Hatimaye ripoti ya tuhuma za rushwa ya Wabunge yatua kwa Spika | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hatimaye ripoti ya tuhuma za rushwa ya Wabunge yatua kwa Spika

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mgomba101, Oct 14, 2012.

 1. m

  mgomba101 JF-Expert Member

  #1
  Oct 14, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 1,788
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Spika wa Bunge, Anne Makinda amepokea taarifa ya uchunguzi kuhusu tuhuma zilizowahusu Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini na baadhi ya Wabunge ya kujihusisha na vitendo vya rushwa wakati wa mjadala wa Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini (2012/2013).

  Ripoti hiyo inafuatia Spika Makinda kuunda Kamati ndogo ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge kuchunguza tuhuma hizo wakati wa Mkutano wa Nane wa Bunge uliofanyika Juni – Agosti, 2012.

  Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Bunge jana kwa vyombo vya habari, ilisema kuwa kwa mujibu wa Kanuni za Kudumu za Bunge (2007), Spika atatoa mwongozo kuhusu utaratibu wa kufuata kuhusu uwasilishaji wa Taarifa hiyo Bungeni ambapo Spika akatoa uamuzi ama Kamati kuwasilisha Taarifa hiyo Bungeni.

  Kamati hiyo ndogo ilikamilisha kazi yake kama ilivyoelekezwa kwenye Hadidu za Rejea na kukabidhi Taarifa ya Uchunguzi huo kwa Spika wa Bunge.

  “Spika atatoa taarifa ya kukamilika kwa uchunguzi huo Bungeni wakati wa Mkutano wa Tisa wa Bunge unaotarajia kuanza Oktoba 30,” ilisema taarifa hiyo.
   
 2. m

  mgomba101 JF-Expert Member

  #2
  Oct 14, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 1,788
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Tusubili mkutano wa tisa ili kujua mbivu na mbichi.Napendekeza hatua kali zichukuliwe kwa wale watakaobainika.
  kamati ya POAC na ile ya nishati na madini zivunjwe kwa sababu baadhi ya wajumbe wake wanatuhumiwa kupokea rushwa na kutaka kumsafisha Mhando wa tanesco.
   
 3. Tango73

  Tango73 JF-Expert Member

  #3
  Oct 14, 2012
  Joined: Dec 14, 2008
  Messages: 1,678
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 135
  Kumbuka Huyu Anna Makinda anajenga Ghorofa pale Kijitonyama mabatini. Hii ripoti haina tofauti na ile repoti ya kumtia hatiani Philimon Luhanjo na wenzake ilivyo watered down ,pale alipomtetea David Gairo. Sasa hiyo repoti ili iwe wateredown, itaundiwa tume ndani ya tume na kuhakikisha kuna tume ya kujua ulkweli wa tume. halafu kuna tume ya maadili ili kuona kama kweli kuna tume kweli. Hapo utajikuta 2015 uchaguzi ushapita. wewe ngoja tuu uone maudhi mengine kutoka kwa wansiasa wetu walio lelewa kikomunisti. haya ndiyo maudhi wanayopyapata warussi mpaka leo, jinsi wakomunisti wajanja wanavyoiba mabilion ya pesa za mafuta na kujilimbikizia miradi mikuu.
   
 4. Tango73

  Tango73 JF-Expert Member

  #4
  Oct 14, 2012
  Joined: Dec 14, 2008
  Messages: 1,678
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 135
  Kumbuka Huyu Anna Makinda anajenga Ghorofa pale Kijitonyama mabatini. Hii ripoti haina tofauti na ile repoti ya kumtia hatiani Philimon Luhanjo na wenzake ilivyo watered down ,pale alipomtetea David Gairo. Sasa hiyo repoti ili iwe wateredown, itaundiwa tume ndani ya tume na kuhakikisha kuna tume ya kujua ulkweli wa tume. halafu kuna tume ya maadili ili kuona kama kweli kuna tume kweli. Hapo utajikuta 2015 uchaguzi ushapita. wewe ngoja tuu uone maudhi mengine kutoka kwa wansiasa wetu walio lelewa kikomunisti. haya ndiyo maudhi wanayopyapata warussi mpaka leo, jinsi wakomunisti wajanja wanavyoiba mabilion ya pesa za mafuta na kujilimbikizia miradi mikuu.
   
