Hatimaye Ripoti ya Intelijensia ya Marekani kuhusu kuuawa kwa Khashoggi yatolewa, MBS atajwa kuhusika

Sam Gidori

Verified Member
Sep 7, 2020
80
150
Baada ya kusubiriwa kwa miaka miwili, hatimaye ripoti ya Shirika la Ujasusi la Marekani kuhusu kuuawa kwa Jamal Khashoggi imeachiwa siku ya Ijumaa ikionesha kuhusika kwa uongozi wa Saudi Arabia katika tukio hilo.

Ripoti hiyo yenye kurasa nne imemtaja Mwanamfalme wa Saudi Arabia, Mohammed Bin Salman kuhusika moja kwa moja kwa kutoka amri ya kuuawa kwa Khashoggi kutokana na ushawishi wake wa kimaamuzi ndani ya Ufalme na kuhusika kwa watu wake wa karibu pamoja na walinzi wake katika tukio hilo, ikiwataja waliohusika katika tukio hilo.

Ripoti hiyo imemtaja MBS kama muungaji mkono matumizi ya nguvu katika kuwanyamazisha wakosoaji wake hata nje ya mipaka ya Ufalme, akiwamo Khashoggi.

"Tangu mwaka 2017, Mwanamfalme amekuwa na mamlaka ya moja kwa moja katika vyombo vya usalama na vya kiintelijensia ndani ya Ufalme, hivyo tukio kama hilo lisingeweza kutendeka bila kibali cha Mwanamfalme," ripoti hiyo ilieleza, ikongeza kuwa MBS alimuona Khashoggi kama 'tishio kwa Ufalme.'

Wizara ya Mambo ya Kigeni ya Saudi Arabia imekanusha kuhusika na kuuawa kwa Khashoggi ikisema kuwa haikubaliani kabisa na uchambuzi wa uongo kuhusu uongozi wa Ufalme, ikisema ripoti hiyo inahusisha taarifa za kupotosha.

Maafisa wa Ikulu ya Marekani wamesema kuwa uongozi wa Biden utaamua hapo baadaye hatua zinazofaa kuchukuliwa dhidi ya Ufalme kufuatia kuuawa kwa Khashoggi baada ya ripoti hiyo kutolewa.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani amejibu ukanushaji wa Saudi Arabia, akisema ripoti hiyo "inajieleza yenyewe," na kuwa uongozi wa Biden "unajaribu kuleta uwazi na kuwashirikisha Wamarekani kile tunachokifahamu."

Mwaka jana, mmoja wa watoto wa Khashoggi, Salah, aliandika katika mtandao wa kijamii wa Twitter kuwa familia yake imewasamehe waliohusika katika mauaji ya baba yao.
Hata hivyo, inadaiwa kuwa Saudi Arabia iliwapa watoto wanne wa Khasoggi kila mmoja nyumba yenye thamani ya dola milioni moja, na kitita cha fedha kama sehemu ya fidia kwa kuuawa kwa baba yao.

Utawala wa Rais Donald Trump ulizuia kuwekwa hadharani kwa ripoti hiyo licha ya Baraza la Congress kupitisha sheria kutaka kuwepo kwa uwazi katika uchunguzi wa tukio hilo. Kashoggi, mwandishi wa habari wa gazeti la Washington Post na mkosoaji wa serikali ya Saudi Arabia, aliuawa ndani ya ubalozi wa Saudi Arabia mjini Istanbul, Uturuki, Octoba mwaka 2018.

Chanzo: Al Jazeera

Isome ripoti hiyo: 👇👇👇
 
Attachments

  • File size
    211.2 KB
    Views
    11

igwee frm anambra

JF-Expert Member
May 16, 2015
681
1,000
Hii inamaanisha MBS hawezi tena kuwa mfalme wa Saudi Arabia in case baba yake king Salman anafariki, .... why? Existence ya Saudi Arabia inategemea ulinzi wa US kwa 100%..... huyu kijana anakurupuka sana ktk maamuzi yake , nafikiri ni utoto+ ujinga na roho mbaya, je ataweza kuwatunishia msuli waamerika? NO hawezi jaribu ' mbabe wa gulf IRAN ataifuta kwenye ramani ya Dunia over night.
He is caught between rock and hard place.

Trump alipenda sana hela zake (ambazo ni nyingi)
Biden amesema hawezi ongea naye, sio level yake ktk madaraka.
 
Scars

JF-Expert Member
Apr 8, 2017
16,071
2,000
kama sikosei kuna makala nilisoma zikimuonesha mfalme wa saudia akikiri kuhusika na mauaji ya khashog now how?
 
Chrisvern

JF-Expert Member
Sep 8, 2011
2,489
2,000
Hii inamaanisha MBS hawezi tena kuwa mfalme wa Saudi Arabia in case baba yake king Salman anafariki, .... why? Existence ya Saudi Arabia inategemea ulinzi wa US kwa 100%..... huyu kijana anakurupuka sana ktk maamuzi yake , nafikiri ni utoto+ ujinga na roho mbaya, je ataweza kuwatunishia msuli waamerika? NO hawezi jaribu ' mbabe wa gulf IRAN ataifuta kwenye ramani ya Dunia over night.
He is caught between rock and hard place.

Trump alipenda sana hela zake (ambazo ni nyingi)
Biden amesema hawezi ongea naye, sio level yake ktk madaraka.
Hapa kazi ipo ktk huu utawala wa Biden.
 
Gebreyesus

JF-Expert Member
Jan 31, 2018
7,585
2,000
Hii inamaanisha MBS hawezi tena kuwa mfalme wa Saudi Arabia in case baba yake king Salman anafariki, .... why? Existence ya Saudi Arabia inategemea ulinzi wa US kwa 100%..... huyu kijana anakurupuka sana ktk maamuzi yake , nafikiri ni utoto+ ujinga na roho mbaya, je ataweza kuwatunishia msuli waamerika? NO hawezi jaribu ' mbabe wa gulf IRAN ataifuta kwenye ramani ya Dunia over night.
He is caught between rock and hard place.

Trump alipenda sana hela zake (ambazo ni nyingi)
Biden amesema hawezi ongea naye, sio level yake ktk madaraka.
Kwanini mnatumia neno MBs kumuadress mwanamfalme? Maana ya MBs ni Nini?
 
permanides

JF-Expert Member
May 18, 2013
5,425
2,000
Kuna mafuta pale !! Kinachofuata ni kumuua uyo mwanamfalme kitechnolojia drone za CIA zitafanya yke
Saudi Arabia ni mshirika muhimu mno kwa USA katika biashara ya mafuta na kumzibiti au kupambana na vitisho vya Iran hapo Middle East. Ili kudeal vizuri na Iran,unahitaji Israel na Saudi Arabia imara. Hivyo pengine USA anataka kuonyesha kuwa Saudi Arabia ni mwovu na atuhumiwe ila USA ajifanye kuonyesha solidarity nae, licha ya uovu wake.
 
Igneous

Member
Jan 21, 2021
21
45
Saudia ni mshirika muhimu sana was U.S.A mashariki ya kati. Marekani alichokifanya ni unafki tu kusema kwamba hakubaliani na Saudia, kabla ya uchunguzi wao hata mawe na miti vilijua kwamba Kashogh kauwawa kwa maagizo kutoka mamlaka za juu za utawala wa kifalme was Saudia. Wanajuana na wanaelewana.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom