Sam Gidori
Senior Member
- Sep 7, 2020
- 165
- 414
Baada ya kusubiriwa kwa miaka miwili, hatimaye ripoti ya Shirika la Ujasusi la Marekani kuhusu kuuawa kwa Jamal Khashoggi imeachiwa siku ya Ijumaa ikionesha kuhusika kwa uongozi wa Saudi Arabia katika tukio hilo.
Ripoti hiyo yenye kurasa nne imemtaja Mwanamfalme wa Saudi Arabia, Mohammed Bin Salman kuhusika moja kwa moja kwa kutoka amri ya kuuawa kwa Khashoggi kutokana na ushawishi wake wa kimaamuzi ndani ya Ufalme na kuhusika kwa watu wake wa karibu pamoja na walinzi wake katika tukio hilo, ikiwataja waliohusika katika tukio hilo.
Ripoti hiyo imemtaja MBS kama muungaji mkono matumizi ya nguvu katika kuwanyamazisha wakosoaji wake hata nje ya mipaka ya Ufalme, akiwamo Khashoggi.
"Tangu mwaka 2017, Mwanamfalme amekuwa na mamlaka ya moja kwa moja katika vyombo vya usalama na vya kiintelijensia ndani ya Ufalme, hivyo tukio kama hilo lisingeweza kutendeka bila kibali cha Mwanamfalme," ripoti hiyo ilieleza, ikongeza kuwa MBS alimuona Khashoggi kama 'tishio kwa Ufalme.'
Wizara ya Mambo ya Kigeni ya Saudi Arabia imekanusha kuhusika na kuuawa kwa Khashoggi ikisema kuwa haikubaliani kabisa na uchambuzi wa uongo kuhusu uongozi wa Ufalme, ikisema ripoti hiyo inahusisha taarifa za kupotosha.
Maafisa wa Ikulu ya Marekani wamesema kuwa uongozi wa Biden utaamua hapo baadaye hatua zinazofaa kuchukuliwa dhidi ya Ufalme kufuatia kuuawa kwa Khashoggi baada ya ripoti hiyo kutolewa.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani amejibu ukanushaji wa Saudi Arabia, akisema ripoti hiyo "inajieleza yenyewe," na kuwa uongozi wa Biden "unajaribu kuleta uwazi na kuwashirikisha Wamarekani kile tunachokifahamu."
Mwaka jana, mmoja wa watoto wa Khashoggi, Salah, aliandika katika mtandao wa kijamii wa Twitter kuwa familia yake imewasamehe waliohusika katika mauaji ya baba yao.
Hata hivyo, inadaiwa kuwa Saudi Arabia iliwapa watoto wanne wa Khasoggi kila mmoja nyumba yenye thamani ya dola milioni moja, na kitita cha fedha kama sehemu ya fidia kwa kuuawa kwa baba yao.
Utawala wa Rais Donald Trump ulizuia kuwekwa hadharani kwa ripoti hiyo licha ya Baraza la Congress kupitisha sheria kutaka kuwepo kwa uwazi katika uchunguzi wa tukio hilo. Kashoggi, mwandishi wa habari wa gazeti la Washington Post na mkosoaji wa serikali ya Saudi Arabia, aliuawa ndani ya ubalozi wa Saudi Arabia mjini Istanbul, Uturuki, Octoba mwaka 2018.
Chanzo: Al Jazeera
Isome ripoti hiyo: 👇👇👇