 5. Father of All

  Father of All JF-Expert Member

  #5
  Oct 14, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 3,093
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Hovyo, spika mwenyewe ameingia kwa njia hiyo hiyo ana nini cha mno? Haya endeleeni kujipa matumaini kwa kutegemea huyu mama aliyechaguliwa si kwa sifa zaidi ya uke wake kuwa atawasaidia au kutenda haki. Yeye hana tofauti na robot. Watakachosema waliomsimika ndicho hicho hicho atafanya.
   
 6. andishile

  andishile JF-Expert Member

  #6
  Oct 14, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 1,430
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  tunaisubiria
   
 7. N

  Naytsory JF-Expert Member

  #7
  Oct 14, 2012
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 1,590
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Sina hakika kama hatawalinda kwa sababu maovu mengi ameyafunika kulinda maslahi ya serikali na chama chake. Hana huruma na maslahi ya Taifa amejaa ushabiki wa kichama.
   
 8. Amiliki

  Amiliki JF-Expert Member

  #8
  Oct 14, 2012
  Joined: May 6, 2011
  Messages: 2,087
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Sinema ile ile, wamembadilisha Starring tu.
   
 9. mchemsho

  mchemsho JF-Expert Member

  #9
  Oct 14, 2012
  Joined: Jun 8, 2011
  Messages: 3,158
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  kwa huyu ma'am speaker tutasubiri sana,labda iwe imechakachuliwa.
   
 10. babalao 2

  babalao 2 JF-Expert Member

  #10
  Oct 14, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,217
  Likes Received: 1,270
  Trophy Points: 280
  Hili jambo kwa mtu makini lazima akubali. Hivi sasa tumeshuhudia chaguzi zinazoelekea ukingoni ndani ya ccm zilivyotawaliwa na rushwa na kupelekea majeruhi wengi kubaki wakilalama.
  Wengi walioshindwa na baadhi walioshinda kwa pamoja wametoa onyo kwa chama chao kinapoelekea kwani Rushwa imegandamana na hakuna jasiri wa kukemea sababu kila mmoja kwa alinufaika na mfumo uliopo hivyo kupelekea nafasi ya BABA WA TAIFA kuwa wazi mpaka leo.
  Wengi wamepiga kelele kutenganisha rushwa, Ufisadi na kupeana vyeo kunakopelekea ccm kudhoofu mbele ya Wapinzani wao kukaa kmya nao wakisubiri matokeo yatakuaje.
  Kumbe kumtoa KOBE GAMBA NI KUMTOA UHAI WAKE.
  KUONDOA RUSHWA NA UFISADI CCM NI MWANZO WA KIFO CHAKE.
  Hili walilotuonyesha kwenye chaguzi zao ni MWANGWI WA YATAKAYOJIRI 2015.
   
 11. m

  mgomba101 JF-Expert Member

  #11
  Oct 14, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 1,788
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  CCM ni marehemu mtalajiwa.
   
 12. T2015CCM

  T2015CCM JF-Expert Member

  #12
  Oct 14, 2012
  Joined: Sep 13, 2012
  Messages: 7,924
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Baada ya waziri wa nishati na madini prof muhongo kuwatuhumu wabunge kuwa walipokea rushwa na hatimaye spika kuunda kamati ya uchunguzi,kamati hiyo imetoa matokeo na kuonyesha kuwa wabunge ni wasafi,hawakuhongwa na kupendekeza kwamba waziri mhongo afute kauli yake mbele ya bunge na katibu mkuu wake eliakim maswi awajibishwe kisheria. My take..wabunge wamejichunguza na hatimaye wamejisafisha ili kulinda maslahi ya wabunge.
   
 13. K

  Kanundu JF-Expert Member

  #13
  Oct 14, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 891
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Rushwa ndani ya CCM ni sawa na MSHIPA NA DAMU. Ukivitenganisha ni kifo!!!!!!!!!!!
   
 14. C

  Concrete JF-Expert Member

  #14
  Oct 14, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 3,607
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  Mkuu funguka vizuri Zaidi, kwa mfano
  1/Hizi ni tetesi au confirmed news?
  2/Chanzo cha taarifa hii?
  3/Wabunge hao ni wakina nani?
  4/Ni vipi hasa hawajahusika?
   
