Hatimaye sasa ni Gabon mpaka Karume Stadium na siyo tena Gabon mpaka Kombe la dunia!

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
59,949
119,214
Nilitahadharisha humu mapema sana lakini matokeo yake.......
  • Nikatukanwa
  • Nikadhikiwa
  • Nikaonekana sijui kitu
  • Nikaambiwa siyo Mzalendo
  • Nikaambiwa Mimi Mkimbizi
  • Nikaambiwa nitaumbuka
  • Nikaambiwa nitakoma
Nayakumbuka maneno yangu ya Kiuchambuzi na ya Kiutaalam kabisa niliyoyasema ambapo nilisema tena kwa kujiamini kabisa kuwa Serengeti Boys haitaweza kufanya vizuri kwakuwa kwanza ina Kocha mbovu kuliko wote Bakari Shime pili Timu haikuwa na maandalizi ya Kisayansi zaidi tu ya Promo za Kijinga Kijinga za kutaka kujifutahisha na Tatu nikasema kuwa TFF na Malinzi yake wanaitumia hii Timu kama tu Mgongo wao wa kubakia Madarakani na chanzo chao cha kupiga Hela ila Timu isingefanya vizuri.

Nawashukuru sana Niger kwa kuweza kufanya kile ambacho wasiojua mpira walidhani kisingefanyika na hatimaye yale maneno ya GENTAMYCINE kuhusu Timu ya Serengeti Boys kutofanya vizuri sasa yametimia.

Sasa kauli mbiu imegeuka na imekuwa ni Gabooooooooooooooon....mpaka........Karume Stadium badala ya ile ya mwanzo ya Gaboooooooooooon.....mpaka......Kombe la Dunia. Yaani cha kuchekesha kabisa eti kuna Wabongo kabisa na akili zao walikuwa wakitegemea kabisa Serengeti Boys watafuzu Kombe la dunia nchini India mwezi November kwakuwa tu kila uchao wanadanganywa wa Wachambuzi wetu uchwara waliopo katika Radio zetu na Magazeti yetu kadhaa.

Watanzania tusikate tamaa na labda tu niishauri TFF na Waziri wa Michezo Harrison Mwakyembe wasikubali kutolewa hivi hivi na badala yake tuwakatie rufaa Niger kwani yawezekana na Wao pengine leo walichezesha Vijeba kwani walikuwa wanatiririka na kuserereka sana.

Nina imani kama tungewaachia tu Congo Brazzaville walishiriki wangefika mbali sana kwani walikuwa wameshajiandaa kwa muda mrefu na walikuwa na Kikosi imara mno kuliko Serengeti Boys ambayo mechi zake zote kuanzia zile za Kirafiki hadi za hili Kombe ilikuwa ikicheza tu kwa kubahatisha na kwamba Timu ilikuwa ni mbovu sijapata kuona.

Sasa ni Gabooooooooooooon.........mpaka..........Karume Stadium kudadadeki. Asante Niger kwani mlistahili kushinda / kuifunga Tanzania!
 
Sawa kujikwaa sio kuanguka..Tujipange upya lawama hazisaidii kipindi hiki
Kujipanga kila siku? Mimi mwenzenu Timu yetu ya mpira ikifungwa Hua naumia mno maana napata aibu mbele ya mkewangu, sisi kila siku Ni watu wa kuishia njiani Tu, kweli jamani?
 
Ila wamejitahidi vijana wetu pamoja na kutoka. Binafisi nawakubali hawa kuliko kaka zao.
Wakiendelezwa vizuri watatutoa
 
Waeudi zao tu sijaona lolote walilofanya huko Gabon, yaani friend mechi walicheza vizuri sana vichwa vikawajaaaa wakajiona wameshakuwa ma star

Nilivyowaona tu leo wanaingia pale Uwanjani hasa vyumbani huku wakiwa wanashangilia kizembe kizembe na kuimba nyimbo za Mafirauni fulani hivi wa Bongo Fleva nikajua mapema tu kuwa tayari nuksi imeshatukuta na hatuna chetu. Halafu kuna Vichezaji fulani hivi viwili vya Serengeti Boys vilikuwa vimeshaanza kujiona kama vile akina Messi na Ronaldo kwa kuwa na mapozi ya hovyo hovyo na kuota majipu ( kuanza kuringa na kujisikia ) kana kwamba wameshafika Kombe la dunia.

