasikia kuwa anajiandaa Kugombea Jimbo la Kawe ila akamwambia wazi wazi kuwa bado Makonda hatoshei / hatoshi kuwa Mbunge wa Kawe na badala yake aendelee tu kuwa Mkuu wa Mkoa.

Na habari ambazo zimenifikia tena hivi punde tu zinasema kuwa na leo tena wakati Katibu Mkuu wa CCM akiwa Ziarani mahala ( Mwembechai BRT Station ) kama kawaida yake amempa za Uso / Makavu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam hasa juu ya Mienendo yake na Kumtaka abadilike upesi na nasikia Makonda alikuwa Mpole hadi kutaka Kuingia chini ya Meza ila sema tu Itifaki ilimzuia.

Pole sana Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kwani safari hii ama hakika umepata ‘ Mbabe ‘ wako Katibu Mkuu wa CCM Dkt. Bashiru Ally. Nina uhakika kuwa kwa 99% Wateule wengine wa Serikali hii ya Tano huko waliko sasa wanafurahi mno jinsi Katibu Mkuu CCM Bashiru anavyowanyooshea Mtu ambaye Wao wanamuogopa na huku wengine wakiwa wamepatwa na ' matatizo ' baada ya ama Kumgusa au kutompa Ushirikiano ambapo nae ( RC Makonda ) aliwasemea kwa Baba yake Kipenzi ambaye ndiyo amekuwa akimpa Kiburi.

Kuna Mtu mmoja ( Muhimu ) ndani ya Taasisi fulani ( Muhimu ) nayo ndani ya Ardhi hii ya Tanzania aliwahi Kunidokeza kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Makonda ameshaanza Kuchokwa na aliyekuwa akimpa Kiburi hivyo sasa amepandikiziwa Mtu ambaye ana Ushawishi mkubwa Kisiasa ( hasa kwa dhamana ya Kichama ) na ambaye anasikilizwa kuliko Yeye ili ammalize au amtulize Moto wake nikamkatalia kata kata ila kwa mwendo huu wa Dkt. Bashiru Ally sasa nawiwa kusema kuwa taratibu ule ' Mvumo ' uliokuwa na Kishindo wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda unaanza Kudhibitiwa na Siku si nyingi ' Umaarufu ' wake utapungua na natabiri huenda kuna Jambo asilolitegemea la Kisiasa litakuja Kumtokea ama mwaka huu au hata mwakani.

 
Kwa sasa Makonda hawezi kuingia kwenye mgogoro na Bashiru ile hali 2020 kazi inaanza na yeye anatafuta pa kwenda. Hivyo ni ngumu kuingia kwenye mgogoro na benchi la ufundi.

Subiri akipata namba 2020 na huyo AB ataona cha mtema kuni.
 
Hizo kweli za uso! Makonda hadi kanywea utadhani watendaji wa kata wale anaowatukana kila siku.
Nashangaa hapo kashindwa kusema "usione tunafanana mashati lakini nakuzidi sana tuu, hivyo jichunge"
Au "katika watu wanakula laha nadhani mie naongoza"
 
Mtukufu anajisikia vibaya jinsi Bashite anavyofanya vioja lakini anamuonea Aibu kaamua kumtumia katibu mkuu kumnyoosha kijanja

Uko sahihi Kiongozi tena kwa 100% kabisa kwani nilichoambiwa kinafanana moja kwa moja na hiki ulichokiandika hapa. RC Makonda kama hatojali basi taratibu sana aanze Kujiandaa Kisaikolojia kwani naanza Kuona kwa hizi Kauli tena za Kujiamini kabisa za Katibu Mkuu wake CCM Dkt. Bashiru Ally Kakurwa sasa ni rasmi kuwa hana muda mrefu Uongozini japo najua Watu wengi hawataamini hili kwakuwa tu wanasema kuwa RC Makonda ' hagusiki ' na ' anapendwa ' kuliko na aliyemteua hapo.
 
Mtukufu anajisikia vibaya jinsi Bashite anavyofanya vioja lakini anamuonea Aibu kaamua kumtumia katibu mkuu kumnyoosha kijanja

Mkuu hiyo sio kumnyoosha bali ni matayarisho ya daraja la uchaguzi 2020 ili kuwafurahisha wale wanaomchukia ndani ya chama na kuwafanya walegeze hasira zao kwa mwenyekiti wao, yote haya ya Bashiru kuanza kumsema vibaya jamaa yetu sio bure huenda hata yeye Mhusika kesha andaliwa na anajua kila nukta ya nini kitatokea baadae kabla ya tarehe kufika
 
Hizo kweli za uso! Makonda hadi kanywea utadhani watendaji wa kata wale anaowatukana kila siku.
Nashangaa hapo kashindwa kusema "usione tunafanana mashati lakini nakuzidi sana tuu, hivyo jichunge"
Au "katika watu wanakula laha nadhani mie naongoza"
View attachment 1196142
aise, jamaa kamchana chana hadi huruma.

Kamwambia ajiandae, naona anguko la Makonda linakuja kwa kasi ya kimbunga yuko under surveillance
 
Uko sahihi Kiongozi tena kwa 100% kabisa kwani nilichoambiwa kinafanana moja kwa moja na hiki ulichokiandika hapa. RC Makonda kama hatojali basi taratibu sana aanze Kujiandaa Kisaikolojia kwani naanza Kuona kwa hizi Kauli tena za Kujiamini kabisa za Katibu Mkuu wake CCM Dkt. Bashiru Ally Kakurwa sasa ni rasmi kuwa hana muda mrefu Uongozini japo najua Watu wengi hawataamini hili kwakuwa tu wanasema kuwa RC Makonda ' hagusiki ' na ' anapendwa ' kuliko na aliyemteua hapo.
Liko strategically hili suala Makonda mwakani anavuliwa ukuu wa mkoa, ili mkuu ajitwalie imani kwa watu kuwa kamgusa mwanae mpendwa kumbe ni picha linacheza jamaa tunakula nae cocktail kila siku hana wasiwasi kabisa..

Ndio kwanza anazidi kunenepa..
 
Isije ikawa wanacheza na akili zenu kuwapumbaza kwa kufanya kile mnac hokihusudu hasa ukiona muda uliobaki si wakuacha wengi Bali wengi wape, miaka ile anapigiwa kelele mbona alikuwa anatazama tu?
 
Back
Top Bottom