 15. p

  politiki JF-Expert Member

  #15
  Oct 14, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,356
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  jamani rushwa haiundiwi kamati na wale wa aina ileile, swala la rushwa ni kosa la jinai inabidi lishughulikiwe na watu wenye
  uzoefu na maswala ya rushwa. tunaambiwa watu ni sawa mbele ya sheria sasa inakuwaje mimi nikifanya kosa la rushwa takukuru watanifuata mpaka chumbani na kunifikisha mahakamani wakati wengine wanaundiwa kamati.usawa huko wapi??
   
 16. T2015CCM

  T2015CCM JF-Expert Member

  #16
  Oct 14, 2012
  Joined: Sep 13, 2012
  Messages: 7,924
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  mkuu hizi ni taarifa za kweli zilizothibitishwa sio tetesi.baadhi ya wabunge ni sara msafiri na selemani zedi na munde tambwe
   
 17. T2015CCM

  T2015CCM JF-Expert Member

  #17
  Oct 14, 2012
  Joined: Sep 13, 2012
  Messages: 7,924
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Pia kamati imemkuta na hatia mh.joseph selasini mb wa rombo kwa kuwatuhumu baadhi ya wabunge kuhongwa na makampuni ya mafuta ili kuyatetea kuhusu zabuni za mafuta,kwamba hana ushahidi
   
 18. T2015CCM

  T2015CCM JF-Expert Member

  #18
  Oct 14, 2012
  Joined: Sep 13, 2012
  Messages: 7,924
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Kamati imependekeza kuwa joseph selasini apewe adhabu ya kutohudhuria vikao kumi mfululizo kuanzia mkutano wa tisa wa bunge ili iwe onyo kwa wengine
   
 19. babykailama

  babykailama JF-Expert Member

  #19
  Oct 14, 2012
  Joined: Mar 5, 2012
  Messages: 241
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Hapo ndipo Spika unaweza kuprove kwamba wewe na kamati yako si wachakachuaji kwa kutamka waziwazi wote waliohusika na rushwa na hatua kali zichukuliwe dhidi yao Wabunge wachovu wasiostahili kuwepo mjengoni. Taarifa ya ufisadi huu ilieleweka kila mahala nchini na nje ya nchi kama ilivyokuwa inajadiliwa na BBC hivi karibuni.

  Watu walianza kuonya hapa kuwa hata ndani ya kamati kuna watu kama Mh. G. Blandes ambaye yeye mwenyewe si msafi na ana ubabaishaji mkubwa sana hata katika uchaguzi wake kutoka kwao. Ukweli kuna habari za kuaminika Blandes alijitahidi kukutana na kigeugeu Mh.Zitto na kumpa taarifa hiyo kwa siri ambayo ilikuwa kama wembe kwa Zitto na wamejitahidi sana kutafuta namna ya kuichakachua. Zitto kama kawaida yake alikimbilia gazeti kama mlivyosikia na kujaribu kuwaondolea watu fikra na kweli iliyoonekana ya mafisadi hata ndani ya Bunge letu. Hivyo watz wanakusubiri sana Spika kuona utakavyosimama dhidi ya ufisadi au kuulinda ufisadi kama wakati wa Jairo alivyotetewa wakati ameshanyea kazi.

  Zaidi ya yote wananchi wanataka kuona akina Mhando na group lake la wabunge waliochafua bunge kama dada yetu aliimba 'wanawake na maendeleo'kumbe sasa nimeona wimbo wake halisi kivitendo ni mwanamke ni kujirahisi kwa mafisadi'.

  Tutakutana hapo Bungeni!
   
 20. w

  wa hapahapa JF-Expert Member

  #20
  Oct 14, 2012
  Joined: Aug 22, 2012
  Messages: 5,546
  Likes Received: 1,599
  Trophy Points: 280
  nasubiri ikiwakilishwa Bungeni ...natumaini mambo yatakuwa ukweli na uwazi na majina ya wahusika,lakini habari za kuformat kwamba et mheshimiwa apinge kauli yake kwa kuwa habari sizo za kweli, kama walivyomnukuu wengi ......... sasa raia hawataki maigizo wanataka mbivu na mbichi....
   
Loading...