Warudi tu kwakweli tuendelee tu kula nao bamia, kisamvu, matembele yetu na maharage kwani ndicho tunachokiweza na siyo mpira. Mnatusumbua tu kila siku katika Radio na Tv kuwa tuwachangieni halafu tunajinyima mnaenda huko mnaishia tu kumbwela mbwela. Tena TFF na Malinzi kesho asubuhi tu nakuja Karume hapo Ofisi zenu za TFF kuchukua Pesa yangu ya mchango kwani nilitoa ili Timu ifanikiwe na siyo iishie njiani kama hivi. Kesho nataka Pesa yangu tafadhali!
 
Sawa kujikwaa sio kuanguka..Tujipange upya lawama hazisaidii kipindi hiki

Tuache tuliotoa michango yetu tulalamike na Wewe usiyetoa chochote baki tu na hizo kauli zako za matumaini hewa. Utafungwaje na Niger? Tena usizidi kututia hasira Mkuu kwani hivi Vitoto vyetu vya Serengeti Boys vilishaanza kuota majipu ( kuringa ) wakati hata bado havijajuwa vizuri principles za mpira. Vingine vimejichora Matatoo mara vingine vimenyoa viduku na kuna kamoja nimekaona kamejipaka sana Powder na Kabishoo mno.

Bora tu walivyofurumushwa na kama ikiwezekana Rais wa TFF Jamal Malinzi ajiuzuru tu au Uchaguzi huu ujao asishiriki na amuachie Mzee Mtemi Ramadhani ( Mchezaji wa zamani wa Simba SC ) awe Rais wa TFF kwani pengine anaweza akatufikisha mbali sana Tanzania kuliko Yeye.

TFF ya Rais Jamal Malinzi ni bure kabisa! Asanteni sana Niger kwa kututoa / kutufurumusha Tanzania. Sasa ni Gaboooooooooon......mpaka....................Karume Stadium kudadadeki!
 
Nimefurahi kinyama bora warudi maana mwakyembe alishawageuza mtaji kisiasa pumbaaafu

Mkuu nadhani hujanizidi Mimi kwa kufurahi kutolewa Kwetu. Manake sasa ilikuwa Kero humu mitaani na katika Maredio kwani kila mara tu utasikia Gaboooooooon.....mpaka......Kombe la dunia na bila shaka kuanzia Kesho tutasikia kauli mbiu mpya ya Gaboooooooon........mpaka........Karume Stadium.

Wewe Timu hata bado haijawa na Mafanikio tayari Kamati Kibao zimeundwa kumbe Kamati zenyewe ni za kupiga / kula tu Pesa.
 
Nilivyomsikia Bakari Shime Jana akisema Niger watakuja kwa nia ya kushambulia kwa nguvu na sisi tutacheza kwa nidhamu kuzuia na kushambulia kwa kustukiza nikajua game ya Leo hawachomoki

Sijawahi kuona Kocha mbovu na Msanii kama huyo. Kazi ni kupenda tu ushirikina na alinikera mno alipokuwa anaifundisha Ruvu ambapo aliibania Simba SC na akaiachia Yanga FC.
 
Wamecheza vizuri, goal keeper tu ndiye aliidharau mpira wa adhabu ule ukazaa goli.
Kwa hakika hii timu ndio ya kuiandaa kupikwa ili iwe timu ya taifa ya wakubwa.
 
Sijawahi kuona Kocha mbovu na Msanii kama huyo. Kazi ni kupenda tu ushirikina na alinikera mno alipokuwa anaifundisha Ruvu ambapo aliibania Simba SC na akaichia Yanga FC.
Alaaaaa kuuuuumbe hp ndio nlipokuwa napatafuta yaani nlijua tu we jamaa lazma chanzo kiwe yanga ple juu umesema uongozi tumpe fala gani cjui mchezaji wa zamani wa simba sikatai mi mwenyewe mmoja wpo natamani hata kesho malinzi atuachie soka letu ila c kwa style yko hii unaleta ushabiki sana ooh Shime kocha mbovu kumbe tatzo alishawahi kuwabania akawaachia yanga unaacha kuchambua kisomi unaleta unazi malinzi atoke aje mtu neutral hatutaki usimba na uyanga!
 
Alaaaaa kuuuuumbe hp ndio nlipokuwa napatafuta yaani nlijua tu we jamaa lazma chanzo kiwe yanga ple juu umesema uongozi tumpe fala gani cjui mchezaji wa zamani wa simba sikatai mi mwenyewe mmoja wpo natamani hata kesho malinzi atuachie soka letu ila c kwa style yko hii unaleta ushabiki sana ooh Shime kocha mbovu kumbe tatzo alishawahi kuwabania akawaachia yanga unaacha kuchambua kisomi unaleta unazi malinzi atoke aje mtu neutral hatutaki usimba na uyanga!

Gabooooooooooooon............mpaka...........................Karume Stadium.
 
Back
Top Bottom